Wednesday, December 12, 2012

KUMEKUCHA TENA

 

CHADEMA WADAIWA KUVUNJA MASANDUKU YA KURA NA KUIBA FEDHA ZA UCHAGUZI

Vurugu Chunya


WATU 13 akiwemo diwani wa viti maalumu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kata ya saza Benadetha Zacharia(38) wanashikiliwa na jershi la polisi kwa kufanya vurugu zilizosababisha uharibifu wa mali ya umma yakiwemo masanduku ya kupigia kura.
Wengine ni katibu wa Chadema kata ya Saza wilayani Chunya Braison Mwasimba(34),John Mponzayo(52),Seleman Tanganyika(24),Ambokile Francis(23),Amos Joseph(24),Abdul Mwandeule(20),Christopher Mwanjayo(37), Baraka Saul(19),Musa Mnyonga(32),Essa Pius(18),Marco Gibson(25) wote wakazi wa kata ya Saza na Paradiso Emanuel(26) mkazi wa kijiji cha Njenjele wilayani Mbeya. Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwan Athuman alisema kuwa mnamo desemba 8 mwaka huu majira ya saa 11:15 katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata ya Saza baadhi ya wananchi wakiongozwa na watuhumiwa waliamua kujichukulia sheria mikononi na kusababisha uharibifu wa mali za umma. Kamanda Athuman alitaja uharibifu uliofanyika kuwa ni kuvunjwa kwa kioo cha mbele cha gari yenye namba SM 3830 Toyota Landcruiser mali ya halmashauri ya wilaya ya Chunya,kuvunja mlango na dirisha la ofisi ya afisa mtendaji kata. Alisema hbaada ya uharibifu huyo watuhumiwa waliingia ndani ya ofisi hiyo na kuharibu masanduku 24 ya kupigia kura ambapo thamani ya mali zote bado haujafahamika. Alisema chanzo cha vurugu hizo ilikuwa kushinikiza kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya mwenyekiti wa kijiji na vitongoji uliokuwa ufanyike siku ya jumapili. Kufuatia vurugu hizo uchaguzi huo ililazimu kusogezwa mbele siku moja na kufanyika jana(Disemba 10) huktaratibu za kisheria zikiendelea ikiwemo kufikishwa jana mahakamani katoka mahakama ya wilaya ya Chunya watuhumiwa 12 na kusomewa mashitaka. Ukiachilia mbali shitaka la uharibifu wa mali za umma linalowakabili washitakiwa wote mahakamani hapo washitakiwa Amos Joseph,Braison Mwasimba na Paradiso Emanuel wanakabiliwa na shitaka jingine la unyang’anyi. Alisema washitakiwa hao walifanya unyang’anyi wa fedha kiasi cha shilingi 2,150,000 zilizokuwa sehemu ya gharama za uchaguzi,simu ya kiganjani na saa ya mkononi.
Habari kwa hisani ya Joachim Nyambo picha Kamanga

 MBEYA TENA

WASHATUPA TENA KITOTO KICHANGA CHAKUTWA KWENYE DAMPO LA MAPAMBANO ASUBUHI YA LEO, MAMA WA MTOTO BADO HAJULIKANI ALIKO. MASHUHUDA WA TUKIO HILO WAANGUA KILIO KWENYE DAMPO HUKU WAKILAANI KITENDO HICHO

MWILI WA KICHANGA HICHO, UKIWA UMEFUNIKWA NA KITENGE CHA MWANAMKE ALIYEHUSIKA KUKITUPA KITOTO HICHO
 BAADHI YA WAKAZI WA KATA YA IYELA MTAA WA MAPAMBANO WAKIWA NA HUZUNI KUBWA BAADA YA KUFIKA ENEO KILIPOTUPWA KICHANGA HICHO
 HAPA MWILI WA KICHANGA HICHO UKIONEKANA BAADA YA KUONDOLEWA KITENGE SAMAHANI KWA PICHA HIZI KWAKWELI INASIKITISHA SANA 
MWENYEKITI WA MTAA WA MAPAMBANO EXSON MWAKALOBO AKIWASILIANA NA JESHI LA POLISI KWA AJILI YA HATUA ZAIDI ZA UCHUNGUZI  kwa hisani ya Jem

