Tuesday, July 25, 2017

Mpango utakaowabana watumiaji wabaya wa Mitandao ya Kijamii waja

wadau wa mawasiliano Tanzania na China wamekutana kwenye Mkutano wa pamoja ‘Round Table Meeting’ uliofanyika Dar es Salaam kwa ajili ya kuzungumzia issue ya matumizi ya internet.

Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Edwin Ngonyani amezungumza na Waandishi na kusema kuwa upo mpango wa kulinda usalama wa matumizi ya internet pindi zitakapokamilika sheria zote tatu za mitandao ambapo mtumiaji atakayetendewa vibaya mtandaoni atakuwa na uwezo wa kupata haki yake.

“Malengo yetu makubwa ni kuangalia namna gani tunahakikisha matumizi ya internet nchini kama ilivyo kwa wenzetu wa China yanakuwa salama, hayatumiki vibaya, hayatumiki kutengeneza maoni ya watu mabaya dhidi ya mtu, Serikali, Taasisi.

“Tunayatumia kwa ajili ya kujiendeleza, kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa mmoja mmoja na kwa Taasisi na nchi nzima.” – Eng. Edwin Ngonyani
Post a Comment