Wednesday, May 22, 2013

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYANI RUNGWE YAANZA LASMI KUKAGUA MIRADI YA WANANCHI INAYOTEKELEWA ILI KUONGEZA UFANISI WA KAZI NA KUDHIBITI UJENZI MBOVU

 
MWENYE TAI NI MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AKIWA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA PAMOJA WA WATENDAJI WA HALMASHAURI YA RUNGWE WAKIKAGUA MRADI WA KIWANDA CHA KUSINDIKA MATUNDA KINACHOJENGWA KIJIJI CHA IPONJOLA

HADI KUISHA KWA UJENZI WA KIWANDA HIKI CHA KUSINDIKA MATUNDA KITAGHARIMU TSH MILION 43.91 NA UJENZI UNATARAJIA KUISHA 28.07.2013DIWANI AKIONGEA NA WANANCHI WA KATA YAKE HUKU AKIMTAMBULISHA MZEE DAIMON MWALINDU KUWA NI MTU WA PEKEE ANANYEPENDA MAENDELEO HASA KWA KUJITOLEA BULE UWANJA WA KUJENGA KIWANDA CHA KUSINDIKA MATUNDA BAADA YA WANANCHI KUUIBUA MRADI HUO KATIKA KATA YAO


MZEE  DAIMON MWALINDU AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MKUU WA WILAYA BAADA YA KUPONGEZWA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA NA KUAHIDI KUUTAMBUA MCHANGO WAKE  KATIKA KULETA MAENDELEO

KAIMU AFISA KILIMO WILAYA YA RUNGWE GODWIN KAKIKO AKIELEZA JINSI KIWANDA CHA KUSINDIKA MATUNDA KITAKAVYO WANUFAISHA WANANCHI HASA WANANCHI WA RUNGWE, SASA KUWA NA UHAKIKA NA SOKO LA MATUNDA HUKU WATU WAKIWA NA UHAKIKA WA AJIRA KIWANDANI HAPO

DAS WA WILAYA YA RUNGWE  MR ALINANUSWE AKIMKALIBISHA MKUU WA WILAYA KUONGEA NA WANANCHI
CHRISPIN MEELA AKIONGEA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA IPONJOLA BAADA YA KUKAGUA MRADI WAO WALIOUIBUA WA KIWANDA CHA KUSINDIKA MATUNDA WANAYOZALISHA  WILAYANI RUNGWE HUKU AKIWATAKA KUUSIMAMIA MRADI HUO KWAKUWA NI PESA NYINGI ZIMEWEKEZWA HAPO NA MRADI UTAKUWA NA FAIDA KWAKO KWA KUONGEZA THAMANI YA MAZAO WANAYOYAZALLISHA WILAYANI RUNGWE

NEEMA MWAIHOJO AKIONGEA KWA NIABA YA WANAWAKE WA KIJIJI CHA IPONJOLA HUKU AKIISHUKURU SERIKALI KWA KUKUBARI KUWALETEA MRADI WAO WA KIWANDA CHA KUSINDIKA MATUNDA HUKU AKIITAKA JAMII KUJIANDAA KUZALISHA NA KUUZA BIDHAA ZAO HAPO NA ZAIDI AMESEMA KIWANDA WATAKILINDA KWAKUWA NI MALI YAO

LOJAS ANYOSISYE AKIONGEA MBELE YA KAMATI YA ULIZI NA USALAM KUWA VIJANA WAMEFURAHI SANA BAADA YA KUONA SERIKALI YAO IMEWAJALI KWA KUWALETEA MRADI HUU WA KIWANDA CHA KUSINDIKA MATUNDA HIVYO WANA UHAKIKA WA KUUZA MATUNDA YAO HAPO NA KUANZISHA BIASHARA MPYA YA KUUZA BIDHAA ZILIZO SINDIKWA  HIVYO KIPATO CHAO KITAONGEZEKA NA KUPUNGUZA UZURULAJI NA MATENDO MAOVU KATIKA JAMII


HAPA NI UJENZI WA KITUO CHA MAFUNZO YA KILIMO WILAYANI RUNGWE

MKUU WA WILAYA CHRISPIN MEELA AKIONGEA NA DIWANI BAADA YA KUKAGUA MRADI WA KITUO CHA KILIMO KILICHOPO KATA YA KYIMO KATIKA KIJIJI CHA IGILIGITO

WANANCHI WA KIJIJI CHA IGILIGITO KATA YA KYIMO WILAYANI RUNGWE KWA NGUVU YA PAMOJA WAMEJENGA BARABARA KWA HISANI YA JACA KWA BAADHI YA VIFAA VYA UJENZI NA MACHINE ZA KUSEMBUA BARABARA ZIKITOLEWA KWA MSAADA WA CHUO CHA MIUNDOMBINU KILICHOPO KK WILAYANI RUNGWE

MUWAKIRISHI WA JACA KONAKO KONDO AKIWA NA WATAALAMA WA WILAYA YA RUNGWE BAADA YA KUJIONEA UJENZI WA BARABARA KIWANGU CHA CHANGALAWE KATIKA KIJIJI CHA IGILIGITO WILAYANI RUNGWE

MKUU WA WILAYA AKIONGEA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA IGILIGITO WILAYANI RUNGWE KWA KUWASHUKURU KUCHUKUA HATUA ZA KUJILETEA MAENDELEO


KWA MIAKA MINGI WANANCHI WA MWAKALELI WAMEKUWA WAKIZALISHA SANA MAZIWA NA KUYAUZA KIHOLELA LAKINI SASA SERIKALI KWA KUPITIA WANANCHI WA MWAKALELI KUUIBUA MRADI WAO WA UJENZI WA KIWANDA CHA KUSINDIKA MAZIWA WANATARAJIA KUINUA KIPATO NA UCHUMI PAMOJA NA KUJIPATIA AJIRA

MKUU WA WILAYA NA KAMATI YAKE YA ULIZI NA USALAMA WAKISIKILIZA MAONI YA WAZEE WA MWAKALELI KUHUSIANA NA UJENZI HUO KWAKUWA KIWANDA HICHO KITAKUWA MKOMBOZI WA MAZIWA YANAYOHARIBIKA

KUSHOTO GIDEON MAPUNDA  KAIMU AFISA KILIMO HALMASHAURI YA BUSOKELO AKITOA MAELEKEZO KWA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE NA KAMATI YAKE  JINSI KIWANDA KITAKAVYOFANYA KAZI YA KUSINDIKA MAZIWA

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA RUNGWE WAKITETA JAMBO BAADA YA KUJIONEA SHUGHURI ZA MAENDELEO YA WANANCHI KATIKA MIRADI WANANYO ITEKELEZA


 LEO TUKUYU MJINI :  UJENZI WA BARABARA YA RAMI KUANZIA TUKUYU MJI,  MBAMBO, LWANGWA , MWAKALELI HADI KATUMBA IMEANZA KUJENGWA

WANANCHI WA TUKUYU MJINI WAKISHUHUDIA GREDA LIKIWA KAZINI KUTANUA BARABARA TAYARI KWA UJENZI

ULINZI NA USALAMA NI MUHIMU SANA

  ..........................................................................................................................

HIVI MOTO UNGELIPUKA HAPA INGEKUWAJE WATANZANIA WATU WA MBEYA HAWAKOMI: SHUHUDIA WANANCHI WA MLIMA NYOKA MBEYA WALIVYO GOMBANIA MAFUTA BAADA YA GARI LA MAFUTA KAMPUNI YA LAKE OIL KUPINDUKA

 WAKAZI WA MLIMA NYOKA MKOANI MBEYA WAKIWA NA PILIKA KUELEKEA KUCHOTA MAFUTA BAADA YA GARI HILO KUPINDUKA.
 SHUHUDIA WAKAZI WA MLIMA NYOKA WAKIWA WANAGOMBANIA MAFUTA
 GARI LA KAMPUNI YA LAKE OIL BAADA YA KUPINDUKA
 KILA MKAZI YUPO BIZE NA MAFUTA
 PICHA NA MBEYA YETU
.....................................................................................................................
 

