Friday, December 7, 2012

MMOJA AFARIKI PAPO HAPO WENGINE 11 WAJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA MAENDEO YA NZOWE MBEYA LEO MCHANA

MCHANA HUU MBEYA  TENA
Gari aina ya hiace Daladala mbili  zimegongwa na Roli  aina ya Lelyand Daf ambalo lilifeli breki  hivyo kwenda kuparamia daladala hizo ambazo zilikuwa zinashusha abiria kwenye kituo cha njia panda itende jijini mbeya yaani barabara kuu iendayo Tunduma


Bibi huyu akiwa anasikitika huku kashika kuni zake mkononi akisema ajali hizi zinazidi kuwamaliza vijana hakuwa na maneno mengi zaidi ya kusema eee mungu tuondolee balaa hili la ajali

Hii ndi hiace ya pili inayofanya safari zake katika sokomatola na iyunga



Umati wa wananchi wakiwa hawaamini kilichotokea hapo 



Hili ndilo Roli lililogonga Hiace zote mbili dereva wa roli hilo kakimbia


Baadhi ya majeruhi wakipata matibabu katika hospitali ya rufaa mbeya

Baadhi ya wananchi wakimiminika kwenda waona ndugu zao waliopata ajali


Moja wa mashuuda wa ajali hiyo akiwasimulia waandishi wa habari jinsi ajali ilivyotokea
Habari kamili na majina ya majeruhi tutawaletea baadae
picha na mbeya yetu
FAMILIA YA SHALO MILIONEA SASA YAIBUMA MAZITO


MWILI WA  MAREHEM SHALO MILIONEA  BAADA YA KUPATA AJALI


Na: Burhani Yakub, Muheza
FAMILIA ya msanii Hussein Ramadhani Mkiety (Sharo Milionea) aliyekufa katika ajali wilayani Muheza wiki
iliyopita imedai kuwa haiamini kwamba kifo cha mtoto huyo kilitokana na ajali, hivyo kulitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kubaini ukweli.

Mjomba wa marehemu , Mohamed Msenga alisema jana kwamba familia imekuwa na shaka juu ya mazingira ya kifo hicho baada ya kurejeshewa nguo za msanii huyo zilizokuwa zimeibwa baada ya ajali lakini hazikuwa na damu.


Msenga alisema muda mfupi baada ya mama mzazi wa Marehemu Zaina Mwaimu Mkiety (54), kuitwa polisi na kukabidhiwa  vitu mbalimbali zikiwamo nguo ambazo marehemu alikuwa amevaa siku ya ajali hawakuona hata alama ya damu jambo ambalo liliwashangaza.
Alisema shaka hiyo ilianzia katika eneo ambalo ajali hiyo ilitokea akisema walipofika na kuonyeshwa mahala alipokuwa ameangukia, hawakuona damu jambo ambalo liliwatia shaka.
Alisema begi la nguo za msanii huyo lilikuwa na udongo mwingi likionyesha kwamba walioiba walikuwa wamelifukia kabla ya kusalimisha lakini hakuna damu zilizoonekana.


Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Teule Muheza, Dk Julius Mjema aliyeufanyia uchunguzi mwili wa Sharo Milionea alisema sababu ya kifo chake ni kichwa kupondeka.
“Mimi ndiye niliyefanyia ‘postmoterm’ (uchunguzi), mwili wa Sharo Milionea, ni kwamba kichwa kilikuwa kimepondeka huku mifupa ya kichwa ikiwa imepondeka pia,” alisema Dk Mjema.


Kuhusu madai ya nguo kutokuwa na damu, alisema marehemu alipata mpasuko wa ndani kwa ndani na siyo wa  nje, ndiyo maana alipofikishwa chumba cha maiti damu zilionekana zikiwa zimeganda masikioni.


Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe alipoulizwa kuhusu madai hayo ya familia  alisema: “Hiyo ni taarifa ambayo jeshi la polisi litaifanyia kazi kwa kuingia kwa kina katika kuchunguza ili kuridhisha pande zote.”



Mama yake alia kukosa mjukuu
Katika hatua nyingine, mama mzazi wa msanii huyo amesema kutoachiwa mjukuu na tarehe za mwisho wa mwezi ni alama ambazo zitasababisha awe akimkumbuka mwanaye huyo milele.
Akizungumza nyumbani kwake, katika Kitongoji cha Jibandeni Kijiji cha Lusanga wilayani hapa alisema kila ulipokuwa ukifikia mwisho wa mwezi ulikuwa ni muda wake wa neema kwani Sharo Milionea alimtumia fedha za matumizi yake binafsi pamoja na familia nzima nyumbani hapo.


“Pamoja na kwamba kila mara alikuwa akinitumia fedha za kutatua shida zangu mbalimbali nilizokuwa nikimweleza lakini kila mwisho wa mwezi alikuwa akihakikisha anatuma fungu la matumizi yangu na ndugu zake hapa nyumbani,” alisema mama huyo.
Alisema mwisho wa mwezi itakuwa ni alama ya kudumu ya kumbukumbu ya mwanawe kwa sababu ni wakati ambao alikuwa akimtumia fedha za matumizi yake pamoja na
familia nzima.


Kuhusu mjukuu alisema: “Sharo ni mwanangu wa pekee wa kiume, amekufa bila kuniachia mjukuu.. hii inaniuma sana lakini namshukuru Mungu kwani amechukua kiumbe chake na ndiye ajuaye siri iliyofichika mbele yangu,” alisema.


Alisema hadi alipofariki hakuwahi kumdokeza juu ya kuwa na mtoto wala kumpa mimba msichana yeyote... “Unajua Sharo Milionea alizaliwa pacha na mwenzake Hassan lakini mwenzake alifariki dunia siku tano baada ya kuzaliwa kwa hiyo katika kizazi changu mwanangu pekee wa kiume alikuwa Sharo Milionea ambaye nilitumaini kwamba angeniletea wajukuu,” alisema Zaina.
WAKATI HUOHUO FAMILIA YA

MAREHEMU SHARO MILIONEA;FAMILIA YAMTEUA KITALE KUSIMAMIA MALI ZA SHARO


Msanii wa vichekesho Musa Kitale.

FAMILIA ya Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’ aliyefariki dunia Novemba 26, mwaka huu kwa ajali ya gari iliyotokea Songa-Kibaoni, Muheza, Tanga imemteua msanii wa vichekesho Musa Kitale kuwa mwangalizi wa mali za marehemu.
NA
 Waziri Mwalimu Azindua Kampeni Za Siku 16 Kupinga Unyanyasaji Wa Kijinsia


Balozi wa Uingereza Diana na Naibu Waziri Ummy wakionyesha moja ya mabango yatakayobandikwa sokoni lenye ujumbe wa “Mpe riziki si matusi” mara baada ya uzinduzi.
Naibu Waziri Ummy Mwalimu na Balozi wa Uingereza nchini Diana Croner, wakikata utepe kuzindua mabango yatakayobandikwa katika masoko mbalimbali yakihamashisha kupinga vita dhidi ya unyanyasaji kijinsia na matusi sokoni.
Naibu Waziri Ummy akiwa na wanawake wafanyabiashara kutoka masoko ya Ilala wakionyesha mabango ya kupinga matusi katika masoko.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya pinga unyanyasaji na matusi sokoni iliyofanyika Soko la Kivukoni, Ferri Jijini Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa siku 16 za kupinga unyanyasaji kijinsia.
NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, ameahidi kuwa atahakikisha vinapatikana vituo maalum vya kuripoti taarifa za unyanyasaji na matusi katika masoko na magulio wilaya ya Ilala ili kurahisisha mapambano dhidi ya unyanyasaji.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni za siku 16 kupinga unyanyasaji kijinsia katika soko la Kivukoni Feri leo iliyobebwa na kauli mbiu ya “pinga unyanyasaji na matusi sokoni” “nipe riziki na si matusi” iliyozinduliwa katika masoko matano ya Ilala, Kigogo Saambusa, Kibasila, Mchikichini na Feri.

Amesema kuwa, kutokana na hali halisi, wanawake wanapaswa kutoa taarifa katika madawati maalum katika vituo vya polisi, lakini kutokana na umbali wa vituo hivyo anaangalia uwezekano wa kusogeza huduma hizo kwenye masoko hayo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, ameeleza kuwa, katika tafiti zilizofanywa zinaonyesha kuwa asilimia 43 ya wanawake wamejikita katika ujasiriamali katika sekta isiyo rasmi ambapo wanakabiliwa na changamoto kadha wa kadha ikiwemo mitaji midogo, maeneo madogo ya kufanyia biashara wakijihusisha na biashara kama za mama ntilie, ushonaji, kutengeneza batiki na nyinginezo.

Ameongeza kuwa, utafiti uliofanywa katika masoko 10 ya jijini Dar es Salaam unaonyesha kuwa wanawake wamekuwa wakikabiliwa na matatizo ya unyanyasaji ukatili wa kingono, matusi na kiuchumi.

Aidha ameeleza kuwa, kampeni hii inatarajiwa kufikishwa katika masoko yote Jijini Dar na baadaye nchi nzima ili kuleta mwamko miongoni mwa watumiaji wa masoko.
Na:  Usu-Emma Sindila na Sakina Mfinanga
PIA
JK Hosts Dinner For GAVI Forum Meeting Members At State House

 President Jakaya Mrisho Kikwete greets Former First Lady of South Africa Mama Graca Machel as the First Lady of Zambia Mama Satta looks on during a dinner he hosted for members of the 5th Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) Partners Forum at the State House in Dar es salaam. Others in the picture are Mr. Dagfinn Hoybraten, Chairman of the GAVI Board and Dr. Seth Berkley, CEO of GAVI.
 President Jakaya Mrisho Kikwete chats to Former First Lady of South Africa Mama Graca Machel as the First Ladies of Tanzan ia and of Zambia, Mama Salma Kikwete and Mama Satta looks on during a dinner he hosted for members of the 5th Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) Partners Forum at the State House in Dar es salaam. Others in the picture are Mr. Dagfinn Hoybraten, Chairman of the GAVI Board and Dr. Seth Berkley, CEO of GAVI.
 
A Cross section of guests during a dinner he hosted By President Jakaya Kikwete for members of the 5th Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) Partners Forum at the State House in Dar es salaam.
President Jakaya Mrisho Kikwete receives a new CD from South Africa song bird and UNICEF's Goodwill Ambassador Yvonne Chakachaka during a dinner he hosted for members of the 5th Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) Partners Forum at the State House in Dar es salaam.
PHOTO BY STATE HOUSE
NA
 Mjadala Kuhusu Ukiukwaji Wa Uhuru Wa Vyombo Vya Habari Wafanyika Zanzibar.

 Meneja wa Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar (MCT)Suleiman Seif akifafanua jambo katika Mjadala wa Waandishi wa Habari kuhusu Ukiukwaji wa Uhuru wa Vyombo vya Habari,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo Kikwajuni Mjini Zanzibar
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Yussuf Omar Chunda akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mjadala wa Waandishi wa Habari kuhusu Ukiukwaji wa Uhuru wa Vyombo vya Habari,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo Kikwajuni Mjini Zanzibar.
 Mwandishi Mkongwe Salim Said Salim akiwasilisha Mada kuhusu Dhana ya Ukiukwaji wa Uhuru wa Vyombo vya Habari katika Mjadala wa Waandishi wa Habari kuhusu Ukiukwaji wa Uhuru wa Vyombo vya Habari,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Meneja wa Udhibiti na Viwango wa Baraza la Habari Tanzania (MCT)John Mireny akifafanua jambo katika Mjadala wa Waandishi wa Habari kuhusu Ukiukwaji wa Uhuru wa Vyombo vya Habari,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo Kikwajuni Mjini Zanzibar. 
  PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
PIA
 AJALI YAUA WATANO WA FAMILIA MOJA HAPO HAPO


Gari aina ya Rav 4 lenye namba za usajili T 770 BNP lililopata ajali eneo la Tanangozi, Iringa lililokua likiendeshwa na Bw. Ezekiel Mwaiteleke (Marehemu) majira ya saa sita na nusu mchana na kusababisha vifo vya watu watano wa familia moja papo hapo jana Desemba 4, mwaka huu.


Gari aina ya Scania lenye namba za usajili T 840 BST likiwa na tela lake lenye namba T 566 BNQ…
Gari aina ya Rav 4 lenye namba za usajili T 770 BNP lililopata ajali eneo la Tanangozi, Iringa lililokua likiendeshwa na Bw. Ezekiel Mwaiteleke (Marehemu) majira ya saa sita na nusu mchana na kusababisha vifo vya watu watano wa familia moja papo hapo jana Desemba 4, mwaka huu.


Gari aina ya Scania lenye namba za usajili T 840 BST likiwa na tela lake lenye namba T 566 BNQ likiwa limegongwa kwa nyuma na Toyota Rav 4 huko Tanangozi, Iringa na kusababisha vifo vya watu watano wa familia moja papo hapo.
Wasamaria wema wakitoa moja ya maiti kutoka katika Toyota Rav 4 baada ya ajali jana.
Baadhi ya akina mama wasamaria wema wa Tanangozi, Iringa wakijaribu kumpepeleka mmoja ya majeruhi wa ajali iliyotokea jana eneo la Tanangozi, Iringa likihusisha Toyota Rav 4 T 770 BMP lililoingia nyuma ya tela lenye namba za usajili T 566 BNQ ambapo watu watano wa familia moja waliokuwa wakitokea Dar kwenda Mbeya walifariki papo hapo.
KUELEKEA MIAKA 51 YA UHURU  WA TANGANYIKA HAYA NI MATUKIO MUHIMU YA AWAMU YA KWANZA YA SERIKALI YA TANZANIA ILIYOONGOZWA NA BABA WA TAIFA JK NYERERE




Mwalimu Nyerere akibebwa juu juu na Watanganyika waliokuwa na furaha baada ya kufanikisha Uhuru wa Tanganyika 1961 kutoka kwa Waingereza

Mwalimu Nyerere alisimikwa kuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika. Kipindi hicho, Uwaziri Mkuu ndio kilikuwa cheo cha juu zaidi hatukuwa na cheo cha Urais

Mwalimu Nyerere akichanganya udongo wa Bara (Tanganyika) na Visiwani (Zanzibar) kuashiria kuundwa rasmi kwa jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hiyo ilikuwa mwaka 1964
Muungano wetu umepatikana kwa mambo makuu mawili. Kwanza, maridhiano baina ya pande mbili za Bara (Tanganyika) na Visiwani (Zanzibar) yaliyosimamiwa kikamilifu na Waasisi Hayati Nyerere na Hayati Karume; Pili Muungano wetu uliundwa kisheria zaidi kupitia makubaliano ya Hati za Muungano kama ambavyo Wanavyoonekana pichani waasisi wakibadilishana Hati za Muungano ambzo zilikuwa na makubaliano ya Mambo 11 (kipindi hicho)


Hii ni picha ya siku ya tukio la kuanzishwa kwa Azimio la Arusha mnamo 1967. Azimio la Arusha lilikuwa na lengo la kuondoa unyonyaji na matabaka ndani ya jamii zetu.

Mwalimu Nyerere alianzisha mbio za Mwenge kwa kuuwasha mwenge na kuwekwa juu ya Mlima Kilimanjaro ili uangaze kote ili penye chuki pawe na upendo; penye dhuluma pawe na haki n.k

Mwalimu Nyerere alifanikiwa vyema kujenga mahusiano mema baina ya Tanzania na nchi mbalimbali za Kiafrika na mataifa mbalimbali ya kimataifa.

Mwalimu Nyerere aliyaongoza majeshi ya Tanzania kwenye kuyaondoa majeshi ya Idd Amin yaliyovamia Kagera. Vita hiyo ilijulikana kama vita ya kagera iliyotokea mnamo 1978 na tulifanikiwa kuyaondoa majeshi ya Idd Amin.
Mwalimu Nyerere aliamua kung'atuka kwa hiari yake na kumuachia kwa njia ya kidemokrasia madaraka ya urais Alhaji Ali Hassan Mwinyi. Hiyo ilikuwa mnamo 1985.
ALLY KINGO
0752881456

No comments: