Wednesday, November 4, 2015

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS   Telephone: 255-22-2114512, 2116898  E-mail: ikulucommpress@googlemail.com Website : www.ikulu.go.tz                Fax: 255-22-2113425     PRESIDENT'S OFFICE,       STATE HOUSE,               1 BARACK OBAMA ROAD,    11400 DAR ES SALAAM. Tanzania. TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI       Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameamua na ameitangaza kesho, Alhamisi, Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa Sikukuu na siku ya mapumziko.      Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne na kuingizwa madarakani Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.      Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo Jumatano, Novemba 4, 2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Yohana Sefue, Rais Kikwete ametoa uamuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyo nayo chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa. Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM.   4 Novemba, 2015

No comments: