Wednesday, December 5, 2012

HABARI ZA JIONI

Waziri Aingilia Mgogoro Kati Ya Kiwanda Na Wananchi


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka (kulia) akiongea na Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha Saruji cha Twiga (Twiga Cement) Bw.Pascal Lessoinne (kushoto) mara baada ya mkurugenzi huyo kutoa taarifa fupi ya maendeleo ya kiwanda hicho na hali ya mvutano wa muda mrefu wa umiliki wa maeneo baina ya wakazi wa kata za Bunju na Wazo jijini Dar es salaam.
Picha na 2. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka akiwasalimia wakazi wa kata ya Bunju na Wazo mara baada ya kuwasili katika eneo  hilo  kwa lengo la kuzungumza nao ili kutafuta suluhisho la kudumu la  mgogoro wa ardhi kati yao na  kiwanda cha Saruji cha Twiga jana jioni.

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka akiongea katika mkutano wa hadhara na maelfu ya wakazi wa kata ya Wazo na Bunju waliojitokeza kufuatilia maendeleo ya mgogoro wa ardhi kati yao na Kiwanda cha Twiga Cement ambapo pamoja na mambo mengine amewahakikishia wakazi hao kuwa mgogoro huo utapatiwa ufumbuzi wa kudumu na kuwaomba kutoa ushirikiano kwake.
 Diwani wa eneo la Bunju na Wazo Sharif Exavery Majisafi akiongea na wananchi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka kuzungumza nao.

 Sehemu ya umati mkubwa wa wakazi wa kata za Bunju na Wazo wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka.
.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO DSM
NA

Mtumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Gladness Mangelele akitoa maelezo mbele ya Waziri Dk. Mwakyembe baada ya kuhusishwa katika sakata hilo ambapo alidai alikuwa hajui chochote kwani alikuwa  akitekeleza majukumu yake ya kawaida katika idara yake.
Dk. Mwakyembe akikagua Malori yanayodaiwa kutaka kutolewa kinyemela na kampuni ya Dhandho, Malori matano kati ya 26 yalipewa baraka na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yatolewe.
Marystella Minja akitoa maelezo yake mbele ya Waziri Dk Harrison Mwakyembe baada ya kutuhumiwa katika sakata hilo.
Mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Andrew Masaga (kulia) anayedaiwa kuhusika kula njama ya kutoa malori hayo  akijitetea mbele ya Waziri (hayupo pichani) katika sakata hilo jana jinoni. Kushoto  ni Mkuu wa Polisi Bandarini Afande FM Misilimu
Ofisa Utawala wa kampuni ya Dhandho Antipasi Otieno (kulia) akitoa maelezo mbele ya waziri Dk. Harrison Mwakyembe
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harisson Mwakyembe akizungumza na waadishi wa habari Bandarini jijini Dar es salaam Jana  jioni wakati akitoa taarifa ya kukamatwa kwa watumishi wa Bandari wanaodaiwa kutaka kutoa  malori 26 kinyemela  bandarini, watu watano wamekamatwa katika sakata hilo.
Dk. Harrison Mwakyembe akiongea na maafisa mbalimbali wa Polisi na Bandari baada ya kukagua magari hayo yaliyotaka kutolewa kinyemela bandarini hapo
PIA
 KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Nape Nnauye
--
Na Mwandishi Wetu-Gazeti la Majira

KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Nape Nnauye, amempongeza Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kukiri kumiliki kadi ya chama chao hadi sasa.

Alisema Dkt. Slaa ameanza kujifunza kusema ukweli baada ya kutambua uongo haulipi kwani kitendo cha kukiri kumiliki kadi ya CCM ni cha kiungwana hivyo anastahili pongezi.

Bw. Nnauye aliyasema hayo Dar es Salaam jana baada ya Dkt. Slaa kujibu tuhuma zake kuwa, wapo baadhi ya vigogo wa CHADEMA ambao wanamiliki kadi za CCM na wanazilipia hadi sasa.

“Dkt. Slaa amekiri katika vyombo vya habari kuwa anamiliki kadi ya CCM hadi sasa akidai anaitunza kama kumbukumbu muhimu hivyo ni vyema akawaeleza Watanzania kadi yake ameilipia hadi lini na aache kuwadanganya wenzake warudishe kadi za chama tawala wakati yeye ameendelea kuwa nayo,” alisema.

Bw. Nnauye amekiri kumheshimu sana Dkt. Slaa kama babu yake na alishtuka sana kusikia Katibu Mkuu huyo anawatuhumu baadhi ya viongozi wa CHADEMA na kudai ni mamluki wa CCM wakati yeye ni namba moja kwani anaowatuhumu hawana kadi za chama hicho.

“Nilimsikia Dkt. Slaa akiwatuhumu baadhi ya viongozi ndani ya chama chao kuwa ni mamluki wa CCM, hili linawasaidiaje Watanzania maskini.

“Kitendo hiki kimethibitisha upeo mdogo alionao katika kufikiri, huyu ni kiongozi mkubwa ambaye namuheshimu lakini anapaswa kujua yeye anaomba kuwa kiongozi hivyo lazima wananchi tumjue tabia zake,” alisema Bw. Nnauye na kuongeza;

“Viongozi wa aina yake ni janga kwa Taifa letu, usipokuwa mwaminifu kwa kidogo, huwezi kuwa mwaminifu kwa kikubwa,” alisema.
 NA  
Kipanya Leo NA DNA

TUMSAIDIE MTANZANIA MWENZETU
Bi Arafa akiwa na Msamaria mwema anaemsaidia kuhakikisha hali ya Mgonjwa huyo Inaimarika.
Bi Arafa Issa akiwa katika kitanda cha ward namba 20 Sewa Haji-Muhimbili hosp asubuhi ya leo.
--
Bi Arafa Issa mwenye umri wa Miaka 38 mkazi wa Kijiji cha Narung'ombe wilayani Ruangwa ambae anasumbuliwa na Uvimbe baada ya kuumwa Kichwa na baadae kupata kipele kilichosababisha Uvimbe kama anavyoonekana Pichani, alifikishwa katika Hospital ya Muhimbili baada ya Wasamaria wema walioguswa na hali hiyo pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi kujitoa kumsaidia kumsafirisha toka Kijijini kwao hadi Muhimbili Hospital.

Baada ya kufikishwa na kupokelewa amelazwa Block la Sewa Haji Ward na 20 NA Baadae alitakiwa kupimwa kipimo cha CT Scan kufuatia kipimo hicho Wauguzi wake waliambiwa kipimo hicho kina tatizo na kuelekezwa kwenda Regency Hospital kupima hali iliyokuwa ngumu kwao kutokana na gharama kubwa kwao ya kumudu kipimo hicho Tshs(264,000/-).

Kwa msaada mwingine Wadau walifanikisha kupimwa kwa mgonjwa huyo na kupatiwa majibu ambayo yanaelekeza kufanyiwa Upasuaji..

Asubuhi ya Leo nilifika katika hospital hiyo na kuonana na Bi Arafa ambae analalamika sana kupata maumizi makubwa Kichwa na kudai kuwa toka amepokewa katika hospital hiyo na kulazwa tarehe 20 NOV 2012 hadi leo ajapata dawa ya aina yoyote zaidi ya panadol anazonunua hali inapomzidi.

Nilifanikiwa kuwasiliana na muuguzi aliekuwepo zamu asb na baada ya kupitia file lake alinikabidhi fomu inayoonyesha mgonjwa anatakiwa apime kipimo kinaitwa MRI Brains na kuelekeza sehemu ya kwenda kulipia kipimo hicho...Baada ya kuwasilisha hiyo fomu imetakiwa Tshs Laki mbili(200,000)Pia itahitajika gharama ya Operesheni ambayo haikutajwa.

Kwa niaba ya Bi Arafa Nawaomba wadau mbalimbali ndugu na jamaa kusaidia hatua inayofuata kumsadia mgonjwa huyo..Yupo hapo Hospital Unaweza kusaidia kwa njia moja au nyingine.

Kwa Mawasiliano zaidi ya mgonjwa huyo wasiliana nami kwa 0716 483532,0787176221 au 0716483532 Abdulaziz Ahmeid wa Lindi Press Club au abdulaziz762@gmail.com

Nawashukuru wote walioguswa kumsaidia Mgonjwa huyo hadi ilipofikia leo,,Ameen
BURUDANI
 Washiriki wa shindano la Miss East Afrika 2012 wakiwa katika picha ya pamoja mapema leo mchana  jijini Dar.
PIA  
MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA TANZANIA DAIMA AJERUHIWA KWA RISASI

