JENGO JIPYA LA HALMASHAURI YA RUNGWE |
JENGO LA ZAMANI AMBALO BADO LINAENDELEA KUTUMIKA |
WATENDAJI WA HALMASHAURI YA RUNGWE |
KAIMU MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA RUNGWE MR MWANSASU AKIJIBU HOJA MBALIMBALI NA KUWASIRISHA HOJA KWA MADIWANI |
. |
KATI YA MADIWANI WALIOPATA NAFASI YA KUONGEA KWA UCHUNGU JINSI HALMASHAURI YA RUNGWE INAVYOPOTEZA MUELEKEO KWA KUTO KUSANYA MAPATO KATIKA VYANZO MBALIMBALI AMBAPO HADI SASA MAPATO YAMESHUKA KUTOKA MAKISIO YA TSH 2,369,298,000/= NA MAPATO YALIYOKUSANYWA NI SH 346,849,409.23 KWA MUDA WA MWEZI WA JUNI HADI MWEZI AGOST |
DC WA RUNGWE MR CHRISPIN MEELA AKIONGEA NA MADIWANI NA WATAALAM PAMOJA NA WANANCHI WALIOHUDHURIA KIKAO HICHO |
MR MBAI KUSHOTO AMBAYE NI AFISA UTUMISHI WILAYA YA RUNGWE NA MR SHIRIMA DT WA RUNGWE WAKIFUATILIA MIJADARA YA MADIWANI KWA MAKINI |
AFISA MICHEZO ENZ SEME AKIENDELEA NA URATIBU WA KIKAO KUONA MAMBO YA SOUND YANA KAA SAWA |
WATAALAM WA HALMASHAURI YA RUNGWE WAKIENDELEA NA KIKAO |
Bavicha yasisitiza kumtimua Shonza
Juliana Shonza
Na: Kelvin Matandiko
BARAZA
la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), limesisitiza
kuwa Juliana Shonza amevuliwa nafasi aliyokuwa akiishikilia ya umakamu
mwenyekiti wa baraza hilo baada ya kukamilisha taratibu zote za
kumuondoa.
Kauli hiyo imekuja kufuatia Shonza kunukuliwa kwenye vyombo vya habari akisema yeye bado ni...
Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo kwa maelezo kuwa hakuwa amepewa barua yoyote ya kumsimamisha.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa BAVICHA, John Heche alisema Shonza alitumiwa barua ya kumvua nafasi hiyo kwa njia ya posta januari 6, hata hivyo amekuwa akikataa kuipokea.
“Lakini sio hivyo tu siku aliyokuwa anazungumza na vyombo vya habari, tulimtumia barua akakataa kuipokea, taratibu zinatuambia kumpatia barua lakini kama ameikataa bado haiwezi kubadili maamuzi ya chama,”alisema Heche.
Baada ya kumtafuta Shonza ili kutoa ufafanuzi juu ya tarifa za kupokea kwa barua hiyo zilishindikana.
Siku mbili zilizopita Shonza alikunukuliwa kwenye vyombo vya habari akisema kikao cha kamati ya utendaji cha Bavicha kilichokutana na kupitisha umamuzi wa kumfukuza kilikuwa sio halali huku akiwatupia lawama Heche na Mwenyekiti wa Chama hicho Freemon Mbowe kwa madai ya kumdhalilisha.
Shonza alisema yeye bado ni Makamu Mwenyekiti wa Bavicha na mwanachama halali wa chama hicho. Aidha alisema anafanya mkakati wa kuwashtaki wale anaowalalamikia kwa kumuita msaliti ndani ya chama hicho.
Shonza alimtuhumu Heche kutengeneza mipango ya kutukuza ukanda waziwazi ndani ya chama hicho huku akiwataka kutoa ufafanuzi wa kikatiba juu ya shutuma zinazotolewa dhidi yake.
MWANANCHI
Mradi wa gesi Kilwa ‘kuzaa’ hospitali ya kisasa ya kimataifa
WASWAHILI husema, ‘mgeni njooo , mwenyeji apone’.
Usemi huu una maana nyingi, lakini mojawapo ni ile ya kuona kwamba mara nyingi mgeni afikapo, ujio wake huwa zawadi hata kwa wenyeji.
Kwa Watanzania ,wengi wao wanaposafiri kwenda kutembelea jamaa zao ni kawaida yao kubeba zawadi.
Usemi huu una maana nyingi, lakini mojawapo ni ile ya kuona kwamba mara nyingi mgeni afikapo, ujio wake huwa zawadi hata kwa wenyeji.
Kwa Watanzania ,wengi wao wanaposafiri kwenda kutembelea jamaa zao ni kawaida yao kubeba zawadi.
Utaratibu huu unaweza kushabihiana na utakaotokea katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi ambako imegundulika gesi.
Kampuni ya Statoil kutoka Norway ikishirikiana na Exxon Mobil iligundua gesi katika Visiwa vya Zafaran na Lavan vilivyopo Kitalu 2, Ukanda wa Pwani ya Tanzania, hususan Pwani ya Kilwa.
Mradi huo una gharama kubwa pia utafanywa na wageni ambao wana utalaamu wa miaka mingi katika biashara ya gesi duniani.
Kutokana na ujio wa wageni hao, Watanzania hususan wakiwamo wakazi wa Kilwa, Lindi na Mtwara kwa jumla hawana budi kupata faida za moja kwa moja na zingine zisizo za moja kwa moja. Miongoni mwa faida zisizo za moja kwa moja ni gesi hiyo kutumika kutengeneza umeme utakaopatikana kwa uhakika na kuuzwa kwa wananchi wote.
Hata hivyo, ujio wa mradi huo kwa upande mwingine una faida kwao kutokana na kutoa ajira ambayo itazingatia uwezo.
Je wakazi wa Halmashauri ya Kilwa watapata faida gani ya kudumu kutokana na gesi hiyo?
Hili ndilo swali ambalo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Adoh Mapunda anasema walijiuliza baada ya kufika kwa wageni hao.
Mapunda anasema madiwani, watendaji na mkuu wa wilaya walikaa na kutafakari kwa kina juu ya faida ya kudumu itakayoonekana wilayani mwao kutokana na ujio wa mradi wa gesi.
“Sisi tulikataa kauli za kusaidiwa madawati kwenye shule zetu, ama kupewa dawa kwenye hospitali na zahanati zetu
Hii ni kwa sababu tuna uwezo nazo, badala yake tukabuni mradi mkubwa wa kimataifa ambao utakuwa na faida ya kudumu kwa Kilwa na taifa kwa ujumla”, anasema.
Anafafanua kwamba mradi huo ni ujenzi wa hospitali ya kimataifa itakayolingana na ile ya Apollo nchini India ambayo viongozi mbalimbali duniani hukimbilia kwenda kutibiwa.
Hospitali ya aina hiyo itajengwa na mwekezaji na itaendeshwa na taasisi nyingine ya kimataifa huku halmashauri ikiwa na hisa za kupata gawio la kila mwaka kutokana na faida.
‘’Tulizungumza na wawekezaji, Statoil , kwamba watujengee hospitali ya aina hiyo ambayo itakuwa na uwezo wa kutoa tiba kwa viongozi wakiwamo marais wa Afrika na wakuu wa kampuni mbalimbali Afrika zikiwamo kampuni za uwekezaji katika gesi , madini na hata usafirishaji na wafanyabiashara wa nchi mbalimbali,’’ anafafanua.
Mapunda anasema mpango huo unatekelezwa kupitia utaratibu uliopo kwenye mikataba kwa wawekezaji kuhusu uwajibikaji na ushiriki katika masuala ya kijamii, Social Co-operation Responsibility (SCR).
Anasema tayari Statoil imetenga Sh18 bilioni kuanza ujenzi wa hospitali hiyo mjini Kilwa wakati wowote kuanzia mwaka huu. Anafafanua kuwa michoro ya hospitali hiyo ipo tayari na imechorwa kama lilivyokuwa jengo la kifalme yaani Kasri lililojengwa eneo la Kilwa Kisiwani enzi za Sultan wa Kiarabu aliyekuwa akimiliki kisiwa hicho.
‘’Tunatarajia kwamba taasisi ya kimataifa ya Aga Khan Foundation ndiyo itakayoendesha hospitali hii kwa kiwango cha kimataifa . Tulikaa na kuzungumza pande zote tatu, yaani Kilwa, Statoil na Aga Khan Foundation na kukubaliana kuanzisha hospitali hiyo, hivyo tuna imani itaendeshwa kama ile ya Apollo,’’ anasisitiza Mapunda.
Anasema hospitali hiyo itaajiri madaktari mabingwa kutoka ndani na nje ya nchi, itakuwa na wafanyakazi wataalamu , pamoja na wahudumu ambao wengi watatoka Halmashauri ya Kilwa.
Kipanya Leo
Wananchi wenye hasira kali hapa nchini wametakiwa kuacha kujichukulia sheria mikononi na kuwapiga ama kuwachoma moto watu wanaodaiwa kuwa ni wezi bila ya kujua kama madai wanaotuhumiwa nayo ni ya kweli au la na wengine kujikuta wakipoteza maisha bila ya kuwa na hatia na kutakiwa kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria na usalama.
Kauli hiyo imetolewa na
0752-881456
No comments:
Post a Comment