Saturday, December 1, 2012

JK Arejea Kutokea Nairobi

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa kwa heshima wakati anaondoka jijini Nairobi, Kenya
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi wenzie wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na washiriki mwishoni mwa kikao cha nne cha Jumuiya nje ya Jengo la  Mikutano wa Kimataifa la Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Kenya.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie i wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakishuhudia utiwaji saini mkataba wa haja ya kuwepo kwa ushirikiano wa kibiashara kati ya Marekani na nchi za Jumuiya hiyo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Kenya. Zoezi hili lilifanywa baina ya Mawaziri wa Bishara wa nchi wanachama wa Jumuiya na Kaimu Waziri wa Bishara wa Marekani Bi Rebecca Blank aliyehudhuria kikao hicho
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia Rais Mwai Kibaki wa Kenya akimkabidhi nyundo Rais Yoweri Muzeveni kama ishara ya kukabidhi Uienyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Kenya
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa nne wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, 
Kenya

PICHA NA IKULU
 JK AWASILI MKOANI LINDI KWA AJILI YA MAADHIMOSHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI
 Viongozi mbalimbali wakimlaki Rais Jakaya Kikwete kwenye uwanja wa ndege wa Lindi mkoani Lindi leo asubuhi hii
 Rais Jakaya Kikwete akiwa katika uwanja wa ndege wa Lindi mara baada ya kuwasili mkoani Lindi  asubuhi hii ambako anahudhuria maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yanayofanyika Kitaifa  kwenye uwanja wa Ilulu mkoani humo, wadau mbaloimbali wanaojihusisha na masuala ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi wamejitokeza na kushiriki katika maonyesho yenye lengo la kuelimisha na kukumbusha juu ya hatari za ugonjwa wa ukimwi na mbinu mbalimbali za kupambana nao Kushoto ni Mama Salma mke wa Ras Jakaya Kikwete na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh. Ludovick Mwananzila
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Mh. Hussein Mwinyi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Lindi Mkoani humo katikati ni Mh. William Lukuvi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera na uratibu wa bunge
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Lindi mjini Salum Barwany wakati alipowasili mjini Lindi asubuhi hii kwenye uwanja wa ndege wa Lindi.
Post a Comment