BIASHARA IMEANZA KUCHANGANYA HUKU WAFANYA BIASHARA WANAOZUNGUKA NA MATUNDA NA MATUNDA VICHWANI WAKIFURAHIA UTARATIBU WA KUKAA PAMOJA |
KUELEKEA USHIRIKA , KATUMBA NA KIWIRA |
USAFIRI WA KUELEKEA MASUKURU |
MOJAWAPO WA USAFIRI WA KWENDA LWANGWA UKIONDOKA KWENDA SAFARI YA KWENDA LWANGWA |
HII NDIO STANDI YA MABASI TU KWA SASA MABASI YATOKAYO MBEYA, KYELA NA DSM PIA ZITARUHUSIWA TAX TU KUINGIA HAPA |
WENGINE WAKIENDELEA NA KUJENGA MEZA KWA AJILI YA BIASHARA |
WENGINE WAKIENDELEA NA KAZI ZA KUTENGENEZA MEZA ZAO |
KULIA NI MKUU WA WILAYA CHRISPIN MEELA AKIONGEA NA KINGO KUHUSIANA NA MIKAKATI YA SERIKALI YA KUWAJALI WAFANYA BIASHARA WADOGOWADOGO WILAYANI RUNGWE HASA KWA KUWATENGEA ENEO LAO LA KUDUMU ILI KUFANYA BIASHARA KWA UHURU PIA KUTAMBULIWA NA TAASISI ZA KIFEDHA KULIKO HIVI SASA WAMAMCHINGA KUZURULA NA BIDHAA NDOGO AMBAZO MWISHO WA SIKU MAENDELEO HUWA DUNI |
..................................................................................................................
MTWARA
PICHA NA FARID HEMED.
..............................................................................
Bajeti Miundombinu: Fedha za wafadhili kumaliza miradi ya Barabara?
Na Victor Karega, Mwananchi
(
- Katika mwaka wa fedha 2012/13, Tanzania ilipanga kupokea Sh397.051 bilioni kwa ajili ya miundombinu. Lakini hadi Machi 2013, Sh16.361 bilioni tu sawa na asilimia 4.1 zikiwa ni ahadi, zimetolewa.
Dar es Salaam. Zikiwa zimepita
siku kumi tangu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lipitishe
bajeti ya Wizara ya Ujenzi ya Sh1.3 trilioni katika mwaka wa fedha
2013/14, bado mpaka sasa kuna kigugumizi katika kuweka bayana ni kiasi
gani cha fedha hizo kimetengwa kwa ajili ya kulipa mikopo ya zamani.
Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli anasema kati ya
fedha hizo Sh845.226 bilioni sawa na asilimia 21.8, zimetengwa kwa
ajili ya kuboresha miundombinu. Sh397 bilioni ni fedha kutoka kwa
wafadhili.
Pamoja na hayo yote, Kamati ya Bunge ya
Miundombinu inasema ni lazima serikali ielezee ni kiasi gani cha fedha
kitakwenda kwenye shughuli za maendeleo. Pia kubainisha serikali
imetenga shilingi ngapi kwa ajili ya kulipa madeni.
“Kamati imetaarifiwa kwamba mpaka Machi 2013,
wananchi na wakandarasi wanaidai Wizara Sh348.666 bilioni, kwa hiyo
kamati inataka kupata uhakika kama fedha ambazo inataka ziidhinishwe,
kweli zitatumika kufadhili miradi iliyolengwa au sehemu yake italipa
mikopo ya zamani,” anahoji Mwenyekiti wa kamati, Profesa Juma Kapuya.
Fedha za wafadhili hazitabiriki
Anashauri kwamba serikali sasa inapaswa kugharimia
maendeleo ya miundombinu nchini kwa kutumia vyanzo vya ndani vya mapato
kwa kuwa fedha za wafadhili zimekuwa hazitabiriki.
Katika mwaka wa fedha 2012/13, Tanzania ilipanga
kupokea Sh397.051 bilioni kwa ajili ya miundombinu. Lakini hadi Machi
2013, Sh16.361 bilioni tu sawa na asilimia 4.1 zikiwa ni ahadi,
zimetolewa.
Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally anasema
hawezi kuunga mkono bajeti ya Wizara wa Ujenzi kwa sababu ahadi ya Rais
Jakaya Kikwete ya kujenga barabara mpya haijatimizwa mpaka sasa. Ahadi
hiyo aliitoa rais katika uchaguzi wa mwaka 2010.
Anafafanua kuwa kinyume na ahadi ya Rais, barabara
ya Sumbawanga- Kanazi-Kibaoni, imejengwa kwa kiwango duni cha asilimia
24 baada ya mwaka jana barabara hizo kutengewa Sh27 bilioni tu.
Lakini kama hiyo haitoshi Keissy anafafanua kwamba makandarasi wa Kichina wanaojenga barabara hiyo wanaonekana wamechoka kifedha na sasa wanauza mchanga, kokoto, na mawe.
Akichangia hutuba ya makadirio ya mapato na
matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Profesa David Mwakyusa (Rungwe Magharibi)
anasema kwa masikitiko kwamba Wilaya ya Rungwe imegawanywa katika wilaya
tatu, lakini kwa bahati mbaya, hakuna barabara ya kuunganisha wilaya
hizo.
...................................................................................................................................................................
...................................................................................................................................................................
No comments:
Post a Comment