Kamishna
wa Bajeti kutoka Wizara Fedha Bw. John Cheyo akitoa ufafanuzi kwa
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu taarifa za
upotoshaji zilizoripotiwa na vyombo vya habari hapa nchini kuwa hazina
yakauka, taarifa hizo ni za upotoshaji kwani mfumo wa Serikali wa bajeti
unaiwezesha Serikali kupanga vipaumbele vya matumizi kulingana na
bajeti ilivyopangwa ambapo fedha zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa
Serikali ndizo hutumika. Kushoto ni Kamishna msaidizi wa Bajeti Bw.
Immanuel Tutuba na kulia ni Mkurugenzi msaidizi Idara ya habari Maelezo
Bw. Vicent Tiganya.
Kamishna
wa Bajeti kutoka Wizara Fedha Bw. John Cheyo akizungumza na waandishi
wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu kubadilishwa kwa matumizi ya
Fedha za Serikali ambazo zitaelekezwa kwenye shughuli zitakazowagusa
wananchi ikiwemo uboreshaji wa sekta ya elimu ambapo awali fedha hizo
zilipangwa kutumika katika sherehe za Uhuru na shughuli zisizo za
lazima. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Idara ya Habari. (MAELEZO) Bw.
Vicent Tiganya.
Kamishna
msaidizi wa Bajeti Bw.Immanuel Tutuba akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa
habari kuhusu namna Serikali inavyokusanya mapato yake na kuyaingiza
katika mfuko mkuu wa Serikali ili yaweze kutumika katika utekelezaji wa
bajeti ya Serikali. Kulia kwake ni Kamishna wa Bajeti Bw. John Cheyo na
kushoto ni msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Fedha na
vyombo vya habari ambapo Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara hiyo Bw. John
Cheyo alitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Serikali
kulingana na mipango iliyowekwa katika kuwahudumia wananchi.
Kamishna
msaidizi wa Bajeti Bw.Immanuel Tutuba akisisitiza jambo kwa waandishi
wa habari leo jijini Dar es salaam .Kulia nia Msemaji wa Wizara ya Fedha
Bi. Ingiahedi Mduma.
(Picha na frank Mvungi- Maelezo)
(Picha na frank Mvungi- Maelezo)
……………………………………………………………………………………………………
Na Jovina Bujulu-Maelezo
Dar es Salaam
Serikali imekanusha taarifa
zinazosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Rais mstaafu wa awamu
ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa amekomba fedha hazina na kuiacha
Serikali bila fungu lolote.
Hayo yamesemwa jijini dare es
salaam na Kamishina wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha Bwa. John Cheyo
huku akiwataka wananchi kupuuza habari hiyo kwani hazina ukweli wowote.
“Hazina inazo pesa za kutosha
na tunajivunia kufanya uchaguzi wa mwaka huu, kununua mashine za BVR
kwa kutumia pesa za watanzania bila kutegemea msaada wowote kutoka nje
ya nchi na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka huu”
alisema Bwa. Cheyo.
Pia aliongeza kuwa serikali
imeendelea kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa
bomba la gesi ambalo limekamilika hivi karibuni, vinu vya kuchakata gesi
na ujenzi wa barabara nchini.
Aliendelea kusema kwamba mfumo
wa serikali wa bajeti unaiwezesha serikali kupanga vipaumbele vya
matumizi kulingana na bajeti ilivyopangwa ambapo fedha zinazokusanywa
kupitia mfuko mkuu wa serikali ndizo hutumika.
Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge
kwa kipindi cha 2015-2016 ni shilingi Trilioni 22.5 na bajeti hiyo
inatengenezewa mpango wa makusanyo na matumizi kwa kulipia mishahara ya
wafanyakazi na miradi mbalimbali iliyoidhinishwa.
Pia katika matumizi mengine
bajeti hiyo inalipia chakula cha wanafunzi, mikopo ya wanafunzi elimu ya
juu, ununuzi wa dawa na vifaa tiba na chakula cha hifadhi ya taifa.
No comments:
Post a Comment