Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti akifafanua
jambo wakati akizungumza waandishi wa habari kuhusu kuvunjika kwa uzio
wa jengo la mfuko huo linalojengwa mkoani Mbeya kutokana na kukumbwa na
mvua na upepo mkali, amesema jengo hilo liko salama kabisa ila uzio
unaosaidia kuwakinga wajenzi ndiyo ulioanguka kutokana na upepo huokulia
ni Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF,Bw Rehani Athuman.
Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti akifafanua
jambo wakati akizungumza waandishi wa habari kuhusu kuvunjika kwa uzio
wa jengo la mfuko huo linalojengwa mkoani Mbeya.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF,Bw Rehani Athuman akionyesha mchoro wa jengo hilo kwa waandishi wa habari, kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti
…………………………………………………………………………………………
Utangulizi:
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) hivi sasa unaendelea na ujenzi wa majengo katika mikoa mbalimbali
nchini, kwa lengo la kujitosheleza kwa majengo ya ofisi na kukidhi
mahitaji ya wanachama wake na wadau wengine.
Moja ya mikoa ambayo inaendelea
na ujenzi huo ni Mbeya, ambako Mfuko unajenga jengo la ghorofa kumi na
mbili litakalokuwa na nafasi za ofisi na huduma nyingine ndani yake.
Tukio la Kuanguka kwa jukwaa:
Wakati shughuli hizo za ujenzi
zinaendelea, jana mchana katika hali isiyotarajiwa mvua iliyoambatana na
upepo mkali ilinyesha mjini Mbeya. Upepo na mvua hizo vilisababisha
kuanguka kwa jukwaa la jengo hilo na kutua juu la paa la jengo la ofisi
ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Mbeya. Kuanguka kwa jukwaa
hilo hakukuwa na madhara yoyote kwa maisha ya binadamu, kwa maana kuwa
hakuna mtu aliyepoteza maisha au kupata majeraha. Hata hivyo tukio hilo
lilisababisha taharuki kwa wafanyakazi wapatao hamsini waliokuwemo ndani
ya jengo hilo na hivyo kusababisha kazi kusimama kwa muda. Aidha
tathmini ya awali iliyofanyika katika paa la jengo la TANESCO
lililoangukiwa na jukwaa hilo inaonyesha kuwa paa hilo ilipata hitilafu
ndogo ambayo itafanyiwa marekebisho kwa gharama za Mkandarasi anayejenga
jengo la NHIF.
Hatua za kisualama zilizochukuliwa:
Kama sheria za ujenzi
zinavyoagiza, kabla ya kuanza kwa ujenzi wa jengo hilo Mkandarasi
alishajenga uzio kuzunguka jengo zima ili kuhakikisha kuwa shughuli za
ujenzi hazileti madhara kwa wapita njia au ofisi zilizo jirani. Umakini
wa Mkandarasi huyo katika kuzingatia taratibu za tahadhari katika
shughuli za ujenzi, umewezesha jengo hilo la ghorofa kumi na mbili
kufikia hatua nzuri ya ujenzi bila madhara yoyote kwa wajenzi wenyewe,
wapita njia au ofisi za jirani.
Aidha kufuatia tukio la Jumatatu
02/11/2015, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeshamwandikia Mkandarasi
anayeendelea na ujenzi katika jengo hilo kuhakikisha kuwa uzio
unaozunguka jengo zima unaimarishwa zaidi hususani wakati huu
tunapokaribia kipindi cha mvua za masika ili kuepuka uwezekano wa
madhara yoyote kwa binadamu wakati shughuli za ujenzi zinaendelea.
Namna Habari ilivyoripotiwa:
Tunapenda kuufahamisha umma
kwamba habari zilizoripotiwa jana na baadhi ya vyombo vya habari kwamba
jengo la NHIF mkoani Mbeya limeporomoka, zilipotosha ukweli wa tukio
hilo, kwani kilichoporomoka siyo jengo, bali ni jukwaa.
Tunapenda kusisitiza kuwa tukio
hilo limesabishwa na mvua kubwa na upepo uliovuma katika mji wa Mbeya,
wala siyo uzembe wa Mkandarasi anayejenga jengo hilo.
Wito kwa Wanachama wa NHIF:
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
unawaomba wanachama na wadau wake nchini kote waendelee kuwa watulivu na
kuvuta subira kwani changamoto ya ufinyu wa ofisi katika mikoa itakuwa
imepatwa ufumbuzi baada ya kukamilika kwa ujenzi wa majengo ya
unaoendelea hivi sasa katika mikoa mbali mbali nchini.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu,
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
No comments:
Post a Comment