Wednesday, January 17, 2018

SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA AFYA NCHINI


Ujenzi wa chumba cha Upasuaji kilichojengwa  katika Kituo cha Afya cha Nkoe kilichopo katika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi. 
Mhandisi  Ronard Mwajeka kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa akisisitiza jambo wakati wa kukagua  ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya Nchini.

Ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi iliyojegwa  katika Kituo cha afya  cha Nkoe, Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.


Angela Msimbira OR TAMISEMI LINDI

Serikali inaendelea  kutekeleza Mkakati wa kuviboresha  na kujenga  vituo vya afya nchini ili viweze kutoa  huduma bora inayoendana  na mahitaji halisi ya wananchi suala ambalo ni mpango wanne  wa Sekta ya afya (HSSP-IV).

Hayo yamebainishwa leo na Msimamizi wa Kitengo cha Dawa Vifaa, Vifaa tiba , vitendanishi na huduma za kichuhuzi za Afya kutoka  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Mathew Mganga wakati akiongea na Wafanyakazi wa Kituo cha afya cha Nkoe kilichopo kilichopo katika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi. 

Bw. Mathew Mganga amesema kuwa Katika kutekeleza lengo hilo Serikali na Wadau  wa Maendeleo  wanashirikiana  katika ukarabati miundombinu iliyopo na kujenga miundombinu mipya ya vituo vya kutolea huduma za Afya kwenye  vituo  vya afya, Zahanati na Hospitali kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi. 

Amesema serikali imekuja na makakati wa kupeleka fedha kwenye vituo vya afya ambavyo vilikuwa havitoi huduma mbalimbali za afya ziweze kutoa huduma hizo kwa wananchi. 

Fedha hizo zimelenga kukarabati au kujenga  katika maeneo ya vipaumbele kama ifuatavyo: Jengo la upasuaji, wodi ya akina mama, wodi ya wototo, Maabara, Nyumba za watumishi inayojitegemea, Chumba cha kuifadhia maiti, Kichomea taka na shimo la kuchomea Kondo la Nyuma, Mfumo wa ukusanyaji wa maji ya mvua na vifaa na vifaa tiba kwenye vituo vya kutolea huduma.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi katika kituo cha afya Nkoe,Wilayani Ruangwa Bw. Mohamedi Pilipili ameishukuru Serikali kwa kutoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya kujenga miundombinu  ya afya katika wilaya hiyo.

Amesema awali kituo cha afya cha Nkoe kilikuwa katika hali mbaya ya uchakavu wa majengo, kutokuwa na chumba cha upasuaji, maabara, wodi ya wazazi na watoto pamoja na chumba cha kuifazia maiti jambo ambalo kwa hivi sasa limeweza kutatuliwa kwa kujengwa ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma za afya katika kituo hicho.

Amesema kuwa  wananchi wameweza  kuchimba msingi pamoja na kuchota mchanga ili kuhakikisha Kituo cha afya kinajengwa kwa wakati na kupunguza changamoto zilizokuwepo za miundombinu ya afya katika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi. 

Aidha Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OT-TAMISEMI)  kwa kushirikiana ofisi ya Waziri Mkuu,  na Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa  Umma na Utawala  Bora zinafanya ufuatiliaji wa maendeleo ya ujenzi  na  ukarabatiwapo  wa vituo vya afya  kwenye Mikoa  na Halmashauri zote zinazotekeleza  miradi ya afya  nchini.

No comments: