|
MKUU WA WILAYA CHRISPIN MEELA WALIOKAA WANNE KUTOKA KULIA AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA |
|
MKUU
WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AKIONGEA NA WAANDISHI WA
MKOA WA MBEYA HASA MAMBO YAHUSUYO KULIJENGA TAIFA MOJA LA TANZANIA KUWA
NA AMANI NA MSHIKAMANO NA KUPINGA MATUKIO YA KIFISADI KWA KUWA MWANDISHI
WA HABARI NI KIOO KATIKA JAMII NA MTU ANAYEAMINIWA SANA NA WATU HIVYO
HAIPASWI KUWA CHANZO CHA UCHAFU KATIKA UTENDAJI WA KAZI NA UCHOCHEZI NA VURUGU ZINAZO SABABISHA KUTOWEKA KWA AMANI
TANZANIA |
|
KULIA MWAKILILI NA MWAKIPESILE WAKIWA MAKINI KUMSIKILIZA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE |
|
JOSEPH MWAISANGO MMILIKI WA MBEYA YETU NA WAJUMBE WENGINE WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA |
|
FRED & HYNES |
|
KWENYE KUNDI LOLOTE LAZIMA PAWE NA WASHAURI HAPO NI BENJAMINI MWAKILILI AKISISITIZA JAMBO LA KUFUFUA MSHIKAMANO KATI YA WAANDISHI NA WANANDISHI WA NCHI JIRANI KAMA ILIVYOKUWA KIPINDI CHA NYUMA |
|
HAPA ULIKUWA NI WAKATI MZURI NA WA FURAHA BAADA YA CHARLES MWAKIPESILE KUWA NDIO MUASISI WA KUJITOLEA MCHANGO WA TSH LAKI MOJA NA KUOMBA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPN MEELA KUMUUNGA MKONO KWA LAKI NNE ILI KUWA NDIO MWANZO WA KUANZISWA KWA SACCOS YA MBEYA PRESS CLUB HIVYO CHACHU HII IKAZAA MATUNDA ZAIDI YA MILIONI MBILI ZIKAPATIKANA KWA AJILI YA KUAZISHA SACCOS YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA |
|
HAPA NI UMAKINI TU WAKUMSIKILIZA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI |
|
MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AKIONDOKA UKUMBINI HAPO AKISINDIKIZWA NA BAADHI YA WAANDISHI BAADA YA KUONGEA NA WAANDISHI WA MKOA WA MBEYA HASA MAMBO YAHUSUYO KULIJENGA TAIFA MOJA LA TANZANIA KUWA NA AMANI NA MSHIKAMANO NA KUPINGA MATUKIO YA KIFISADI KWA KUWA MWANDISHI WA HABARI NI KIOO KATIKA JAMII NA MTU ANAYEAMINIWA SANA NA WATU HIVYO HAIPASWI KUWA CHANZO CHA UCHAFU NA UCHOCHEZI WA KUTOWEKA KWA AMANI TANZANIA |
|
KAMATI YA MUDA IKAKABIDHI TAARIFA KWA WAJUMBE NA KURUHUSU UCHAGUZI KUFANYIKA KAMA ILIVYOANDALIWA |
|
UKAFIKA WAKATI ULIOSUBIRIWA NA WANACHAMA SIKU YA UCHAGUZI NA HAPO NI KAMATI YA UCHAGUZI ILIYOONGOZWA NA BENJAMINI MWAKILILI KATIKATI NA KUSHOTO MAKAM MWENYEKITI CHARLES MWAKIPESILE PIA KULIA NI KATIBU MR MOSSES |
|
WAGOMBEA NAFASI YA UENYEKITI WAKAPATA NAFASI YA KUOMBA KURA KWA WAJUMBE WA UCHAGUZI |
|
WWAGOMBEA WENGINE WAKATUMIA SIFA ZA KUWA NA PASPOTI KUWASHAWISHI WAPIGA KURA ILI WAWAPE KURA ZA NDIO |
|
UKAFIKA WAKATI WA KUAMUA NANI AWE KIONGOZI KWA KUPIGA KURA KWA WAJUMBE WA MBEYA PRESS CLUB |
|
KWA KUTUMIA KARATASI MAALUM KURA ZILIPIGWA KWA UMAKINI HAKUNA KUCHAKACHUANA HAPO |
|
KWA MKOTO PIA KURA ZILIPIGWA |
|
KURA ZIKAHESABIWA KWA UMAKINI WA KUTOSHA |
|
MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI BENJAMINI MWAKILILI AKITANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI KUWA MWENYEKITI NI USWEGE LUHANGA, MAKAMU MWENYEKITI NI MODESTUS MUKULU NA KATIBU NI EMANUEL LENGWA, MTUNZA HAZINA BRANDINA NELSON, KAMATI YA MAFUNZO FESTO SIKAGONAMO, |
|
UONGOZI MPYA UKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA HUKU VYOMBO VYA HABARI VIKIENDELEA NA KAZI YA KUCHUKUA TUKIO LA KIHISTORIA MKOANI MBEYA BAADA YA KUFUKUZWA UANACHAMA KWA ALIYEKUWA MWENYEKITI CHRISTOPH NYANYEMBE NA MTUNZA HAZINA UPENDO BAADA YA KUKUTWA NA TUHUMA YA KUCHAKACHUA PESA ZA CLUB |
|
UONGOZI MPYA UKISHUKURU WAJUMBE KWA KUWAPA NAFASI YA KUONGOZA MBEYA PRESS CLUB |
|
BAADA YA UCHAGUZI AMANI IMEPATIKANA NA MAKUBARIANO NI KUFANYA KAZI KWA BIDII NA UADIRIFU ILI MBEYA NA TAIFA ZIMA ILIFAIDIKE NA TAARUMA HII YA HABARI |
|
ALIYE SIMAMA NI CHRISTOPHA NYANYEMBE HAPO SIKU ALIPOKUWA KASHURUTISHWA KUJIUZULU UONGOZI BAADA YA KUTUHUMIWA KUHUJUMU MAPATO YA CLUB YA WAANDISHI WA HABARI MBEYA |
|
KUSHOTO NI PENDO FUNDISHA ALIYEKUWA MTUNZA HAZINA WA MBPC |
|
MWENYE TISHET YA PUNDAMILIA NI MR NYANYEMBE AKISHUHUDIA KURA ZA KUMUONDOA MADARAKANI BAADA YA KUTUHUMIWA KUFUJA PESA ZA WANACHAMA WA MBEYA PRESS CLUB |
|
BAADA YA KAMATI YA MUDA KUPITIA TUHUMA MR NYANYEMBE NA PENDO FUNDISHA KUKUTWA NA HATIA ZA KUFUJA MALI ZA CLUB AZIMIO LA PAMOJA KWA WANACHAMA LIKATOKA NI KUFUTWA UANACHAMA WA MBEYA PRESS CLUB HIVYO WATU HAWA WAWILI SIO WANACHAMA WA MBPC ILA WATABAKI KUWA WAANDISHI NA WAWAKILISHI KATIKA VYOMBO VYAO
MKUU wa wilaya ya Rungwe Bw.
Chripin Meela amesema, changamoto zinazokabili sekta ya habari na vyombo
vya habari kwa ujumla ni matokeo ya umuhimu wa taaluma hiyo katika ukuaji
wa demokrasia nchini
Akizungumza kwenye mkutano wa
uchaguzi wa klabu ya wandishi wa habari mkoa Mbeya Mkuu wa wilaya ya
Rungwe Chrispin Meela amesema, wananchi wana matumaini makubwa na vyombo vya
habari na pale kipapota doa la utendaji ni muhimu kujirekebisha kabla ya
kutengeza picha mbaya mbele ya jamii wanayoihudumia
Amesema hali iliyojitokeza hivi
karibuni kwenye klabu hiyo inahitaji kuweka misingi imara ya kiutendaji
na kwamba jitihada za kufanya uchaguzi wakati huu ni hatua muhimu za
kuimarisha mfumo wa kujiwajibisha kama taasisi ya taaluma.
Amesema ikiwa viongozi wa dini na
vyombo vya habari vitajihusisha na ubadhirifu na wizi ni dalili kuwa hakutakuwa
na mwingine wa kukemea jamii itakayokuwa huru na yenye kukemea vita dhidi ya
rushwa
Bwana Meela amesema inashangaza
kuona hata vyombo vya habari vinaingia kwenye ufisadi na akaohoji ninani
atakayehoji ufisadi serikali na kwingineko kama nanyi mnaingia kwenye mitego
hiyo hiyo?
Katika hatua nyingine amependekeza
Vyombo vya habari kujenga utamaduni wa kujihusisha na ufuatiliaji wa
maendeleo vijijini na kwa kufanya hivyo kutawezesha wananchi kuwasilisha
changamoto zinazowakabili kwa watunga sera.
Amesema katika kufikia hilo
ni vyema pia Viongozi wa serikali ngazi za chini kuondoa uoga katika
kufanya kazi na vyombo vya habrari na kwa kufanya hivyo kutasadia kusukuma
mbele jitihada za maendeleo
Katika hatua nyingine Bwana Meela
amechangia kiasi cha shilingi 400,000 kwaajili ya uanzishaji wa chama cha
kuweka na kukopa cha wanahabari SACCOS ili kuwezesha kuwapa fulsa
wana habari kujisimamia kiuchumi na kupunguza changamoto za
kimaisha zinazowakabili
Katika kufanikisha hilo wanachama
wa Mbeya Press club walijitokeza kuchangishana wenyewe ambapo wamefanikiwa
kukusanya mtaji wa papo kwa papo kiasi cha shilingi 1,400,000/=
Aidha ameshauri klabu ya wandishi
wa habari kuwa na ofisi yake na hvyo kwa kuomba kiwanja kwenye mamlaka za
majiji itasaidia kuwapa nguvu katika kusimamia haki zao wakiwa na uhuru wa
kuwekeza kwenye majengo yao.
|
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE WAISHI KWA AMANI NA UPENDO PASIPO UFISADI
.................................................................................................................................................................
|
Mwandishi wetu Joseph Mwaisango aliyembeba mtoto Joshua akiwa na ofisa maendeleo na ustawi wa jamii Habiba Iblahimu |
|
Mwandishi
wetu Joseph Mwaisango akikabidhi msaada ya Magodoro, nguo na lishe kwa
niaba ya familia ya Mama Masawe wa DSM ambayo iliguswa sana na hali
aliyokuwanayo mtoto Joshua |
|
Hakika
mtoto Joshua sasa angalau siku mbili hizi hata kusimama na kutembea
ameanza tunawashukuru wote mnaomsimamia mtoto huyu hapo ikuti Iyunga |
|
Mtoto Joshua akiangalia zawadi alizopatiwa |
|
Mama mlezi wa Joshua akiwa haamini kabisa kwa msaada waliopatiwa kwa ajili ya Joshua |
|
Yaani
majirani wakibaki kuduwaa na kusema mungu awabariki kazi za mikono yao
wote waliomchangia mtoto huyu na wasiishie hapo wawajali na watoto
wengine Tanzania |
|
Balozi
wa Mtaa wa Ikuti Aron Mboya, aliwashukuru wasamaria hao na kwamba
serikali ya kijiji itasimimia na kuhakikisha mtoto huyo anapata huduma
zote za kiafya pamoja na kumsimamia mama mlezi kutumia misaada hiyo kwa
malengo yaliyokusudiwa kwa mtoto huyo. |
|
Daktari
wa kituo cha Afya, Inyala kilichopo Kata ya Iyunga, Queen Mwakijambile,
amesema baada ya vipimo kufanyika mtoto huyo amekutwa na tatizo la
utapiamlo huku uzito wa mwili ukiwa haulingani na umri wake. |
|
Mama mlezi wa Joshua akiwa kituo cha afya |
|
Mtoto Joshua siku ya kwanza tulipomkuta alikuwa hivi
HATIMAYE
wasamaria wameanza kujitokeza katika kumsaidia mtoto Joshua Joseph ambaye
alifungiwa ndani zaidi ya miaka miwili huku akikosa matunzo muhimu na kupelekea
mtoto kupata ugonjwa wa utapia mlo.
Moja ya Wasamaria hao Familia ya mama Masawe toka DSM wametoa magodoro mawili, nguo,mashuka,chakula
pamoja na lishe ya mtoto.
Akipokea
msaada huo jana, ofisa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamiii, Habiba Ibrahimu
alisema wasamaria hao wameonyesha uzalendo na kuokoa maisha ya mtoto
ambayo kwa asilimia kubwa yalikuwa hatarini.
Aidha,
Daktari wa kituo cha Afya, Inyala kilichopo Kata ya Iyunga, Queen Mwakijambile,
alisema baada ya vipimo kufanyika mtoto huyo amekutwa na tatizo la utapiamlo
huku uzito wa mwili ukiwa haulingani na umri wake.
“Baada
ya mtoto Joshua kufikishwa kwenye kituo hiki cha matibabu na kufanyiwa vipimo,
tumebaini mtoto alikosa lishe pamoja na uzito wake kufikia kilo nane
ukilinganisha na umri wake wa miaka miwili,”alisema
Alisema,
uzito wa kilo nane ulipaswa kuwa na mtoto wa miezi sita au saba hivyo hatua
aliyofikia alikuwa kwenye hatari ya kupoteza uhai wake.
Naye
Balozi wa Mtaa wa Ikuti Aron Mboya, aliwashukuru wasamaria hao na kwamba
serikali ya kijiji itasimimia na kuhakikisha mtoto huyo anapata huduma zote za
kiafya pamoja na kumsimamia mama mlezi kutumia misaada hiyo kwa malengo
yaliyokusudiwa kwa mtoto huyo.
Picha na Mbeya yetu
...................................................................................................
Muono
wa jicho la samaki katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya AU katika
makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013
Viongoi AU wakiwakumbuka waliotangulia mbele ya haki.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya AU katika makao
makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya AU katika makao
makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013
PICHA NA IKULU
.........................................................................................................................
|
No comments:
Post a Comment