Washirika sita wa ‘polisi wa bangi’ wakamatwa wakiwa na magunia 30

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Leberatus Sabas akionyesha bangi iliyokamatwa jana 
Na Mussa Juma ,Filbert Rweyemamu  (email the author)

“Siku za karibuni tulipata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba kuna mtandao wa wahalifu wanaoshirikiana na baadhi ya polisi wasiyo waaminifu,” alisema Kamanda Sabas.
Arusha. Polisi mkoani Arusha, imekamata magunia mengine 30 ya dawa za kulevya aina ya bangi kwa watu sita ambao inadaiwa ni washirika wa polisi wawili, waliokamatwa na magunia 18 ya bangi katika maeneo ya Himo mkoani Kilimanjaro.
Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas akizungumza na waandishi wa habari jana, alisema watuhumiwa hao, walikamatwa Mei 19 saa 10 jioni katika Kijiji cha Kisimiri juu, Kata ya Ngaramtoni wilayani Arumeru.


“Wakati askari hao, waliokamatwa mkoani Kilimanjaro, polisi mkoani Arusha pia tulikuwa katika msako wa kuwatafuta watuhumiwa wengine wanaoshirikiana na polisi hao, katika biashara ya kusafirisha bangi kutoka Arumeru kupeleka nchini Kenya,” alisema Sabas.
“Siku za karibuni tulipata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba kuna mtandao wa wahalifu wanaoshirikiana na baadhi ya polisi wasiyo waaminifu,” alisema Kamanda Sabas.
“Watuhumiwa hawa walifanikiwa kukimbia kabla ya kukamatwa na kutelekeza bangi hiyo kwenye nyumba zao”alisema Sabas.
Kamanda Sabas alisema uchunguzi wa tukio hilo, ukikamilika watuhumiwa hao, watafikishwa mahakamani.
Habari zilizopatikana baadaye jana kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz kuwa askari wawili waliokamatwa juzi na magunia 18 ya bangi, watashtakiwa katika mahakama za kiraia kama wakosefu wengine.
Wakati huo huo, Kamanda Sabas jana alikiri kuwapo taarifa ya kuuawa Watanzania watatu nchini Kenya kwa tuhuma za ujambazi na kupatikana na bunduki ya polisi aina ya Sub Mashine Gun (SMG).
Watanzania hao,Tigiki Pasto,Steven Webo na mmoja ametambulika kwa jina moja la Kadogoo, waliuawa Mei2, mwaka huu baada ya kuvamia wafanyabiasha na kuwapora na kuwaua wawili.
Hata hivyo, baadaye walizingirwa na wananchi hao na kuuawa na ndipo waliipata bunduki hiyo mali ya polisi.
“Ni kweli tukio hilo lipo, ila sasa kwa kuwa linahusisha nchi mbili, linashughulikiwa kwa taratibu nyingine za nchi na nchi”alisema Kamanda Sabas.
Hata hivyo, alikiri pia kushikiliwa kwa polisi wawili kwa uchunguzi kutokana na kupotea kwa silaha hiyo, kwenye ghala la polisi Wilaya ya Ngorongoro.
...........................................................................................................................

