Monday, November 12, 2012

MTOTO WA MIAKA MITATU ACHOMWA MOTO KISHA KULAZIMISHWA KULA KINYESI CHAKE MAJENGO JIJINI MBEYA

HIVI NDIVYO ALIVYOUNGUZWA MTOTO ANETH NA MAMA YAKE MDOGO
WANANCHI WENYE HASIRA KALI WALIMCHUKUA MAMA HUYO NA KUMPELEKA KITUO CHA POLISI


MWENYEKITI WA MTAA HUO HABIBA MWAKITALU AMEMBEBA MTOTO ANETH TAYARI KWA KUMPELEKA HOSPITALI HUKU NYUMA AKIFUATIWA NA MWESHIMIWA DIWANI KATA YA MAJENGO SAMWELI

Katika hali isiyo ya Kawaida Mkazi wa majengo jijini Mbeya Ndugu Bahati Rukangara amemchoma moto mtoto mdogo wa mika 3 aliyefahamika kwa jina la Aneth kisha kumfungia Ndani na kumlazimisha ale kinyessi chake.
Akizungumza Mwenyekiti wa mtaa huo Ndugu  Habiba Mwakitabu amesema   kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 10 :30 asabuhi ambapo majirani na mwanamke huyo waligundua mara baada ya kusikia sauti ya mtoto huyo akilia kutokana na maumivu.
Amesema mara baada ya kusikia sauti hiyo walifika eno hilo na kunza kumhoji ili kufahamu kiini cha tatizo hilo ambapo  alishindwa kutoa ushirikiano ndipo walipo  anza kumpiga  .
Amesema kutokana na hali hiyo majirani walilazimika kubomoa mlango ndipo walipo mkuta mtoto huyo akiwa uchi huku ameungua vibaya mwilini hasa katika upande mmoja eneo la mkono wa kushoto .
Amesema mara baada ya kumhoji mtoto huyo aliwaeleza kuwa mama yake mdogo alichukua nguo na mkumfunga mkononi kisha kumwagia maji ya moto pamoja na kumlazimisha ale kinyesi chake hali ambayo iliwafanya washindwe kuvumilia na kuanza kupiga kelele kwa lengo la kuomba msaada kwa watu wengine.
Kwa mujibu maelezo ya mwenyekiti huyo amesema kuwa Mtuhumiwa huyo amekuwa akifanya vitendo vya manyanyaso kwa mtoto huyo marakwamara ambapo wamekuwa wakimuonya lakini amekuwa si mtu wa kusikia.
Ameesema mtoto huyo si wa kwa kwakwe kwani amekuwa akiishi naye kwa muda mrefu sasa ambapo aliachiwa na dada yake ambaye hakufahamika kuwa nayishi wapi kwa sasa.
Hata Diwani wa kata hiyo Ndugu Samuel Mamboma alifika eneo hilo tukio na kutoa msaada wa usafiri kwa lengo la kumfikisha mama huyo polisi pamoja na mtoto huyo ambaye naye alikimbizwa Hospitali.
Hata hivyo amesema tukio hilo si la kwanza kutokea katika meaeno hayo kwani kumekuwepo na matukio mengi hasa ya utoaji mimba na kutupwa watoto.
HABARI KWA HISANI YA EMANUEL MADAFA
Post a Comment