HAPO KUANZIA KULIA NI MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA, ALLY KINGO, MZEE MWAKAPALA KATIBU TARAFA NA ALIYE VAA SHAT JEUSI NI MR MASANJA AMBAYE NI AFISA UTUMISHI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO |
WILAYA YA RUNGWE WAPATA GARI MPYA KWA AJILI YA OFISI YA DC ILI KUWAHUDUMIA WANANCHI KWA HARAKA NA UFANISI |
WANANDOA ENG, UWEZO MWALWEGA NA DR MAGRETH SHIRIMA WAPOKELEWA KWA SHANGWE MBEYA NA KUFANYA IBADA YA SHUKRANI KKKT USHARIKA WA RUANDA MBEYA
MUNGU NA AWABARIKI SANA KATIKA SAFARI YA NDOA YENU MAANA NDOA NI PARADISO NA TAMBALALE |
MCH MWASANGUTI WA USHARIKA WA RUANDA MBEYA AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WANANDOA BAADA YA IBADA YA SHUKRANI YA PEKEE |
DADA NA SHEMEJI SALASALA WAKIWA NA MAMA WENYE NYUSO ZA FURAHA |
PICHA YA PAMOJA BAADHI YA WANAFAMILIA YA MCH MWALWEGA |
HONGERA SANA MR & MRS UWEZO MWALWEGA |
..............................................................................................................................
MAKAMANDA wa polisi wa Mikoa ya Kikanda, wamekutana Jijini Mbeya, kujadili hali ya uhalifu ikiwa na kuweka mikakati itakayosaidia kuwabana askari watakaobainika kukiuka sheria na taratibu za kazi.
Baadhi ya maafisa wa jeshi hila la Polisi wakiwa makini kusikiliza mwenyekiti wao katika kikao hicho |
Baadhi ya makamanda wa polisi wakiwa maetulia kwa umakini kumsikiliza mwenyekiti wa kikao hicho |
Picha ya pamoja |
MAKAMANDA wa polisi wa Mikoa ya Kikanda,
wamekutana leo Jijini Mbeya, kujadili hali ya uhalifu ikiwa na kuweka
mikakati itakayosaidia kuwabana askari watakaobainika kukiuka sheria na
taratibu za kazi.
Mkutano huo unafanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, lengo kuu likiwa ni kujadili hali ya
usalama na uhalifu wa maeneo katika Mikoa ya Morogoro, Iringa, Ruvuma,
Njombe na Mbeya .
Akizungumzia mikakati hiyo, Mwenyekiti wa
Mkutano Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ndugu Faustine Shilogile
alisema katika kikao hicho agenda kuu itakuwa ni kujadili matukio ya uhalifu wa
unyang’anyi wa kutumia silaha, matukio ya ajali pamoja na kujadili nidhamu kwa
watendaji wa jeshi hilo.
Amesema Wahalifu wamekuwa na tabia ya kuhama
hama mara wanapofanya tukio, hawakai sehemu moja hivyo mkutano huu utasaidia
kwa wajumbe kubadilishana na kupeana uzoefu wa kazi,’alisema
Aidha, amefafanua kuwa jeshi la polisi
hivi sasa kupitia baadhi ya askari limekuwa likikumbwa na matukio
ya ukiukwaji wa maadili kwa kukutwa na tuhuma mbalimbali za uhalifu.
Kwa upande wake, Kamanda wa polisi wa mkoa wa
mbeya, Ndugu Diwani Athumani ambaye ni mwenyeji wa Mkutano huo , alisema kikao
hicho kinatarajia kutoka na mikakati itakayosaidi kupunguza wimbi la uhalifu
pamoja na ajali barabarani.
Amesema mara nyingi Wahalifu wamekuwa wakitumia
njia nyingi kufanya uhalifu na kukimbilia mikoa ya jirani hivyo
mkutano huu ambao unahudhuriwa na Makamanda pamoja na wakuu wa upelezi
utasaidia kuwabaini ikiwa na kusambaratisha mtandao uliopo
Mkutano huo ni watatu baada ya mkutano wa kwanza
kufanyika Mkoani Iringa na wapili ulifanyika Mkoani Morogoro na kwamba
wajumbe wanatarajia kutoka na maadhimio mapya.
Na Mbeya yetu
................................................................................................................