MTOTO MWENYE UMRI ZAIDI YA MIAKA MIWILI AFUNGIWA NDANI ZAIDI YA MIAKA MIWILI NA WAZAZI WAKE IYUNGA JIJINI MBEYA

Mtoto Joshua akiwa amekaa uwani kwenye nyumba  yao huku wazazi wake wakiwa wamemwacha peke yake toka asubuhi bila ya kumpatia chakula mtoto huyo tumemkuta katika hali mbaya sana kwani tunemkuta amejisaidia haja ndogo na hana hata nguo za kubadilisha

Kwa ujumla mtoto Joshua hata kutembea hawezi kwani simama yake ni ya kutetemeka migu tu 

Hizi ni nguo za joshua na kaka yake nguo hizi hazifuliwi bali zikirowa na mkojo huwanikwa tu juani na kisha kuvaliwa tena

Mtoto Joshua akiwa ana tushangaa maana anaona amevamiwa kwakweli inasikitisha sana

Hapa ndiyo mtoto joshua huwa anacheza wakati wa mchana

Mlango ulio wazi ndimo mtoto Joshua hufungiwa humo

Hiki ndicho chumba mtoto Joshua hufungiwa kama picha unavyoiona kona hiyo ndiyo mtoto huyo hujibanza

Kushoto ni kaka wa Joshua yeye amesema huwa anashinda nyumba za jirani kucheza wakati mdogo wake amefungiwa ndani

Mama wa mlezi wa Joshua akiingia numbani kwake na kutushangaa tumekuja fuatanini kwake

Angalia picha hii kwa makini jinsi mtoto Joshua anavyomwangalia mama yake mlezi yaani mama wa kambo

Sekera Watsoni (40) amembeba mtoto Joshua kuonyesha anampenda na kuwa anamhudumia vizuri mtoto huyo

Huyu mama pamoja na mumewe ndiyo wanaomtesa mtoto Joshua

Hawa kaka zake Joshua wakituonyesha sehemu wanayolala pamoja na joshua wakati mama huyo yeye amesema  yeye huwa analala na joshua chumbani kwake 

Baadhi ya majirani wakisimulia mkasa huo

Amini usiamini mtoto Joshua baada ya kuona mkeka mzuri alijilaza kwa furaha kwani amezoea kulala sakafuni

Mama mlezi wa Joshua akijiandaa kumpeleka joshua kituo cha afya akapate matibabu baada ya kuamriwa kufanya hivyo

SAFARI YA KWENDA HOSP IKAANZA

Habiba Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la aibu kubwa hivyo halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo


Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto mwenye umri wa zaidi ya miaka miwili amefungiwa ndani na wazazi wake kwa kipindi cha miaka miwili sasa bila kutoka nje pamoja na kukosa matunzo muhimu hali ambayo imepelekea mtoto huyo kudhoofu kiafya.
Tukio hilo limetokea leo jijini mbeya katika  mtaa wa Ikuti kata ya Iyunga ambapo majirani wa karibu na mtoto huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa mtaa huo kufika nyumbani anapoishi mtoto huyo kwa lengo la kufahamu maendeleo yake .
Mtoto huyo amefahamika kwa jina la Joshua Joseph umri unao kadiriwa  kuwa ni kati ya miaka miwili au mitatu  ambaye alikutwa nyumbani hapo akiwa pekee yake huku wazazi wake wakiwa wameondoka kuelekea kwenye shughuli zao .
Akizungumzia tukio hilo Kaimu barozi wa mtaa huo wa Ikuti Ndugu Aloni Mboya amesema kuwa hali hiyo imenza kujitokeza kwa kipindi cha miaka mitatu sasa hali ambayo imepelekea mtoto huyo kukumbwa na maradhi ya utapiamlo.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2011 mwezi wa tatu alipokea  taarifa kuhusiana na   suala hilo  ambapo baba wa mtoto huyo ndugu Joseph Simoni aliitwa katika ofisi za mtaa kwa lengo la kumhoji juu ya malezi ya mtoto huyo.
 Aidha baada ya kuhojiwa alikiri kosa ambapo alipewa onyo na viongozi wa mtaa ambao walimtaka kuhakikisha anamtunza vema mtoto huyo kwa kumpatia chakula bora  pamoja na huduma nyingine.
Mara baada ya mtu huyo kupewa kalipio na viongozi wa mtaa hali hiyo iliendelea tena ambapo wao kama viongozi wa shina pamoja na wananchi walimuita yeye pamoja na mke wake aitwaye  Sekera Watsoni (40) kuhama mtaani hapo kwa kwa kipindi cha miezi sita ambapo walikaidi agizo hilo.
 Amesema mara baada ya watu hao kugoma waliamua kuwaacha na kuwaondoa katika umoja wa ubarozi wao na kuto watambua tena kama wananchi wa eneo hilo kutokana na vitendo vyao vya kikatili dhidi ya mtoto huyo.
Kwa upande wao Maafisa maaendeleo ya jamii kata ya Igawilo na Iyunga ambao ndio waliofika katika eneo hilo wamesema kuwa matukio kama hayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara ndani ya jamii hasa kwa vitendo vya kunyanyaswa kwa watoto wanawake.
Mmoja wa Maafisa hao Ndugu Habiba Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la aibu kubwa hivyo halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo
 
