Thursday, January 17, 2013

ANUSURIKA KUUWAWA KWA WIZI WA MOTA ILOMBA MBEYA


JAMAA ANAEHISIWA KUWA MWIZI WA MOTA AMEPATA KIPIGO KIKUBWA NUSURA AUWAWE KWA HASIRA ZA WANANCHI AMEJULIKANA KWA JINA MOJA TU WILLY
JAMAA HUYU INASEMEKANA NI MZOEFU SANA WA WIZI ANATAFUTWA SANA ENEO LA ISYESYE JIJINI MBEYA KWA TUHUMA ZAKE ZA WIZI
HII NDIYO MOTA ALIYOKUTWA NAYO HUYO ANAEHISIWA KUWA MWIZI
JAMAA ASHUKURU POLISI LASIVYO MAUTI YANGEMKUTA


PICHA NA Jem

Manumba mahututi, alazwa Aga Khan


 
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi (DCI), Kamishna Robert Manumba 
Na:  Raymond Kaminyoge
HALI ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi (DCI), Kamishna Robert Manumba ni mbaya na amelazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU), Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.Habari zilizopatikana jana zilieleza kuwa Manumba amelazwa hospitalini hapo baada ya kusumbuliwa na maradhi kadhaa, ikiwamo figo.

Mabasi ya kasi Dar kuajiri 80,000

 

 
Na Elias Msuya 
“Dar es Salaam inakuwa kwa kasi, msongamano wa magari ni tatizo kwa ukuaji wa uchumi kwa sababu unapunguza uzalishaji kwa kupoteza muda wa watumiaji wa barabara. Hali hiyo inatishia ukuaji wa baadaye wa mji na nchi kwa jumla na unaongeza uharibifu wa mazingira,” ilisema taarifa ya WB na kuongeza

0
BODI ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia (WB), imeidhinisha Dola za Marekani 100 milioni kwa ajili ya Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi (BRT) jijini Dar es Salaam.


Taarifa ya benki hiyo iliyopatikana Dar es Salaam jana imeeleza kuwa mradi huo utakaozalisha ajira 80,000 kwa Watanzania, utasaidia abiria 300,000.

“Ajira hizo 80,000 zitapatikana hadi mwaka 2015 na zitatokana na kazi zinazotarajiwa kuwapo, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, vituo vya abiria, vituo vidogo na vituo vya kuratibu barabara hiyo,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Philippe Dongier alisema kiasi hicho cha fedha kimelenga kukamilisha awamu ya pili ya mradi huo.

Dongier ambaye pia ni msimamizi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Uganda na Burundi, alisema mradi huo utagharimu jumla ya Dola za Marekani 290 milioni.

“Dar es Salaam inakuwa kwa kasi, msongamano wa magari ni tatizo kwa ukuaji wa uchumi kwa sababu unapunguza uzalishaji kwa kupoteza muda wa watumiaji wa barabara. Hali hiyo inatishia ukuaji wa baadaye wa mji na nchi kwa jumla na unaongeza uharibifu wa mazingira,” ilisema taarifa ya WB na kuongeza:

“Mfumo wa BRT utasimamiwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi kwa Dola za Marekani 40.9 milioni ukihusisha wasimamizi binafsi wawili wa mabasi na mkusanya nauli mmoja. Mfumo huo mpya utatekelezwa kwa mabasi yapatayo 148 yatakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 140 kila moja kwa safari za haraka na za kawaida.

“Mabasi mengine 100 yenye uwezo wa kubeba abiria 60 kila moja yatatembea katika barabara ndogo. Kutakuwa na kilometa 20.9 zitakazokuwa na njia za waendesha baiskeli na wapita kwa miguu kila upande na vituo vya mabasi kwa kila umbali wa wastani wa mita 500.”

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka alisema hana taarifa za benki hiyo kuidhinisha fedha hizo, lakini akasema atafuatilia ili kujua idadi ya ajira, hasa zitakazowanufaisha wazawa.

“Kwa kweli hizo taarifa ndiyo kwanza nazisikia kwako, labda unipe muda nizifuatilie ili nije na majibu ya uhakika. Lakini kama kawaida, ajira za kampuni kama hizo huwa na wataalamu wa nje na wa ndani, kwa hiyo tutahakikisha kuwa sheria zinalindwa,” alisema Kabaka.

Mtaalamu wa usafiri katika Benki ya Dunia, Yonas Mchomvu alisema: “Tunafurahishwa na kasi ya utekelezwaji wa mradi wa mabasi yaendayo kasi, hasa kwa kuwa makandarasi wote wanaotakiwa wameshapewa fedha na ujenzi unaendelea,” alisema Mchomvu.                                                          Daladala wachekelea
Licha ya taarifa hiyo kueleza kuwa mradi huo utasababisha kuondolewa kwenye mzunguko daladala 1,800, bado wamiliki wa magari hayo wamepokea mradi huo kwa furaha.
Mwenyekiti wa Wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (Darcoboa), Sabri Mabrouk alisema hiyo ni fursa kubwa kwao ambayo hawako tayari kuikosa.

“Siyo kwamba mradi huo utatuathiri na siyo daladala 1,800 tu zitakazoondolewa, ni daladala 3,000. Sisi ndiyo walengwa wa mafanikio hayo kwani hayo mabasi yanayokwenda haraka tutamilikishwa. Hapa ndipo tunahimizana kujiunga ili tujue tutayamiliki vipi,” alisema Mabrouk.

Post a Comment