MUONEKANO WA DARAJA LA KIGAMBONI DSM
Daraja
la muda la kigamboni likiwa limemalizika ambapo hutumiwa na mafundi na
magari ya kubebea vifaa mbalimbali vya ujenzi kuvusha upande wa pili
kwaajili ya ujenzi wa daraja la kudumu
........................................................................................................................Wizara yaendelea kusisitiza MSD iliuziwa ARV ‘feki’ Wizara yaendelea kusisitiza MSD iliuziwa ARV ‘feki’
Serikali
kupitia Wizara ya ya Afya na Ustawi wa Jamii imeendelea kusisitiza
kwamba Kampuni ya TPI Ltd iliiuzia Bohari ya Dawa (MSD) dawa bandia za
kupunguza makali ya Ukimwi aina ya TT-VIR 30 toleo Na.0C.01.85,kwa
mujibu wa nyaraka zilizopo na kwamba dawa hizo zilibainika kuwa ni
bandia.
Msisitizo
huo umetolewa katika vyombo vya habari jana na ofisi ya Wizara ya afya
na Ustawi wa jamii kupitia kwa msemaji wake Nsachris Mwamwaja ili
kuondoa mkanganyiko ambao umeanza kujitokeza kwa wananchi.
Katika
taarifa hiyo Serikali imesema kuwa kama ilivyoelezwa katika taarifa
mbalimbali za umma zilizokwisha kutolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii pamoja na TFDA kuhusiana na suala hili, bado inasisitizwa dawa
hizo zilikuwa bandia.
"Tunapenda
kusisitiza kwamba, waziri katika hotuba yake hakukanusha kuwa Kampuni
ya TPI Ltd iliiuzia MSD dawa bandia bali alieleza kwamba uchunguzi wa
awali katika kiwanda cha kampuni hiyo haukuonyesha dawa hiyo ilizalishwa
na TPI Ltd bali vifungashio ni vya TPI Ltd na nyaraka zinaonesha TPI
Ltd kuiuzia MSD dawa hizo bandia,"ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Aidha,
msemaji huyo wa wizara katika taarifa hiyo alieleza kuwa vyombo vya
usalama bado vinaendelea kulichunguza suala hilo ili kubaini chanzo na
wahusika wakuu wa dawa hizo bandia .
Hivyo kwa
kuzingatia unyeti wa suala hilo,wizara imetoa wito kwa vyombo vya
habari kusubiri hatma ya uchunguzi unaofanywa na vyombo vya usalama na
kuepuka kutoa taarifa ambazo zinaweza kupotosha umma na jitihada kubwa
za Serikali katika kupambana na dawa bandia nchini.
Mnamo Mei
9, 2013, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi katika
kuhitimisha hoja ya bajeti ya wizara alitolea ufafanuzi suala la dawa
bandia ya ARV kufuatia hoja zilizokuwa zimetolewa na Zarina Madabida
(Mb) kuhusu kuhusika kwa Kiwanda cha Dawa cha Tanzania Pharmaceutical
Industries Ltd (TPI) katika sakata la dawa bandia ya ARV.
..............................................................................................................................................................
Mbunge Msigwa akishuka katika gari ya polisi baada ya kufikishwa mahakamani mchana huu (Picha kwa hisani ya Fununublog)
……………………………………………
Watuhumiwa
70 wa vurugu za machinga na polisi mjini Iringa akiwemo mbunge wa
jimbo hilo mchungaji Peter Msigwa wamefanyiwa utaratibu wa
dhamana kutokana na mahakama kukubali kutoa dhamana baada ya
kusomewa mashitaka matatu huku mbunge akisomewa mashitaka mawili
likiwemo kushawishi na kufanya mkutano bila kibali .
Watuhumiwa wote wamekana mashitaka dhidi walikuwa wakifanyiwa utaratibu wa dhamana katika mahakama hiyo ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa Mheshimiwa Godfrey Isaya . Hata hivyo wamekana mashitaka yote yaliyotolewa ambayo shitaka la kwanza la mbunge ni kushawishi kufanya vurugu ,huku wengine wote kosa la kwanza kufanya mkutano bila kibali , kuharibu mali kinyume na sheria na kufanya vurugu . Dhamana ya watuhumiwa hao ilikuwa ni wadhamini wao kusaini hati ya dhamana yenye thamani ya Tsh milioni 1 na kuwa na mdhamini mmoja mwaminifu.
Mbunge Msigwa akishuka katika gari hilo la polisi tayari kwa kuelekea chumba cha mahakama
Mbunge Msigwa akiwa na gazeti mkononi baada ya kufikishwa mahakamani leo
Watuhumiwa wengine 70 wa vurugu za machinga na polisi wakishuka katika karandinga la polisi
|
No comments:
Post a Comment