Amesema hali ya kiafya ya mtoto si ya kulizisha kutokana na kusumbuliwanna maradhi mbalimbali yanayotokana na kukosekana kwa lishe bora pamoja na huduma nyingine.
Amesema anawashukuru majirani pamoja na viongozi wengine wa serikali ya mtaa ambao wamekuwa karibu na mtoto huyo kwa kipindi chote cha miaka miwili licha ya kutokuwepo kwa ushirikiano toka kwa  wazazi wa mtoto ambaye kwa sasa amefikishwa katika kituo cha afya  Inyala Kata ya Iyunga  jijini hapa.
Awali inaelezwa kuwa baba na mama wa mtoto huyo  wamekwisha tengana kwa kipindi kirefu sasa kutokana na kutokuwepo kwa maelewano ndani ya nyumba hiyo hali ambayo ilimfanya baba huyo kuoa mwanamke mwingine ambaye ndiye anaye ishi na mtoto kwa sasa kama mama wa kambo.
Amesema kutoka na kuwepo kwa mgawanyiko huo ndani ya familia baba pamoja na mama huyo ambaye ni mke wa pili walichukua jukumu la kuishi na watoto wote walio achwa na mwanamke wa kwanza ambapo kwa asilimia kubwa ndiko kuliko sabababisha kuwepo kwa hali hiyo ya manyanyaso ya mtoto.
Hata wakati wa tukio hilo la kumtoa mtoto huyo ndani baba mzazi wa mtoto hakuwepo katika maeneo hayo ya nyumbani ambapo maafisa ustawi wa jamii pamoja na majirani waliamua kuchukua jukumu la kumpeleka mtoto huyo katika kituo cha afya Inyala kilichopo Kata ya Iyunga kwa lengo la kumfanyia uchunguzi na kutambua nini kinacho msumbua mtoto huyo

Picha na Mbeya yetu 
..................................................................................................
 
TANGAZO KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
A
WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII DKT. HUSSEIN MWINYI
TANGAZO KWA UMMA

 Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia Tangazo lake kwenye Gazeti la Habari Leo la tarehe 20 Aprili, 2013 siku ya Jumamosi na la tarehe 23 Aprili, 2013 siku ya Jumanne na kwenye tovuti ya Wizara, ilitangaza nafasi mbalimbali  za kazi za Kada ya Afya zikiwemo za Maafisa Ustawi wa Jamii, Maafisa Ustawi wa Jamii Wasaidizi, Walezi wa Watoto, Maafisa Lishe na Maafisa Lishe Wasaidizi.
 Wizara inapenda kuwajulisha waombaji wa nafasi za Kada tajwa hapo juu zitashughulikiwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira.
 Hivyo, waombaji wote waliotuma maombi yao Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wanajulishwa kuwa maombi yao yatapelekwa Sekretarieti ya Ajira kwa ajili ya uchambuzi na usaili.
 Tangazo hili halihusu waombaji walioomba Kada mbalimbali za Afya ambazo zitashughulikiwa moja kwa moja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
 Kaimu Katibu Mkuu
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
22 Mei, 2013
..........................................................................................................................................

CARTHBERT KAJUNA ANASEMA:FANI YA UANDISHI WA HABARI IMEVAMIWA, TUSIPOZIBA UFA TUTAJENGA UKUTA.


Wanahabari wakichukua baadhi ya matukio.

Watu wengi kwa sasa wameibuka na kutokea kuipenda fani ya uandishi wa habari bila kujua misingi na miiko ya uandishi wa habari. Tatizo moja ambalo limeonekana ni kubwa sana ni utandawazi ambao umekuwepo na kutokea ibuko la kila kijana kufungua gazeti tando (blog).
Hatukatai kuja kwa magazeti tando ila naomba tujiulize, yanatumika ipasavyo ama ndiyo limekuwa ni wimbi vamizi lenye kutoa ama kusambaza habari hata zile zisizokuwa na vyanzo kamili na visivyojitosheleza.Kwa sasa imezuka tabia ya wanaojiita wamiliki wa magazeti tando,wengi wao kukopi na kupaste vitu wanavyoviokota katika mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter, facebook na mingine mingi.
Sina nia ya kumsema mtu bali napenda tuelimishane kama vijana wenzangu,ambao wametokea kuipenda fani ya uandishi wa habari, wakumbuke kuwa fani ya uandishi wa habari ina miiko na maadili yake, mfano. Katika kuandika habari za mazingira, siasa, elimu, uchumi, michezo, burudani ukiangalia habari hizi zote zina misingi na miiko yake. Leo hauwezi kumchukua mwandishi wa habari za michezo ukamwambia aandike habari za uchumi kwa vile hatakuwa na takwimu za uchumi na hata akiandika hiyo habari na ukiisoma utakuwa unajiuliza maswali mengi bila kupata majibu.
Vile vile ni vizuri vijana wenzangu kutambua kuwa kila kazi ina mipaka na misingi yake, juzi juzi nilisoma habari katika gazeti tando moja wapo ikisema, ‘ALIYEONGOZA MAANDAMANO YA IRINGA MHESHIMIWA MCHUNGAJI MSIGWA ASWEKWA NDANI’ nilijiuliza maswali mengi ambayo kiukweli nilikosa majibu yake, kuona huyu aliyeandika hiki kichwa cha habari kweli amepitia fani ya uandishi wa habari ama ndio ule upepo vamizi?
Maana unapoandika habari za mahakamani, polisi kuna misemo yake, hauwezi kumuhukumu mtu moja kwa moja kwa kusema fulani ni mwizi, hata hao polisi ambao huwa wanakwenda kukamata watu eneo la tukio hawawezi kusema fulani ni mwizi mpaka apelekwe mahakamani ndipo sheria ichukue mkondo wake na kumbaini huyo aliyekamatwa ni mwizi.
Naomba tufike mahali tuheshimu utu wa watu na kuepuka udhalilishaji wa bila kujua naamini baadhi ya vijana wengi walioamua kufungua magazeti hayo tando ambayo yanatoa habari, hawana taaluma ya uandishi wa habari.
Napenda kuwapongeza wale walioamua kufungua magazeti tando katika milengo yao tofauti ikiwemo kutoa habari kwa njia ya ‘kufundisha masuala ya urembo, mapishi, kuwasaidia kuwatangaza vijana katika muziki na hata wale walioamua kuandika habari zao binafsi.
Nayasema yote hayo kwa vile kumezuka wimbi la vijana wanaotaka kuichafua fani ya uandishi wa habari na ionekane si fani ya watu walioenda shule bali ni ya wahuni tu wasiojua mambo, naomba vijana tuelimike na tujifunze kwa watu wanayoyajua mambo ili tuweze kufika mbele zaidi.
Namalizia kwa kusema tusipoziba ufa tutajenga ukuta.
Asanteni sana kwa kusoma.
Imeandikwa na Cathbert A. Kajuna
Post a Comment