Wednesday, May 10, 2017

Anogewa na mume kutoka Boko Haram, agoma kurudi nyumbani

Nigeria.
Mmoja wa wasichana wa Chibok waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria ameshangaza wengi baada ya kuamua kubaki na mwanaume wa kundi hilo anayedai ni mumewe baada ya yeye na wenzake kuachiwa huru Jumamosi iliyopita.


Msemaji wa Ikulu, Nigeria, Garba Shehu amenukuliwa akisema kuwa wasichana 83 walitarajiwa kuachiliwa huru lakini mmoja wao amesema; “Hapana nafurahi nilipo, nimepata mume.”


Kutokana na uamuzi wa binti huyo, kundi la Boko Haram liliwaachia huru wasichana 82 baada ya mazungumzo kati yao na shirika la ICRC.
Wapiganaji hao wanadaiwa kuwazuia zaidi ya wasichana 100 kati ya 276 waliowateka katika eneo la Chibok miaka mitatu iliopita.

Post a Comment