Mandela augua mapafu,alazwa

Serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa rais wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela amepatwa tena na ugonjwa wa mapafu na anaendelea vyema na matibabu .
Bwana Mandela ambaye ana umri wa miaka 94, amekuwa hospitalini mjini Pretoria tangu Jumamosi .
Hii ni taarifa ya uhakika ya kwanza kutolewa kuhusu afya ya kiongozi huyo aliyepinga utawala ubaguzi wa rangi . Bw mandela alitibiwa mapafu miaka 2 iliyopita.
Habari kuwa Mandelela anatibiwa ugonjwa wa mapafu, bila shaka imemaliza wasiwasi wa siku kadhaa kuhusu ukosefu wa taarifa zozote kuhusu afya yake
Wananchi wa Afrika Kusini wanafuatilia kwa maakini taarifa za afya ya Mandela
Msemaji wa rais huyo mstaafu hakueleza kuhusu ikiwa hali ya Mandela ni mbaya sana au itakuwa sawa lakini alisisitiza kuwa anaendelea kupokea matibabu.
Miaka miwili iliyopita, hali kama hii ilijitokeza kuhusu Mandela baada ya kulazwa hospitalini kwa tatizo la kupumua ingawa aliweza kutibiwa vyema.
Mandela pia alipokea matibabu ya kifua kikuu wakati alipokuwa gerezani, katika kisiwa cha Robben na afya yake, inaendelea kuwavutia watu wengi.
Mac Maharaj, msemaji wa rais, alisema kuwa wanajitahidi kadri ya uwezo wao kuweza kufahamisha watu,kuhusu afya yake lakini pia alitaka kutoingilia kazi ya madaktari pamoja na kutaka jamaa za Mandela kuruhusiwa kumzuru bila matatizo tyoyote.

JK: Apokea Majengo Mapya Matatu Ya Huduma Za Mama Na Mtoto


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mbunge wa Ubungo Mhe John Mnyika na Balozi wa Korea kwa pamoja wakifungua rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sinza Palestine Kinondoni jijini Dar es salaam leo December 12, 2012



Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mbunge wa Ubungo Mhe John Mnyika na Balozi wa Korea kwa pamoja wakikata utepe kufungua rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sinza Palestine Kinondoni jijini Dar es salaam leo December 12, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete na Balozi wa Korea kwa pamoja wakitembelea sehemu ya chumba cha upasuaji mkubwa chenye vifaa vya kisasa baada ya kufungua  rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Ilala ijini Dar es salaam leo December 12, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete wakimsalimia mzazi aliyejfungua salama alipofanya ziara baada ya kufungua  rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sinza Palestine Kinondoni jijini Dar es salaam leo December 12, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipewa saluti alipowasili kufungua rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sinza Palestine Kinondoni jijini Dar es salaam leo December 12, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mbunge wa Ubungo Mhe John Mnyika na Balozi wa Korea  pamoja na madaktari na wauguzi katika picha ya pamoja  baada ya kufungua rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sinza Palestine Kinondoni jijini Dar es salaam leo December 12, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete na Balozi wa Korea kwa pamoja katika picha ya pamoja na madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Mnazi mmoja  baada ya kufungua  rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Ilala ijini Dar es salaam leo December 12, 2012
                        NA

Mnyika Aanika Mafisadi 16 Tanesco


 Na : Raymond Kaminyoge
MBUNGE wa Ubungo John Mnyika, ametaja majina ya watu 16 ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambao amewahusisha na ufisadi ndani ya shirila hilo la umma.
Mnyika ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Madini na Nishati alisema watu hao ndio wanaoshirikiana kuihujumu Tanesco na kuliingiza taifa katika hasara.


Kati ya majina hayo ambayo ameyaita kuwa ni ya awamu ya kwanza wamo baadhi ya waliokuwa watendaji wa shirika hilo ambao wamesimamishwa kupisha uchunguzi unaofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).


Alipoulizwa wiki iliyopita kuhusu uchunguzi huo, GAG Ludovick Utouh alisema uchunguzi huo umeshakamilika na kilichokuwa kikisubiriwa ni kuikabidhi ripoti hiyo kwa bodi ya Tanesco.


Mnyika aliwataja vigogo wengine watatu wa Tanesco na kueleza kuwa walifanya uzembe na kushindwa kusimamia sheria ya ununuzi wa umma na kupendekeza kampuni mbili kupewa zabuni, licha ya kuwa hazikutimiza masharti kwa sababu ya mgongano wa maslahi.

Mnyika alipendekeza vigogo hao kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Aliwataja watumishi wawili ambao walishindwa kutoa taarifa za ukiukaji wa vigezo vya utoaji wa zabuni namba PA/001/09/HQ/W/014 na kufanya kampuni moja kati ya hizo mblii kupewa zabuni.

Alisema watendaji hao walichangia kufanya kampuni hiyo kupewa zabuni pamoja na kwamba haikuwa na fedha na kuiwezesha kupewa malipo ya asilimia za ziada kinyume na mkataba.

Akapendekeza watendaji hao kuchuliliwa hatua za kinishamu. nMnyika aliwataja watumishi wengine sita wa Tanesco ambao kwa pamoja walifanya uamuzi uliosababisha kutolewa kwa mkataba namba PA/001/HQ/W/14 wa Machi 11,2010 kwa kampuni hiyo bila kuzingatia uwezo wa kitaalam, kifedha na hivyo kukiuka sheria ya ununuzi wa umma.

