Diwani wa kata ya
Bagamoyo Bwana Zakayo Yohana Njate,ameelezea namna shughuli za maendeleo
zinavyo endelea katika kata yake, huku akiwa pongeza wananchi pamoja na wadau
mbalimbali kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo katika kata hiyo.
Baadhi ya wananchi wa
kata hiyo wamezungumzia namna wanavyo shiriki katika shughuli za kimaendeleo
zinazo endelea katika kata hiyo ya Bagamoyo,hususani katika ukarabati wa miundo
mbinu unao endelea katika eneo hilo.
Hata hivyo Diwani wa kata ya Bagamoyo Zakayo
Njate,amezungumzia namna shughuli za bomoa bomoa zilivyo waathiri wananchi wa kata
hiyo,kutokana na nyumba zao nyingi kubomolewa kupisha upanuzi wa bara bara.
Aidha diwani huyo amesema
kuwa kunamiradi mbali mbali ambayo inafanyika kwa nguvu za wananchi,hususani katika ukarabati wa vyoo
katika shule nne,ambapo shule mbili tayari ukarabati umekamilika.
Sanjari na hayo amesema
kuwa anawaomba wananchi kuendelea na moyo huo huo katika shughuli za
kimaendeleo,ambapo ameiomba halmashauri iweze kuongeza nguvu kwa wananchi hao
wa kata ya Bagamoyo katika shughuli za maendeleo.
No comments:
Post a Comment