 Shabaan Matutu akionesha sehemu ya mkono wake wa kulia ambao ulipata majeraha wakati polisi walipotumia nguvu kuingia chumbani kwake na kumtwanga risasi iliyompiga upange wa kushoto wa kifua chake.
 Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Free Media inayochapisha magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Shaaban Matutu akionesha jeraha lililotokana na kupigwa risasi na Polisi katika tukio lililotokea usiku wa kuamkia leo - baada ya polisi kuvamia nyumbani kwake Tegeta jijini Dar es Salaam kwa madai ya kumtafuta mtuhumiwa waliyekuwa wakimsaka. Matutu kwa sasa amelazwa Hospitali ya Muhimbili katika Kitengo cha Mifupa (MOI) kwa ajili ya matibabu zaidi.
 Shabaan Matutu akionesha sehemu ya mkono wake wa kulia ambao ulipata majeraha wakati polisi walipotumia nguvu kuingia chumbani kwake na kumtwanga risasi iliyompiga upange wa kushoto wa kifua chake.
 Daktari aliyekuwa zamu katika Hospitali ya Mwananyamala akiangali picha ya X-Ray ya Matutu mara baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo na kufanyiwa kipimo hicho, kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Wafanyakazi wa Free Media, Khadija Kalili kushoto na Maria Kayala (kulia) ambao walifika Hospitali ya Mwananyamala baada ya kupata taarifa za tukio hilo.Picha Zote na Habari na Dande Francis(POLE SANA KAMANDA WANGU MUNGU AKUPE AFYA NJAMA 


KUTOKA KWENYE UKURASA WA MH.EDWARD LOWASSA KATIKA FACEBOOK

KAZI NI MSINGI WA MAENDELEO KWA KILA TAIFA LILILO PIGA HATUA,
Ewe Kijana mzalendo wa taifa hili chapa kazi ujenge heshima yako na heshima ya Taifa letu…
Huu si wakati wa KIJANA kulalamika ni wakati wa KIJANA kuchapa kazi…Read more: KUTOKA KWENYE UKURASA WA MH.EDWARD LOWASSA KATIKA FACEBOOK - BongoCelebrity

VYANDARUA VYATUMIKA KUSAFIRISHIA CHUPA CHAKAVU MBEYA

Chupa chakavu zikiwa zimefungwa vizuri katika vyandarua tayari kwa kusafirishwa kwenda DSM

Sisi kama Mbeya yetu hatuna maneno tumejionea wenyewe na wewe ona sasa toa maoni yakoBonge la mzigo limefungwa kisawasawa tayari kwa kusafirishwaChandarua kazin
VIJANA WA MJI MDOGO MBALIZI MBEYA WILAYANI MBEYA VIJIJINI WAFANYA USAFI WA KUZIBUA MIFEREJI NA KUTENGENEZA BARABARA

Vijana wa Mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani Mbeya leo wamefanya kazi ya kufagia kuzibua mifereji na kutengeneza barabara kivutio kikubwa kilikuwa kwa kina dada kwani walijitokeza kwa wingi na kuchapa kazi sambamba na kaka zao
Hakika vijana wa Mbalizi tuwape pongezi kwa kazi nzuri wanayoifanya kwani ni vijana wachache sana wanaojitolea kufanya kazi hizo za usafi wa kujitolea

Vijana hao wa mbalizi wamesema si vema kila kitu kuiachia serikali waka kazi nyingine tunaweza fanya kama hizi za usafi na kutunza mazingira hapa vijana wakipeana mikakati ya kuboreza mjiwao wa mblizi kwa usafi
Hakika ina pendeza mweshimiwa diwani kata ya utengule usongwe ambae pia ni mwenyekiti wa kijiji cha Mbalizi mwenye koti la kijani Mh. Eliah Mkono na mkuu wa kitengo cha kinga na tiba Mbeya vijijini  Emanuel Mwaigugu wakifurahia baada ya kuona vijana wamejitokoza kwa wingi kusafisha mji wao wa mbalizi
Mweshimiwa diwani akikagua kazi inayoendelea ya kuzibua mifereji na kutengeneza barabara
kazi inaendelea

Mweshimiwa diwani hakuwa nyumba katika kuwasaidia vijana 
Kwenye kazi utani pia upo ili kazi iende vizuri dada na kaka wanataniana
Safi sana vijana wa Mbalizi


Mratibu wa Vijana wazalendo wa mji wa Mbalizi Gordon Kalulunga,akiwa na kiongozi mwenzake wakifurahia jinsi kazi inavyoendelea
Hali halisi ya mifereji ya mbalizi ni hii sasa vijana ndiyo wanaizibua
Baada ya kuzibuliwa  kwa ujumla tunawapongeza sana vijana wa mbalizi kwa umoja wenu tunaomba na vijana wengine muige mfano huo wa kujitolea kufanya usafi zoezi la usafi litaendelea kesho
KABABU ZA TUKUYU
MSOSI WA LEO HUO
BAADA YA MAJUKUMU YA SIKU UNAPATA MSOSI SAFI KUTOKA KWA KAMANDA WA YESU MR DICK

Post a Comment