Tuesday, July 25, 2017

21 WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI WILAYANI RUNGWE.
RUNGWE,

Sheria ndogo ya halmashauri juu ya  uhifadhi mazingira ya mwaka 2012 kifungu na 16 kinaeleza kuwa ni marufuku kulima ,kukata miti,kuchunga,na kufanyana shughuli yoyote umbali wa mita 60  katika vyanzo vya maji.

katika kutekeleza sheria hiyo Watu ishilini na moja [21] wakazi wa kata ya ibigi  kijiji cha katumba wamepelekwa mahakamani kwa kosa la kufanya shughuli za kibinaadam katika vyanzo vya maji kwenye mto ijingija na mto katumba .

Halmashauli ya wilaya ya rungwe imewafumgulia kesi watu hao katika mahakama ya mwanzo katumba one ambapo kesi hiyo ilikuwa imesikilizwa tarehe 24 /7/2017  kutokana na tarifa za watuhumiwa kuto wafikia kwa muda muwafaka hivyo kesi imeahirishwa mpaka tarehe 31/7/2017.


Afisa mazingira wilaya ya Rungwe amewaasa watu kuto kufanya shughuli katika vyanzo vya maji wala kumiliki eneo lililopo katika chanzo cha maji kwani ni kinyume cha sheria na husababisha maji kukauka hivyo kupelekea ukame.
Post a Comment