Monday, May 15, 2017

Shule ya Lucky Vicent yafunguliwa

Arusha. Shule ya Lucky Vincent ya jijini hapa imefunguliwa baada ya mapumziko ya wiki moja.

Shule hiyo ilifungwa  baada gari la shule hiyo kupata ajali na kusababisha  vifo vya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wao huku wengine watatu wakijeruhiwa.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Ephraim Jackson amesema wanafunzi wamefika kwa wingi shuleni na kwamba madarasa yote na wanafunzi wa darasa la saba wamefika 50 katika ya 71 huku watatu wakiwa kwenye matibabu nchini Marekani.

"Tumefungua leo na masomo yanaendelea kama kawaida,"amesema.
Pia shule hiyo imepokea wataalamu wa saikolojia kwa ajili ya kutoa msaada wa ushauri kwa wafanyakazi na wanafunzi.

No comments: