Thursday, December 6, 2012

POLISI WAMKOSAKOSA KUMUUA MWANDISHI WA HABARI SHABANI MATUTU NI JUZI TU MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI AMEUWAWA NA BADO TUKIO HALIJAFUTIKA KATIKA AKILI ZA WATANZANIA LEO TENA POLISI HAOHAO JE POLISI WAKO JUU YA SHERIA? NANI ANAWALINDA HAWA HADI WANAKUWA NA AMRI YA KUUA KILA KUKICHA?

SIKU TULIPOANDAMANA WAANDISHI WA HABARI MBEYA KUPINGA MAUAJI YA KIKATILI YALIYOFANYWA N JESHI LA POLISI MKOA WA IRINGA  KWA  MWANDISHI  DAUDI MWANGOSI

SIKU YA MAANDAMANO YA AMANI KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA




BAADHI YA WAANDISHI WA MKOA WA MBEYA

KATIBU WA CHADEMA DR SILAA AKITOA SALAM ZA RAMBIRAMBI SIKU YA MAZIKO YA DAUDI MWANGOSI

PROF MACK MWANDOSYA MBUNGE WA RUNGWE MASHARIKI AKITOA RAMBIRAMBI SIKU YA MAZIKO YA DAUDI MWANGOSI KIJIJI KWAO BUSOKA WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA
WAWAKILISHI WA CHANNELTEN WAKIWA PEMBENI YA KABURI LA MWENZAO  DAUDI MWANGOSI

MAREHEMU DAUD MWANGOSI ENZI ZA UHAI WAKE  . BADO MACHUNGU HAYAJAFUTIKA POLISI HAOHAO TENA WAMPIGA RISASI MWANDISHI WA HABARI SHABANI MATUTU.

Mwandishi Aliyepigwa Risasi Anaendelea Na Matibabu MOI

Ndugu wapendwa, DSM City Press Club imepata taarifa za kushtusha kufuatia ya kupigwa risasi na kujeruhiwa begani kwa mwandishi wa Tanzania Daima Bwana Shabani Matutu (30) ambaye pia ni mwanachama wa Dar City Press Club (DCPC). Sambamba na taarifa hizo imeelezwa kuwa mwandishi huyo amelazwa katika Taasisi ya mifupa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI). Chanzo hasa cha kupigwa risasi kwa mwandishi huyo bado hakijaeleweka kwa DCPC, uongozi wa DCPC unafuatilia. Tutakapojiridhisha na taarifa zilizotolewa pamoja na zile tutakazozipata tutawataarifu rasmi. Kwa sababu hizo tunaomba waandishi wote, ndugu, jamaa, marafiki, wapenda haki na amani, wanaharakati washirika na wadau wote wa vyombo vya habari kuwa watulivu tukimjulia hali kwa misaada ya hali na mali mwandishi mwenzetu Shabban Matutu ili apone majeraha

Ukistaajabu Ya Mussa Utayaona Ya Firauni



Katika pitapita zake kwenye manispaa ya Moshi , kamera ya  ikanasa tukio hili  huyu ni binti wa miaka 14  na tayari ana watoto wawili

MICHEZO 
NGASSA ATUA MERREIKH KWA DOLA 75,000 NA MSHAHARA MNONO WA DOLA 4,000 YEYE MWENYEWE AKATIWA DOLA 50,000 ZA WINO

Ngssa; Sasa mutu ya fweza

Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
BIASHARA imeisha. Azam FC imemuuza Mrisho Khalfan Ngassa kwa dola za Kimarekani 75,000 kwenda El Merreikh ya Sudan ambako amesaini mkataba wa miaka miwili, utakaomuwezesha kulipwa mshahara wa dola za Kimarekani 4,000 kwa mwezi huku naye akilipwa dola 50,000 za kusaini.
Awali, Merreikh walitaka kumpa mkataba wa miaka mitatu Ngassa wenye thamani ya dola 100,000, lakini wakala wake Alhaj Yussuf Said Bakhresa akakataa akisema utambana mchezaji wake aking’ara na kutakiwa na klabu nyingine.
Sasa Ngassa baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge mwishoni mwa wiki hii, atakwenda Sudan kufanyiwa vipimo tayari kujiunga na klabu hiyo, ambayo ni jambo la kawaida kucheza hatua ya makundi ya michuano ya klabu Afrika.
Azam FC imesema imeweka mbele maslahi ya mchezaji na taifa kwa ujumla katika maamuzi ya kumuuza Sudan, kutoka Simba alikokuwa akicheza kwa mkopo. “Hii timu (Merreikh) kila mwaka inacheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, maana yake huyu mchezaji atakwenda kupata maendeleo na kuja kuisaidia zaidi Tanzania katika mashindano ya kimataifa,”alisema kiongozi mmoja wa Azam.  
Alipoulizwa kuhusu Simba SC aliyokuwa anaichezea klabu hiyo, kiongozi huyo alisema wao walimtoa kwa mkopo Ngassa kwenda kwa Wekundu wa Msimbazi hadi Mei 31, mwakani na mkataba wao ndio unasema hivyo.
“Sisi tuliwapa Simba huyu mchezaji kwa mkopo hadi Mei 31 na wakatupa Sh. Milioni 25, ila tuko tayari kuwarudishia fedha zao walizota, lakini huyu mchezaji ni mali yetu  na hata TFF wanatambua hilo, na tumekwishamuuza Merreikh,”alisema.
Alipoulizwa kuhusu Simba kusaini mkataba mpya na Ngassa, alisema; “We uliona wapi dunia nzima timu inapewa mchezaji kwa mkopo halafu inamsainisha mkataba? Simba lazima ifike wakati waache kurudia makosa, haya ndio mambo ya Mbuyu Twite sasa,”alisema kiongozi huyo wa Azam.
Katika kukamilisha mauzo ya mchezaji huyo, kiongozi wa Marreikh akiwa Dar es Salaam mbele ya viongozi wa TFF na Azam, alipigiwa simu Ngassa aliye hapa Kampala, Uganda na kuhusishwa katika dili hilo, naye akakubali ndipo mambo yakamalizwa.
Aidha, Azam wameomba TFF ihakikishe kunakuwa na ulinzi katika kambi ya timu ya taifa mjini hapa, ili Simba wasimfanyie vurugu Ngassa na kumvuruga kisaIkolojia, wakati ndiyE tegemeo la timu katika kampeni ya kutwaa Kombe la Challenge mwaka huu mjiini hapa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe akizungumza kutoka Dar es Salaam, alisema kwamba watawapeleka mahakamani Azam kwa kitendo cha kumuuza mchezaji wao kinyume cha sheria.   
“Haiwezekani wamuuze wao, wakati wao walituuzia huyu mchezaji na sisi tuna mkataba ambao tulisaini nao, hii ni kinyume cha sheria na sisi tutawapeleka mahakamani,”alisema Hans Poppe ambaye anatua kesho mjini hapa.
Azam walimtoa kwa mkopo Ngassa mwanzoni mwa Agosti, mwaka huu baada ya kukerwa na kitendo cha mchezaji huyo kubusu jezi ya timu yake ya zamani, Yanga, katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Alifanya hivyo, baada ya kufunga bao la ushindi akitokea benchi na kuiwezesha Azam kutinga fainali ya michuano hiyo, ambako walifungwa na Yanga 2-0, naye kwa mara nyingine akitokea benchi na kushindwa kufunga, hivyo kutuhumiwa kucheza kinazi.
Ilielezwa kwamba Simba walitoa Sh. Milioni 25 kumnunua kwa mkopo mchezaji huyo, ingawa baadaye Simba wakasema waliununua mkataba wa mwaka mmoja aliobakiza mchezaji huyo Azam FC, nao wakamuongezea wa mwaka mmoja kwa kumsainisha kwa Sh. Milioni 30, kati ya hizo Milioni 12 akipewa taslimu na 18 akipewa gari.
BURUDANI
UKITAKA KUOA SIKU HIZI LAZIMA UJIPANGE SAWASAWA LASIVYO UTAUMBUKA
KUOA KAZI SANA SIKU HIZI.
mhh ndio maana wanaume wanaogopa kuoa ( wapo wapo saaaaaaana!!!!!!jamani embu cheki hii ..... Hivi jamani, mnazijua gharama anazoingia bwana harusi hadi anapooa? Katika hali ya kawaida kabisa, kama wewe ni mwanaume na unataka kuoa, jiandae kwa mambo haya:
1. Kujitambulisha ukweni. Hapo utatakiwa uende kijijini alikozaliwa mkeo mtarajiwa ukajitambulishe huko. Kama mfano

mkeo anatokea Mwanza, na mnaishi Dar, andaa nauli ya watu wawili, malazi kwa siku mbili, na utagharamia shuhuli hiyo ya utambulisho. We tenga 500,000. Hapo tuna assume mkeo atajitegemea. Otherwise 800,000 itakutoka.
2. Kumtambulisha mkeo kwenu. Kama nyie nyumbani ni Arusha, utatakiwa umpeleke huko Ngarenanyuki. Sio umlete hapo Tabata mlipopanga. Hapo sio kwenu! Andaa nauli yako na atakaekusindikiza, nauli ya binti na mwenzie, na gharama za vinywaji na chakula siku hiyo. Utahitaji kama 700,000
3. Kifuatacho ITV ni kuwaalika wakwe zako nyumbani. Uwatoe watu kama nane Mwanza, uwalete Arusha. Wale, walale, wajisaidie, kwa gharama zako. We acha ubishi, tenga 800,000 tu.
4. Kwani we wazazi wako wanajua unakooa? Sasa je? Wasafirishe kwenda Mwanza! Watu watano. Utahitaji kuwa na 500,000. Beba pia ATM card yako, kuna imejensi.
5. MAHARI ndio topic inayofuata sasa. Ukiwa mjanja, unganishia kwenye hiyo safari hapo juu uue ndege wawili. Pamoja na hayo, itabidi ubebe 2,000,000.
6. Sasa kijana unaweza kumvisha mchumba wako pete. Nunua ya kawaida kabisa ya dhahabu. 350,000. Tukio lenyewe la kumvisha pete unaweza ita marafiki wawili watatu ukatumia 200,000. Au fanya sherehe kabisa. Mi simo
7. Oke, sasa unaweza kuitisha vikao vya harusi. Tengeneza kadi za mwaliko wa kamati kwa 200,000, kikao cha kwanza gharama zote ni juu yako. Andaa 500,000. Swali la kwanza kwenye kikao: "We una shing ngapi?" Sema 2,500,000.
8. Utahitaji 100,000 ya sms na simu kukumbushia michango. (Shukuru Mungu kuna cheka time)
9. Wakati vikao vinaendelea, utatuma 200,000 kwa m-pesa ili mambo ya kimila yaendelee kule nyumbani. We unaelewa
10. "Darling, sasa mi kwenye kitchen party ntavaa nini?" 300,000!
11. "Darling, kuna mahali nimeona gauni zuri la send." 400,000!
12. "Baby, rafiki yangu alinunua gauni la harusi China yani lilimpende..." 700,000!
13. Wakati huo wewe mwenyewe hujajua utavaa nini, hujanunua pete za harusi, hujamvalisha best man na mkewe. Tuseme unahitaji kama 1,500,000 maana utalia lia sana. Kumbuka, gharama hizi huchangiwi na kamati. Wala hutarudishiwa.
14. Siku ya send off lazma uende Mwanza. Utaenda mwenyewe? Ndugu wawili watatu na mshenga 600,000. Kwenye send off utatakiwa kutoa sijui blanketi la bibi, vitenge vya mashangazi, na vikorokoro kibao. Nunua hivyo vitu 300,000 uende navyo ili kupunguza gharama. Beba 200,000 za wale mashangazi watakaoibuka ghafla!
15. Mshonee baba mkwe suti 100,000 mama mkwe yeye atavaa gauni la 50,000.
16. Fotokopi hiyo hapo juu (namba 15) kwa wazazi wako. 150,000
17. Watu watakaopenda kuvaa sare wajitegemee! Mimi sina hela! Ila utavishonea nguo vile vitoto kwa 80,000.
18. Siku mbili kabla ya harusi, utaanza kupokea wageni. Unatakiwa uwatafutie malazi na chakula. Kwa ujumla utahitaji kama 500,000
19. Jioni watoe auti mashemeji zako ambao hawajawahi kufika Dar ukawanunulie bia ili wakuone wa maana. 200,000
20. Siku ya harusi bibi harusi na mwenzie na watoto na ma maids watatakiwa wakapambwe saluni. 200,000
21. We na mwenzio mtaenda kunyoa hapo kwa nanii. Ndevu na nywele na black kibishi 40,000
22. Siku ya harusi beba sadaka 10,000. Wakati huo umeshamtuma kijana akakulipie hoteli mtakayofikia baada ya harusi. Kamati haitoi hela hiyo, so utalipa malazi ya siku mbili 200,000
23. Kama mtaenda honeymoon sehemu yoyote nzuri nzuri nje ya mji, si chini ya 800,000 kwa angalau siku 5.
24. Wakati uko huko honeymoon, huna hata kumi, mwanakamati mmoja ambae hakuchanga anakupigia simu " Sasa tunavunja lini kamati?" Pesa yote iliyochangwa ilitumika kwenye harusi, sasa gharama za kuvunja kamati ni za nani?? 500,000! 25. SASA MNAANZA MAISHA YA UNYUMBA. 14,180,000 poorer. KAZI KWENU MSIOOA/MTAKAOOA TENA.KAM VIPI JIWEKE MAPEMA HAAA HAAAAAA HAAAAAA. FUATANA NAMI KATIKA
www.kingotanzania.blogspot.com

KINGO
0752-881456

KALI YA MWAKA 2012 HII HAPA

BABA ANAETUHUMIWA KUZINI NA KUZAA NA MWANAE WA KUMZAA ATINGA MAHAKAMANI BAADA YA KESI KUAIRISHWA AZOMEWA NA KINA MAMA NA KUKIMBIA KAMERA ZA WANDISHI WA HABARI

 Mkazi wa Mtaa wa Mbete,Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad(39),anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa(16) jina lake limehifadhiwa. akiingia mahakamani leo mbele yake ni mke wake na mtoto wake aliyezaanae ambao sura zao tumefunika

Bwana Yussuf Hamad anaetuhumiwa kuzaa na bintie akitaka kumpokonya kamera  mwandishi wa gazeti la majira Rashid Mkwinda ili asimpige picha

Jamaa kuona amezidiwa akaamua kujifunika na shati lake huku akitoa maneno makali kuwa nyie waandishi mmekosa cha kuandika mmeona hii ndiyo habari hakuna habari nyingine? alihoji mtuhumiwa huyo

Huyoooo anatoka nje ya mahakama


Sasa anavaa kofia yake ili watu wasimtambue huku akisema nifuateni niwaonyeshe kazi

Njooni sasa huku kashika jiwe

Kuona anazidi kufuatwa akaamua kuondoka mahali hapo huku  akiwa na jiwe lake mkononi

Akina mama wanamsindikiza kwa kumzomea mtuhumiwa huyo


 Mkazi wa Mtaa wa Mbete,Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad(39),anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa(15) jina lake limehifadhiwa.
Hayo yamethibitishwa na Mama mzazi wa binti huyo Bi, Regina Simon(35) baada ya kupata taarifa Mei 11 mwaka huu kuwa binti yake ana ujauzito wa miezi minne,na kuamua kutoa taarifa kwa Balozi  wa mtaa huo Bwana Steven Ovaova ambaye naye alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji Bwana Angelo Sanga.
Viongozi hao wa mtaa walimuita  mtuhumiwa na ili kupata ukweli wa tukio hilo,lakini mtuhumiwa alikanusha ingawa binti yake alithibitisha kutendewa ukatili huo na kwamba alikuwa akitishiwa kwa mapanga kila alipokuwa akifanya naye tendo la ndoa.
Baada ya uongozi kupata maelezo kutoka kwa binti huyo na mzazi kukataa waliamua kuipeleka kesi hiyo Polisi,ambapo walitoa PF3 iliyomwezesha binti huyo kupelekwa kwa 
daktari ambaye alithibitisha kuwa binti huyo ana ujauzito.
 Binti huyo amejifungua mtoto wa kike ambae sasa anamiezi mitatu mtoto huyo kaletwa leo mahakamani kama ushahidi kesi hiyo imeairishwa mapaka tarehe 12/12 mwaka huu,
 PICHA KWA HISANI YA JEM

No comments: