Wednesday, May 10, 2017

Rais Jacob Zuma kuzuru Tanzania Leo.


Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini
Image captionRais Jacob Zuma wa Afrika Kusini
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anatarajiwa kuzuru nchini Tanzania hii leo katika ziara ya rasmi ya siku tatu kufuatia mwaliko wa rais John Pombe Magufuli.
Akizungumza na vyombo vya habari siku ya Jumatatu Waziri wa maswala ya kigeni nchini Tanzania Augustine Mahiga alisema kuwa ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara mbali kuangazia maswala mbali mbali ya maendeleo.
Rais Zuma ataandamana na mawaziri sita pamoja na wafanyibiashara kadhaa kutoka Afrika Kusini.
Atakuwa nchini humo kuanzia tarehe 10 hadi 13 akitarajiwa kufanya mazungumzo na mwandalizi wake rais Magufuli katika ikulu ya rais.
Kulingana na Mahiga kiwango cha biashara kati ya mataifa hayo mawili kimeongezeka kutoka dola milioni 803 mwaka 2006 hadi dola bilioni 2.2 2016 hatua iliobuni ajira 20,916.

No comments: