Sunday, May 21, 2017

Mazito ya Mwigulu Baada ya kutua Kibiti

Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba amesema serikali haiwezi kuvumilia mauaji ya mara kwa mara kama yanayotokea Somalia.

 Akizungumza leo katika jiji cha Bungu, Kibiti  ilipo kambi ya Polisi wanaotunza amani, na kuwataka polisi hao kusonga mbele katika mapambano ya  kuwasaka wauaji.

 Amesema wauaji na wanaoshirikiana nao wapo hapa hapa Kibiti na hivyo waziri huyo aliagizwa wote wakamatwe.

“Kibiti haiwezi kuwa kama Somalia hata siku moja. Wauaji wamejichanganya na raia wema na sasa tuwamulike hadi wapatikane,” amesema

 Amesema umefika wakati tuondokane na dhana kuwa wauaji wamekimbilia mahali pasipojulikana ilhali wapo hapa hapa Kibiti
Post a Comment