Alisema hao wanatakiwa kuchukuliwa hatua ili kuwadhibiti watumishi wa umma wanaoliingiza taifa katika mikataba mibovu.

Mnyika katika taarifa yake hiyo aliwataja wafanyakazi watatu wa Tanesco akieleza kuwa walihusika katika kutoa mapendekezo yaliyowezesha kampuni ya McDonald kupewa mkataba wa zabuni kinyemela.

Mnyika alipendekeza wachukuliwe hatua za kisheria ili kuepusha Tanesco kuingia mikataba kuliongezea shirika mzigo wa gharama na kusababisha ongezeko la bei ya umeme.
PIA

Taarifa ya Dar City Press Juu ya Tukio la Mwandishi Kupigwa Risasi Dar

Shabaan Matutu (30) aliyejeruhiwa begani kwa risasi na polisi na kulazwa katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
KUFUATIA kupigwa risasi, kujeruhiwa begani na kulazwa katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa mwandishi wa Tanzania Daima Bwana
Shabani Matutu (30) ambaye pia ni mwanachama hai wa Dar City Press
Club(DCPC), uongozi wa Klabu uliamua kufuatilia tukio hilo kwa karibu
ili kujua na kuhakiki kwa kina yaliyotokea na sababu zilizopelekea
hayo kutokea.
Kutokana na hayo DCPC imebaini yafuatayo.
1. Ni kweli kwamba Shabaan matutu(30) alipigwa risasi na askari
wa jeshi la Polisi mwenye namba F.8991 D/C Idrissa nyumbani kwa
Shabaan kimakosa baada ya askari huyo na wenzake wanne kufungua kwa
nguvu na bila ya kujitambulisha kwa mwenye nyumba (Shabaan na Mkewe)
licha ya kuombwa kufanya hivyo kabla.
2. Kuna maelezo yanayokinzana katika kuelezea jinsi tukio hilo
lilivyotokea kwa pande mbili zinazohusika yaani maelezo ya shabaan na
ya polisi
3. Kwamba sababu za askari polisi hao kufanya hivyo hazikuwa
zimefanyiwa uchunguzi wa kutosha hadi kujiridhisha kuchukua hatua hiyo
hivyo hata wao walikiri kukosea pamoja na kueleza kwamba Shabaan ndiye
aliyeaanza kuwashambulia askari Polisi kabla ya wao kumjeruhi kwa
risasi.
4. Shabaan mpaka sasa anaendelea na matibabu licha ya kuuguza
majeraha aliyosababishiwa na polisi na kwamba ameshauriwa kitaalamu
kupumzika nay eye binafsi ameomba asibughudhiwe ili afya yake irejee
haraka na kwamba pindi atakapokuwa katika hali nzuri zaidi ya sasa kwa
mujibu wa ushauri huo wa kitabibu, atawasiliana na yeyote wakiwemo
polisi ambao wamekuwa wakimmghasi kwa kuja kumhoji mara kwa mara.
Kwa sababu hizo basi Dar es salaam City Press Club
1. Tunaiomba Serikali na mamlaka za juu zaidi ya jeshi la Polisi
hususan Wizara ya mambo ya ndani ifanye uchunguzi wa kina na huru
wenye kuhusisha taasisi wakilishi katika jamii juu ya tukio hilo na
kulichunguza jeshi la polisi linavyofanya kazi zake kwa kuzingatia
kanuni na sheria.
2. Tunalitaka Jeshi la Polisi liache mara moja kutuma askari wake
kwenda kwa Shabaan kwa lengo la kumhoji ama kutaka atoe maelezo yake
kwa viongozi wa jeshi hilo ilhari walishamtuhumu na kueleza kuwa
aliwashambulia Polisi kwa Panga kabla ya wao kumfyatulia risasi.
Tunasema hivi kwa kuzingatia kanuni za afya na haki za msingi za
binadamu.
3. Tunalitaka Jeshi la Polisi liueleze umma bila kuficha ukweli
na kwa jinsi ile ile ambayo lilitoa taarifa mara baada ya tukio,
lieleze kwa nini linatumia habari na vyanzo dhanifu kujeruhi na
kuhatarisha maisha ya raia wasio na kosa huku likitoa maelezo
yasiyofanyiwa uchunguzi.
4. Mwisho tunalitaka jeshi la Polisi lenyewe lijitafiti na
kujipanga upya ili liweze kufanya kazi kisayansi na weledi kama
ambavyo viongozi wake wamekuwa wakijinadi mbele ya vyombo vya habari.
Tamko hili limetolewa leo Tarehe 08/Desemba/2012.
Joseph Kayinga
Katibu Mkuu-DCPC

No comments: