Sunday, December 9, 2012

SIKU YA UHURU NA RELI YETU WANANCHI WASHEREKEA KUANZA TENA KWA SAFARI ZAKE KAMA KAWAIDA

Dk. Mwakyembe Nimeona Kazi Yako Leo Jijini Mwanza

 Gari moshi likikaribia kufika stesheni ya Mwanza

Jengo la Shirika la Reli Mwanza
Tangazo likionyesha kuanza kwa safari za gari moshi

Abiria wakishuka baada ya gari moshi kufika steshen ya mwanza

Raia wa kigeni nao walikuwa miongoni mwa abiria waliowasili na gari moshi

Waandishi wa habari wakizungumza na naibu waziri wa uchukuzi Dk. Charles Tizeba

Moja ya mabehewa ya Gari Moshi

Wananchi waliofika kushuhudia kufika kwa gari moshi kwenya stesheni ya mwanza

Moja ya behewa la gari moshi likiwa katika hali mbaya

Naibu waziri wa uchukuzi Dk. Charles Tizebaakitoka kuzindua safari za gari moshi

Salamu kwa Dk Mwakyembe
Shikamoo Dk  Mwakyembe, habari ya Jumapili najua utakuwa umepumzika leo jumapili baada ya majukumu ya wiki iliyopita , mimi rafiki yako Mkami Jr baada ya kutoka kukusaidia kazi ya kukagua Reli ya Moshi, Nimeamua nisafiri mpaka kanda ya ziwa  nikusaidie tena kazi ya kukagua.

Dk Mwakyembe najua utashangaa kwanini nimejipa kazi hii bila kupewa kibali cha ofisi yako (Wizara ya uchukuzi), binafsi mimi nimejiajiri kufanya kazi zote za umma hivyo nadhani hata kazi hii ya kuja mwanza kukagua reli ni moja ya majukumu yangu kama mfanyakazi wa umma nisiye na ofisi wala mshahara au posho ya safari Dk mwakyembe usije shangaa siku nyingine nikafika hadi bandarini nikusaidie kupunguza msongamano wa makontena kwa kazi hizi nazofanya sihitaji kusifiwa, sihitaji posho ila nimeipenda tu kazi hii.

Dk Mwakyembe kama ambavyo niliyoona hali ya reli kule Moshi ambapo nilikuta Reli na majengo mabovu na behewa moja tu na sikuona dalili zozote za reli ile kufanya kazi na wala sikuona matumaini kama kuna siku itafanya kazi.

Leo hii Dk Mwakyembe umeniwahi huku Mwanza  sina budi kukupongeza wewe na timu yako kwa kazi nzuri kazi nzuri mnayofanya, leo nimeona Gari moshi likifika stesheni ya Mwanza na nimeomuona Naibu Waziri wako Dk  Dk. Charles Tizeba akizungumzia ujio wa safari za Gari moshi huku akisema maneno yenye kutia matumaini ikiwemo kuboresha usafiri huo kadri uwezo unapopatikana ni maneno ya faraja naamini amezungumza kwa niaba ya ofisi yako hivyo nawe unahusika kutekeleza aliyoyasema msaidizi wako, 
Pamoja na sifa ambazo wananchi wanakumwagia ila Rafiki yangu Dk Mwakyembe kazi ngumu ipo mbele yako ndio maana nikaona nikusaidie baadhi ya mambo , Jambo kubwa ambalo wananchi wamekuwa wakizungumzia usafiri huu ambao kwao ni ukombozi ni jambo la kuhujumiwa , mfano leo nimesikia kuwa wenye mabasi hutumika kuhujumu miundombinu ya reli na kufanya gari moshi kusimama kufanya kazi mara kwa mara, Sina ushahidi kuhusiana na jambo hili ila waswahili walisema lisemwalo lipo kama halipo laja..
Nikutakie kazi njema Dk harrison Mwakyembe na msaidizi wako  Dk. Charles Tizeba  na timu yako ya wizara ya uchukuzi na timu nzima ya Shirika la reli kwa kazi nzuri mnayoifanya ila inabidi mjipange kukabiliana na changamoto ikiwamo hujuma katika miundombinu na kuboresha magari moshi hapa nikiwa na maana kukarabati injini za gari moshi na kukarabati mabehewa yawe ya kisasa zaidi. 
Asante sana Dk Mwakyembe nikutakie mapumziko mema ya weekend na fikisha salamu  zangu kwa familia yako bila kumsahau dereva wako na kesho ukiwa ofisini fikisha salamu zangu kwa Katibu Muhtasi wako hawa ni watu muhimu pia kwenye kazi yako.

PICHA KWA HISANI YA Mkami Jr- (Mjengwa Blog-Mwanza)
 
LEO SIKU YA UHURU WA TANGANYIKA MIAKA 51

RAIS DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGOZA WATANZANIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA UHURU WA TANZANIA UWANJA WA UHURU

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dk.Jakaya Kikwete akiwasili katika gari maalum la Kijeshi na Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya  maadhimisho ya miaka 51 Uhuru wa Tanzania Bara 2012 yanayofanyika kila mwaka Desemba 9, Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “Uwajibikaji, Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu”
(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWEBLOG.COM)
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika maadhimisho hayo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika maadhimisho hayo
Kikosi cha Brass Band cha majeshi ya Ulinzi na usalama  kikitumbuiza katika maadhimisho hayo

Viongozi mbalimbali wakiwa katika maadhimisha hayo kutoka kulia ni Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mama Maria Nyerere, Rais wa Msumbiji Mh. Armando Guebuza,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Gharib Bilal na Mzee Ali Hassan Mwinyi rais Mstaafu wa awamu ya pili
Rais wa Msumbiji Mh. Armando Guebuza akipokewa  na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Said Meck Sadik mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Taifa.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mh. Joseph Kabila akipokewa  na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Said Meck Sadik mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Uhuru asubuhi hii.
Mama Maria Nyerere akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kuhudhuria maadhimisho hayo huku akisindikizwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadik.
Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho hayo.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa vimejipanga tayari kwa gwaride  la utii na heshima mbele ya Amiri jeshi Mkuu na Rais Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete.
Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili uwanjani hapo, katikati ni Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.
Rais Jakaya Kikwete akipokea gwaride la heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara yanayofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi
Rais Dk. Jakaya Kikwete kulia akipokea Gwaride la Heshima lililpokuwa likipita mbele yake wanaofuatia katika picha ni Rais wa Zanzibar Dk. Mohamed Shein, Rais wa Namibia Mh. Ifikepunye Pohamba na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakiwa katika maadhimisho hayo
Vijana wa chipukizi wakionyesha michezo na ujumbe mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo.
Hapa wakionyesha ukakamavu wao huku wakiwa wameshika silaha.
Kikosi cha wanaanga Jeshi la wananchi JWTZ kikitoa heshima kwa gwaride kali mbele ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jakmhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete
Kikosi cha ardhini Jeshi la wananchi la Tanzania JWTZ kipita kwa gwaride la heshima mbele ya Rais Dk. Jakaya Kikwete.
 

Mkutano Wa SADC Wamalizika Na Maazimio Yatolewa Katika Mkutano Wa Wanahabari

Baadhi ya wapiga picha za televisheni mbalimbali kutoka nchi wanachama wa SADC wakichukua matukio
 Rais Kikwete (kushoto) akiagana na Katibu wa SADC Tomaz Salomao baada ya kumalizika mkutano wa dharura wa SADC

 Rais kikwete (kushoto) akijibu masuali ya waandishi wa habari, (kati) Mk wa SADC Armando Guebuza (kulia)katibu wa SADC
 katibu wa SADC Tomaz Salomao (kulia) akisoma maazimio ya kikao, (shoto ) Mk wa SADC Rais Armando Guabuza wa Mozambique
Rais Jakaya Kikwete ( kushoto) akijibu masuali ya waandishi wa habari pichani hawapo
 na 

MTOTO WA MIAKA SABA AACHIWA MTOTO MCHANGA NA MWANAMKE ASIYEJULIKANA MBEYA

Mtoto Sharifu huyoo wa darasa la pili shule ya msingi Mbata akiletwa na wenzake kuja kuzungumza na waandishi wa habari waliokwenda kumtembelea shuleni hapo ili kujua kisa kilichomtokea mpaka akaachiwa mtoto
Kazi kweli kweli  watoto wakimwimbia wimbo wa kumtania sharifu kuwa kapakaziwa mtoto
Kwakweli tulikuta watoto wa shule ya msingi Mbata wamechangamka sana na kutupokea vizuri
Sharifu huyo katikati jamani  sasa mwachieni  tunashukuru kwa kutuletea tuongee nae
Rafiki yetu sharifu tayari wenzake wamemwachia na anaanza kutupa kisa cha kuachiwa mtoto mchanga

Sharifu 7 amesema yeye alipokua anatoka shule mida ya saa nne asubuhi kuna mama alimwita huyo mama alikuwa amebeba mtoto mchanga na ndipo mama huyo akamwambia sharifu naomba nisaidie kumbeba mtoto kwani nimesahau kuchukua kitu fulani nyumbani 

sharifu bila kujua akamchukua mtoto huyo  na mama wa mtoto akaondoka  sharifu anasema ilipita muda mrefu sana bila ya kumuona tena mama huyo na mtoto huyo alianza kulia na sharifu kuona mtoto analia nayeye akaanza kulia
Ndipo akatokea mwanafunzi huyu na kumuuliza sharifu mbona unalia na mtoto analia? sharifu akamjibu mwanafuzi mwenzake kuwa kuna mama kaniachia mtoto toka saa nne mpaka sasa sijamwona mama huyo nae nami nimechoka kumbeba ndipo mwanafunzi huyo akamwambia twende tumpeleke kwa walimu
Upendo Mwakipunda mwalimu wa shule ya msingi mbata amekiri kutokea kwa tukio hilo kweli walimpokea mtoto huyo na kumpeleka kituo cha polisi 
Mwaisango  mpiga picha wa tulio hili na mtoto sharifu baada ya kuongeanae habari wakiwa katika pozi la picha
Kwa ujumla baada ya kumaliza maongezi tulianza kuona jinsi watoto wakiwa katika michezo mbalimbali shuleni hapo dogo katulia dirishani mwa darasa lake huku akipata embe kwa raha zake

Wengine madirishani wengine wanachora ukuta ni furaha tu shuleni hapo

Wa kuruka kamba haya wa kucheza mpira sawa
Wanafunzi wakifurahia chandarua walichobuni shuleni hapo

Wakifurahia kutembelewa shuleni kwao (picha kwa hisani ya jem mwaisango)

KAMPENI YA VITA DHIDI YA UKIMWI, 

Kitanda katika Hoteli ya St, Monica iliyopo mjini Zanzibar, kikiwa kimetandikwa katika mtindo wa kuwakumbusha wateja umuhimu wa kujikinga na Ukimwi.

Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akitoa muhtsari kwa waandishi wa habari juu ya Taarifa kuhusu Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Msaada wa Maendeleo UNDAP 2011-2015 ambao unaelezea ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika kuendeleza nyanja mbalimbali ikiwemo kupunguza umaskini wakati wa Semina ya kuwapa uelewa waandishi wa habari juu ya Haki za Binadamu tukielekea kwenye maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani itakayoadhimishwa tarehe 10 Disemba mwaka huu.

Mwezeshaji wa Semina hiyo Katibu wa Jukwaa la Wahariri nchini Neville Meena akitoa changamoto kwa wanahabari kutumia fursa mafunzo hayo katika kuhabarisha jamii kuhusu kazi zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.

Mwakilishi Msaidizi wa UNICEF Bw. Paul Edwards akielezea nia ya Umoja wa Mataifa kuwakutanisha waandishi wa habari kila mwaka katika semina za mafunzo ambapo amesema jitihada za Umoja huo kutoa mchango katika juhudi endelevu za kupunguza umaskini na kupatikana kwa haki za Binadamu kulingana na visheni ya Maendeleo ya Taifa la Tanzania.

Mtalaam wa Program wa UNDP Bw. Amon Manyama akiwasilisha kwa wanahabari mpango kazi maalum wa miaka minne unaojulikana kama United Nations Development Assistance Plan 2011-2015 (UNDAP) uliotenga dola za Kimarekani Milioni 777 kwa Serikali ya Tanzania mpaka kukamilika ifikapo 2015.

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yasiyo na ukazi hapa nchini Bi. Aine Mushi akizungumzia jinsi mashirika hayo yanvyoweza kufanya kazi kwa pamoja 'Delivering As One' na Mashirika ya Umoja wa mataifa yenye ukazi hapa nchini.

Pichani Juu na Chini ni Washiriki wa Semina ya siku moja kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh. Mahfoudha Alley Hamid akizungumzia haki za msingi za Binadamu na wajibu wa vyombo vya habari katika kutetea haki hizo na kufichua pale zinapokiukwa ikiwemo kufuata maadili.

Afisa Mipango Mwandamizi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Bw. Anthony Rutabanzibwa akitoa somo jinsi waandishi wa habari wanavyotakiwa kuripoti masuala yanayohusu hakiza Binadamu bila kutoka nje maadili ya kazi zao.

Pichani Juu na Chini ni baadhi ya washiriki wakichangia mada na kutoa maoni wakati wa semina hiyo.

Mwenyekiti wa timu ya Mawasiliano ya Umoja Mataifa Bw. Yusuph Al Amin wakati wa semina hiyo akifafanua jinsi sekta ya mawasiliano vikiwemo vyombo vya habari inavyoweza kuchangia maendeleo na kufanikisha kufuatwa kwa haki za binadamu.

Afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi.Usia Ledama akitoa changamoto kwa wanahabari kusoma makabrasha yanayotolewa na mashirika mbalimbali ya umoja wa mataifa wakati wa mikutano na semina za kuelimishana kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusu jamii kwani kwa kufanya hivyo ndivyo watakavyoeweza kuelewa ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika kupunguza umaskini na kutetea haki za binadamu.

Baadhi ya Maofisa wa Umoja wa Mataifa na Wanahabari wakati wa Semina hiyo.

No comments: