Tuesday, December 11, 2012

HI NI KALI NA HATARI KULIKO.....


NI KWELI TULIBURUDIKA MIAKA 51 YA UHURU LAKINI WATOTO NYAMBULI MGANGA (3) NA GOZBERT BWERE (3) HAWANA ULINZI WA KUTOSHA

Ukiangalia katika picha hii utawakumbuka watoto hawa Nyambuli Mganga (5) na Gozbert Bwere (3) kutoka mkoani Mara ambao walikuja jijini Dar es salaam na kikundi cha ngoma za asili kutoka mkoani humo, kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, watoto hawa walitia fora sana mbele ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Bara Dk. Jakaya Kikwete na wageni mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi waliohudhuria katika maadhimisho hayo.
Shughuli kubwa iliyofanywa na mtoto mdogo Gozbert Bwere (3)katika upigaji wa ngoma ndiyo iliyowafanya baadhi ya viongozi wa kisiasa na Serikali kuenda kumtunza mtoto huyo, ambapo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC CCM Nape Nnauye na Katibu Mwenezi wa chama hicho Mwigulu Nchemba walienda na kumtunza mtoto huyo kwa umahiri wake katika kupiga ngoma.
Jana nilipita maeneo ya Manzese katika moja ya kiota cha siku nyingi Frieds Coner na kumkuta mmoja wa wanakikundi akiwa na watoto hao nje ya hoteli hiyo, akajitambulisha kwamba yeye ni Mpalala Mwendwa na ni  msaidizi wa Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Mara akaongeza na kusema yeye amefuatana na kikundi hicho kama mmoja wa viongozi wa msafara kutoka mkoani Mara.
Kilichinisikitisha sana ni kiongozi huyo kuonekana akiwa ameshika chupa ya pombe kali aina ya Value akionekana kuwanywesha watoto hao pombe hiyo kwa kifuniko cha chupa hiyo, huku mtoto Gozbert Bwere akikunja sura mara baada ya kunywa pombe hiyo ikiwa ni kuashiria kwamba hawezi kumudu kuinywa.
Kitu kilichiniumiza sana nilipoongea na  Bwana Mpalala Mwendwa aliniamba kuwa wazazi wa watoto hao wamebaki Musoma. Hivyo watoto hao wako chini ya uangalizi wa kikundi hicho pekee jambo ambalo si jema na kuna uwezekano mkubwa wa kumomonyoka kwa maadili ya watoto hao, kwani hawana ulinzi wa kotosha kama ilivyoshuhudiwa jana wakiwa wananyweshwa  pombe hiyo ya Value na kiongozi huyo.
         Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC CCM Nape Nnauye na Katibu Mwenezi wa chama hicho Mwigulu Nchemba wakirejea jukwaani mara baada ya kuwatunza watoto hao Nyambuli na Gozbert wakati wakicheza ngoma katika maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwenye uwanja wa Uhuru.
        Mtoto Gozbert Bwere (3) akionyesha uwezo wake katika kupiga ngoma huku akiwa amelala chini katika maadhimisho hayo.
        Mtoto Gozbert Bwere (3) akifanya vitu vyake  katika kupiga ngoma katika maadhimisho hayo

MAISHA PLUS YAMKUTANISHA IBRAHIM NA NDUGU ZAKE, ALITELEKEZWA NA MAMA YAKE AKIWA MCHANGA

       Ibrahim Matebu akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam mara baada ya kukutanishwa na ndugu zake kufuatia kipindi cha Maisha Plus kumhoji na kuelezea matatizo yake mara baada ya kutelekezwa na mama yake Hedinesta Kileo kwenye basi mpakani mwa Tanzania na Kenya, ambapo kijana huyo akiwa bado mchanga aliokotwa na mama wa Kisomali ambaye alimlea mpaka alipofikisha miaka minne na yeye akamtelekeza , ndipo alipochukuliwa na serikali ya kenya akalelewa na kusoma huko.
Ibrahim alirudi nchini kwa kumfuata rafiki yake hakumtaja jina ambaye inadaiwa ni mkenya wakawa wanaishi mkoani Arusha, na ndipo alipofanikiwa kuingia katika kuwania nafasi ya kushiriki katika Shindano la  Maisha Plus, hata hivyo hakufanikiwa kupita  katika mchujo huo.
Mama mkubwa wa Ibrahim alimfananisha Ibrahim na mshindi wa pili wa Maisha Plus Venance Mushi ambaye ukiangalia kwa kiasi wanafanana, kutokana na historia aliyoitoa Ibrahim jambo lililompa mashaka kwani mdogo wake Hedinesta aliwahi kuwa na mimba lakini haikujulikana kilitokea nini mara baada ya kukimbia nyumbani kwao Arusha na kwenda kwa dada yake huko mpakani mwa kenya na Tanzania ambako inadaiwa alijifungua na baada ya mwezi mmoja akumtelekeza mtoto huyo, aliyeshika kipaza sauti ni Emanuel Anderson ndugu yake na Ibrahim
      Kutoka kulia ni Emmanuel Anderson ndugu yake na Ibrahim, Ibrahim Mwenyewe na Venance Mushi ambaye ni mshindi wa pili wa Maisha Plus.
Mama Mkubwa wa Ibrahim akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dares salaam mara baada ya kukutana na mwanaye huyo ambaye ni mtoto wa mdogo wake Hedinesta Kileo, ambapo ameishukuru Maisha Plus kwa kumkutanisha na mtoto wake, lakini pia akaomba radhi kwa wazazi wa Venace Mushi na Venance mwenyewe kwa usumbufu uliotokea baada tukio hilo la kumfananisha mtoto wao  Ibrahim na Venance kutokana na matukio yaliyomkuta Ibrahim akiwa bado mdogo
Mkurugenzi wa Maisha Plus Masoud Kipanya akizungumzia sakata hilo ambapo amesema Maisha Plus mbali ya kazi yake ya kawaida kama shindano, lakini imemkutanisha Ibrahim na ndugu zake na akasema kumbukumbu za picha zimetusaidia kujua ukweli wa jambo lenyewe kuhusu sakata la Ibrahim.
 NA

Maadhimisho Ya Siku Ya Haki Za Binadamu Duniani Na Miaka 64 Ya Tamko La Kimataifa La Haki Za BinadamuMeza Kuu ikipokea maandamano ya Wanafunzi na Taasisi mbalimbali za Kiserikali na zisizo za Kiserikali wakati sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu zilizofanyika jijini Dar leo.

Jaji Kiongozi (Mstaafu) Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh.Amiri Ramadhani Manento akisoma hotuba yake katika maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu ambapo aliwasilisha Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa nchi zote zihakikishe kuwa zinafuata maazimio ya tamko la haki za binadamu na wananchi wake wanufaike na haki zilizomo ndani yake.

Mwanasheria Mkuu wa Sreikali Jaji Frederick Werema akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa ambapo amesema chini ya mpango wa pamoja, Umoja wa Mataifa nchini Tanzania unasaidia vitengo muhimu vya serikali na wadau wengine wa mzunguko wa Haki za Binadamu, kwa mfano ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na idadi kubwa ya Asasi zisizo za kiserikali zinazohusika na masuala ya Haki za Binadamu.
Vilevile amesema Umoja wa Mataifa unaendelea kuinga mkono serikali kufuatilia ahadi zilizotolewa kwa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na mapendekezo yakiwemo kutoka katika Bodi za Mikataba ya haki za Binadamu.

Afisa Mipango kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Kanda ya Afrika Mashariki Bw. Abdu Mohammed akisoma hotuba kwa niaba ya Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ambapo amesisitiza kila raia anapaswa kuwa na haki na fursa ya kushiriki katika masuala ya umma, moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi huru wa kuchaguliwa, pia kila binadamu ana haki ya kupiga kura na kuchaguli na na kuweza kufikia huduma za kijamii sambamba uhuru wa kujieleza, kukusanyika na kuungana.
Amongeza kuwa haki hizi zinatakiwa kumhusu kila mtu na hakuna hata mmoja atakaye baguliwa kwa moja kati ya hizo kwa sababu ni mwanamke, au anatoka katika kundi dogo, au anaabudu katika dini Fulani, au kwa sababu ni shoga, au ana ulemavu, anaamini siasa Fulani, au mkimbizi au ana rangi fulani, anatoka katika kabila Fulani.

Mgeni rasmi Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisoma hotuba yake ambapo amesema Pamoja na kuadhimisha kumbukumbu ya Siku ya Haki za Binadamu, pia tunaadhimisha kumbukumbu ya Siku ya Kimataifa ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa pamoja. Kaulimbiu ya mwaka huu katika Kupambana na Rushwa ni “Unaweza kuzuia rushwa, chukua hatua sasa”. Kauli hii inaonesha umuhimu wa Wananchi wa rika zote kupiga vita rushwa.
Mh. Pinda amesema hatua ya kuunganisha maadhimisho haya na kufanyika sehemu moja kunapunguza gharama kwa upande wa Serikali, na pia kunatoa nafasi kwa Wananchi kufahamu umuhimu wa siku zote mbili bila kulazimika kuondoka eneo moja la tukio kwenda eneo jingine. Napenda kuzipongeza Taasisi zote husika kwa kuunganisha matukio haya mawili na kuadhimisha sehemu moja na kwa wakati mmoja.
Ameongeza kuwa Huu ni mwaka wa tano tangu Taifa letu lilipoanza kuadhimisha siku hii Kitaifa. Kaulimbiu ya Kimataifa kwa mwaka huu ni: “Sauti yangu inachangia” (My voice counts). Ujumbe huu unatukumbusha kushiriki katika kutoa maoni katika shughuli mbalimbali za Kijamii au Kitaifa.

Mh. Waziri mkuu Mizengo Pinda akizindua taarifa ya miaka 10 ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB). Wanaoshuhudia uzinduzi huo ni Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Mathias Chikawe (kushoto) na Naibu wake Mh. Angellah Kairuki (kulia).

Sasa imezinduliwa rasmi….Mh. Waziri mkuu Pinda akionyesha ripoti hiyo kwa wageni waalikwa (hawapo pichani). Kulia ni Jaji Kiongozi (Mstaafu) Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh.Amiri Ramadhani Manento na Kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Mathias Chikawe (kushoto).

Waziri Mkuu Pinda akipitia ripoti hiyo.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akipitia nakala taarifa ya miaka 10 ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Kikundi cha Wana wandime ya kwetu ngoma wakitoa burudani wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

Pichani Juu na Chini ni Wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za serikali, Wanafunzi wa shule za Sekondari, Wadau wa Haki za Binadamu na Wananchi wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu.


Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika picha ya pamoja na Viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Waziri wa Katiba na Sheria na Naibu wake.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiagana na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh. Mahfoudha Alley Hamid.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiondoka katika viwanja vya Mnazi Mmoja baada ya sherehe za maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu huku akisindikizwa na Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. picha na ofisi ya waziri mkuu

UTAMADUNI WETU WATANZANIA NI UPI?

       Kikundi cha halaiki chenye watoto 2,625 kutoka Tanzania Bara na Visiwani kikionesha sura mbalimbali ya  kitabu, ugonjwa wa mapambano dhidi ya malaria, nchi yangu Tanzania ,miaka 51 ya UHURU, Maliasili na Utalii.. (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO)
      Kikundi cha ngoma cha Taifa kutoka Rwanda kikionyesha umahiri wake wakati wa maadimisho  ya miaka 51 ya Uhuru a Tanzania Bara jana katika Uwanja wa UHURU jijini Dar es Salaam, ambapo Rais Kikwete aliwashukuru wasanii  hao kwa kuja Tanzania  katika maadhimisho.(Picha MAELEZO

Post a Comment