Tuesday, December 4, 2012

Nafasi Za Ufadhili Kwa Wasichana


RafikiElimu  FOUNDATION  ni  Taasisi  isiyokuwa  ya  kiserikali  inayo  jishughulisha  na  Maendeleo  ya  jamii. Taasisi  inapenda  kutangaza  nafasi  za  ufadhili  wa  masomo  ya  sekondari  kwa  waombaji  wenye  sifa  zifuatazo  :
1. Awe    yatima  wa  jinsia  ya  kike  au  awe  masichana  anayeishi  katika  mazingira  magumu.
2.Awe  raia  wa  Tanzania.
3. Awe  anajiandaa  kujiunga  na  masomo  ya  kidato  cha  kwanza  kuanzia  Januari  2013. AU 
4. Awe  anajiandaa  kujiunga  na  masomo  ya  kidato  cha  tano   katika  mwaka  wa  masomo 2013/14.
5. Awe   ni  mwanafunzi  ambaye  tayari  anasoma sekondari   lakini   anashindwa/ ama  ameshindwa  kuendelea  na  masomo  yake  kutokana  na  kufiwa  na  wazazi ama  walezi wake.

*  N.B  : Ufadhili  wa  masomo  kwa  kidato  cha  tano  na  sita   utatolewa  kwa  wanao  taka  kuchukua  masomo  nya  michepuo  ya  ARTS

Tuma  barua  yako  ya  maombi  ya  ufadhili  wa  masomo  kwenda  kwa

MKURUGENZI  MTENDAJI,
RAFIKIELIMU   FOUNDATION,
S.L.P  35967,
DAR  ES  SALAAM.

*   Katika  barua  yako  ambatanisha  barua  ya  serikali  ya  mtaa  unaoishi, cheti  chako  cha  kuzaliwa ama  Hati  ya  Kiapo " AFFIDAVIT " , picha  zako nne  za  rangi, pamoja  na  vielelezo  vingine  vinavyo  thibitisha  kwamba  wewe  ni  yatima.

* Maombi  yako  yatufikie  kabla  ya  tarehe   07  JANUARY 2013.

*  Maombi  yanaweza  kutumwa  na  msimamizi  wa  mwanafunzi  husika  kwa  niaba  yake.
Kwa  maelezo  zaidi  tembelea  ;  www. rafikielimu. blogspot.com

na wakati huohuo

Wenye Ulemavu Wakumbukwa...!


Na: Mwandishi Maalum
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ametaka kuwapo kwa msukumo mpya wenye lengo la kujenga jamii inayothamini utofauti  baina ya watu na ushirikishwaji.
Ban Ki Moon ameyasema  hayo katika  k salamu zake wakati wa maadhimisho ya  siku ya Kimataifa ya watu wenye ulemavu. Maadhisho hayo hufanyika kila desemba tatu.
Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa  ameeleza kuwa, kwa kutambua nafasi  na mchango wa watu wenye ulemavu katika sekta mbalimbali, ndiyo maana Umoja wa Mataifa umeandaa  mkutano wa kilele wa wakuu wa  nchi na serikali,  mkutano ambao utajadili kwa kina masuala ya watu wenye ulemavu na maendeleo.
 “Maadhamisho haya ya leo “. Akasema   Ban Ki Moon,  “ Ni mwanzo wa maandalizi ya mkutano huo wa kilele  kwa lengo hasa la kuchochea  na kuhakikisha kwamba haki, mahitaji na mchango wa watu wenye ulemavu vinazingatiwa kwa ukamilifu.
Mkutano huo utafanyika   Septemba 23  mwaka 2013 ikiwa ni sehemu ya  Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la 68 la Umoja wa Mataifa.  kufanyika kwake kunatokana na mchango na msukumo mkubwa  uliofanywa na  Balozi za Tanzania na Ufilipioo katika Umoja wa Mataifa wa kuandaa na kusimamia majadiliano yaliyozaa maazimio mbalimbali ambayo hatimaye yalijenga ushawishi mkubwa wa kuwa na mkutano huo katika ngazi ya viongozi wakuu wa nchi na serikali.
Maazimio hayo   likiwamo lililopitishwa hivi karibuni, yanahimiza pamoja na mambo mengine, ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika shughuli  na maamuzi  yanayohusu masuala ya maendeleo ikiwamo utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya millennia.
Aidha maamizio hayo yanazihimiza serikali na taasisi za kimataifa    kuwa na mipango madhubuti na endelevu ya ukusanyaji wa raslimali zitakazohakikisha ushiriki wa  kundi hilo la jamii  na  halikadhalika maazimio hayo yanaisisitiza pia haja na umuhimu  wa kuwa na taarifa na takwimu sahihi za watu wenye ulemavu. 
Katika maadhimisho yaliyofanyika hapa Makao Makuu   yakiambatana pia na mijadala mbalimbali, Ban Ki Moon anasema  watu wenye ulemavu wana mchango mkubwa katika jamii. Na kwamba wanaweza kufanya vizuri zaidi ikiwa vikwazo vinavyokwamisha ushiriki wao vitaondolewa. 
Aidha Ban Ki moon  ameeleza kwamba  changamoto kubwa ni katika utoaji wa fursa  sawa na ukidhi wa mahitajio  ya msingi ya watu wenye ulemavu.
“ kwa umoja wetu lazima tuhakikishe kwamba tunajitahidi kutekeleza  malengo ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watu wenye Ulemavu.  Kuondoa ubaguzi na kutoshirikishwa, na kujenga jamii ambayo inathamini na kuhimiza ushirikishwaji” akasema Ban Ki Moon.
Inakadiriwa kwamba watu bilioni moja sawa na  asilimi 15 ya  idadi ya watu wote  duniani wanaishi na aina moja ama nyingine ya ulemavu.
Umoja wa Mataifa umekuwa ukiadhimisha siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu tangu mwaka 1992, na   mwaka 2007 ulipitishwa  Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa  Haki za Watu wenye  Ulemavu na ukaanza kufanya kazi mwaka 2008.
Mkataba huo pamoja na mambo mengine unatambua vikwazo  vinavyowakabili watu wenye ulemavu   kwa sababu tu ya ulemavu wao, na kwa sababu hiyo Mkataba  unatamka  kwamba watu wenye ulemavu wana haki ya msingi ya kupata elimu  jumuishi.
Hadi kufikia mwezi Novemba mwaka huu nchi 126  sawa na theluthi mbili   ya wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa zilikuwa zimeuridhia  Mkataba huo.
Post a Comment