Mbunge mchungaji Peter Msigwa |
Polisi waliotoka kumkamata mbunge Msigwa leo |
POLISI YATUMIA NGUVU KUTAWANYA WANANCHI MTAA WA MASHINE TATU, WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO MAARUFU KWA JINA LA MACHINGA WAKIWA NA MBUNGE WAO,
Francis Godwin, Iringa
MASAA zaidi ya 6 ya
mapambano kupiga mabomu ya machozi na
kurushiana mawe kati ya
wafanyabiashara ndogo ndogo (machinga ) na askari
wa kikosi cha kutuliza
ghasia (FFU) mkoani Iringa
yaishia pabaya kwa jeshi la
polisi kumkamata mbunge wa
jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (chadema) na
watu wengine zaidi ya 60
Polisi watumia mabom ya machozi kutawanya machinga wapiga mabomu hadi stendi kuu ya mabasi abiria
walazimika kutimua mbinu na kuacha mizigo yao katika magari huku machinga hao wakitumia mawe na kuchoma mataili moto barabarani kuvunja vioo vya gari la Zimamoto na kuharibu mali mbali mbali kama njia ya
kupambana na polisi
Tukio hilo la Mapambano kati ya machinga na polisi lilitokea leo kuanzia muda wa saa 3 asubuhi
na kuendelea hadi saa 8 mchana katika eneo la Mashine tatu
mjini Iringa na maeneo mbali
mbali ya mji wa Iringa .
Askari huo walilazimika
kukesha wakilinda eneo hilo
kufuatia kauli ya mbunge
Msigwa aliyoendelea kuitoa
katika mikutano yake ya hadhara mjini hapa
kuwhamasisha machinga hao ambao
Halmashauri ya Manispa ya
Iringa iliwahamisha eneo hilo la mashine tatu na kuwapeleka
eneo la Mlandege kabla ya mbunge
Msigwa kuwahamasisha kurejea tena
eneo hilo.
Kabla ya mbunge
Msigwa kufika eneo hilo majira ya saa 3 asubuhi machinga hao ambao
walikuwa wamejikusanya makundi
madogo madogo bila kupanga
biadhaa zao walisikika wakidai
kumsubiri mbunge Msigwa kama
alivyopata kuwaahidi kuwa atafika
eneo hilo kuungana nao kwa kuwa
machinga mpya .
Hata hivyo baada ya mbunge
huyo kufika akiwa na gari lake la
kibunge ambalo lilikuwa lilikokota
tela la
kuhifadhia mizigo alisimama eneo hilo na
kuendeleza msimamo wake wa kuwataka machinga kupambana na baada ya muda alitoweka eneo hilo kabla ya polisi
kuanza kuwatawanya machinga hao kwa mabomu ya machozi .
Wakizungumzia hali
hiyo ambayo ni ya kwanza kutokea katika mji wa
Iringa wakazi wa mji wa Iringa
walisema kuwa mbunge na
viongozi wengine wa
serikali wanapaswa kulaumiwa kwa
kushindwa kutumia njia nzuri
ya kukutana kwa ajili ya kumaliza mvutano huo
ambao unaendeshwa kisiasa zaidi.
Festo Sanga
alisema kuwa hali
ilipofikia ni mbaya zaidi na hivyo
busara zinahitajika kwa ajili
ya kutatua tatizo
hilo ikiwa ni pamoja na
kutazama eneo zuri kwa ajili ya
machinga bila kuendelea
kuonyeshana ubabe .
Sanga alisema kuwa machafuko yaliyojitokeza leo ni machafuko ambayo wakazi wa mji
wa Iringa walikuwa wakishuhudia katika vyombo
vya habari katika mikoa
mingine ukiacha lile la Septemba 2 mwaka jana lililotokea kijiji
cha Nyololo kati ya wafuasi wa Chadema na polisi na kupelekea kifo cha
aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya
waandishi wa habari mkoa wa Iringa marehemu Daud Mwangosi.
“Kweli katika hili
mbunge wetu hapaswi kuendelea
kulazimisha machinga kuvunja sheria
ila anayo nafasi ya kukutana na
viongozi wenzake ili
kutafuta suluhu ya jambo
hilo vinginevyo wanaoteseka na
machinga na wale waliokamatwa kwa vurugu hizo
ujue wengi waliopigwa mabomu ya machozi si machinga wengine
walikuwa wasafiri na badhi
yao walikuwa wakielekea makanisani ”
KUhusu kukamatwa kwa
mbunge huyo na kuhojiwa na polisi
juu ya vurugu hizo Sanga alisema kwa upande wake analipongeza jeshi la
polisi kwa kutumia busara zaidi
ya kumkamata mbunge
kama mhusika mkuu na kuliomba
jeshi la polisi kuwaachia wananchi
waliokamatwa kwa vurugu
hizo.
Huku Sarah
Kalinga alidai kuwa
chanazo cha machafuko hayo ni mvutano kati ya CCM na Chadema na kuwa
ilipaswa vyama vyote viwili
kukutana na kuwasaidia machinga
badala ya kuwanyanyasa kwa
kutumia nguvu kuwabana .
Hata hivyo alisema wao kama walalahoi wanampongeza mbunge wao kwa kuonyesha kuwapigania japo
haungi mkono njia inayotumiwa na mbunge
ya kuwahamasisha kuvunja
sheria na kuwa matatizo na
majeraha wanapata wao
wananchi na sio mbunge.
Awali mbunge
mchungaji Msigwa kabla ya kukamatawa na
jeshi la polisi alitoweka katika
mazingira tata katika eneo hilo la mashine tatu na
kuibukia eneo la chuo kikuu cha
Tumaini Iringa ambako kulikuwa na harambee
ya kuchangia Kanisa na mgeni rasmi akiwa
waziri mkuu mstafu Frederick Sumaye na mara baada ya
shughuli hiyo kumalizika ndipo alipokamatwa na polisi na
kufikishwa kituo cha polisi.
Kabla ya
kukamatwa kwake mbunge Msigwa
alizungumza na mwandishi wa habari hizi
na kuwa yupo tayari kukamatwa wakati
wowote na kuwa kamwe ataendelea
na msimamo wake wa
kuwataka Machinga kufanya biashara
eneo hilo.
Mbali ya
kukamatwa kwa mbunge
Msigwa kwa kuhusishwa na vurugu hizo pia
jeshi la polisi mkoani Iringa
linawashikilia watu wengine
zaidi ya 60 akiwemo aliyekuwa
kampeni meneja wa Chadema jimbo la Iringa mjini na mgombea udiwani
kata ya kwa Kilosa Abuu Changawa Majeck.
Huku idadi ya
majeruhi waliojeruhiwa kwa kupigwa mawe na machinga na badhi ya machinga waliokamatwa kwa vurugu
hizo pia wakijeruhiwa vibaya wakati
wakipambana na polisi hao.
Taarifa kutoka jeshi
la polisi zilizothibitishwa na kamanda
wa polisi mkoa wa Iringa Michael
Kamuhanda zinadai kuwa
watu zaidi ya 60 ndio wamekamatwa
hadi sasa na jitihada za
kuwasaka wengine waliohusika
katika vurugu hizo ambazo zimesababisha uharibifu mkubwa wa
mali za
wananchi unaendelea.
Huku akidai mali mbali mbali
zimeharibiwa likiwemo gari hilo
la zimamoto mjini Iringa pamoja na uharibifu
mwingine mdogo mdogo
wa mali za wananchi .
Jeshi hilo la
polisi limesema kamwe halipo tayari kumwachia mbunge Msigwa kwa leo hadi hapo
atakapofikishwa mahakamani Kesho
.................................................................................................................
Rais Kikwete afungua na kuongoza semina ya Wabunge wa CCM Dodoma
Mwenyekiti
Wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua semina maalum ya
wabunge wa CCM ilkiyofanyika katika ukumbi wa White House mjini Dodoma
leo.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Spika wa bunge Anna Makinda,
Katibu wa Wabunge wa CCM Jenista Mhagama, Waziri mkuu Mizengo
Pinda,Makamu wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana(picha na Freddy Maro)
Baadhi ya wabunge wa CCM waliohudhuria semina maalum iliyofanyika katika ukumbi wa White House mjini Dodoma leo.
..............................................................................................................................
UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) na Umoja wa Wanawake (UWT) wa Chama hicho Mkoa wa Mbeya wametoa matamko makali kupinga kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Dk. Wilbroad Slaa pamoja na Mkewe juu ya Raisi Kikwete.
UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) na
Umoja wa Wanawake (UWT) wa Chama hicho Mkoa wa Mbeya wametoa matamko makali
kupinga kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo(CHADEMA) Dk. Wilbroad Slaa pamoja na Mkewe juu ya Raisi Kikwete.
Matamko hayo yalitolewa na Wenyeviti hao
katika Mkutano na Vyombo vya habari uliofanyika katika Ofisi za UVCCM Mkoa wa
Mbeya, ambapo walisema kamwe hawawezi kufumbia macho maneno ya uzushi na
uchonganishi kati ya Serikali na wananchi.
Akisoma tamko Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Mbeya
Amani Kajuna alisema Umoja wa Vijana hauko tayari kufumbia macho matusi
anayotukanwa Raisi Kikwete na Dk Slaa anapokuwa akihutubia wanachama wake
jukwaani.
Alisema katika Mkutano alioufanya Mei 12, Mwaka
huu Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya Dk. Slaa akihutubia wananchi kuwa Raisi
Kikwete ni Freemason, Mdini, Mawaziri hawamsaidii pia ni Mafisadi na
kuongeza kuwa ana ushahidi wa Cd ambazo Raisi Kikwete akihamasisha udini
na kuhusu uchinjaji.
Alisema maneno ya Dk. Slaa ni uzushi ambao
unalengo la kufitinisha Watanzania na Serikali ya Chama cha Mapinduzi hususani
anapofanya mikutano ya Hadhara katika Mkoa wa Mbeya ambapo aliongeza kuwa
Ufisadi anaousema yeye kwa Mawaziri wa Ccm ili hali yeye mwenyewe anaongoza kwa
ubadhilifu wa fedha za Wananchi.
Alitolea mfano wa ubadhilifu uliofanywa na
Chadema mkoani Mbeya kuwa ni pamoja na Kitendo chaMwenyekiti wao Freemani Mbowe
kuchangisha fedha Milioni Tatu kwa wananchi kwa kile alichodai zingetumika
kununulia maji na matibabu wakati wa maandamano lakini hazikufanya kazi hiyo na
hazijulikani zilipo.
Kajuna alisema mbali na fedha hizo
kutokujulikana matumizi yake pia Dk. Slaa alichangisha fedha zingine
Shilingi Laki saba kwa ajili ya posho ya Wabunge waliofukuzwa bungeni jambo
ambalo lilileta sintofahamu kwa wakazi wa Jiji la Mbeya.
Alisema ufisadi mkubwa uliopo ndani ya Chadema
ambao kila Mwezi wanapata ruzuku ya takribani Milion mia Tatu lakini hawajawahi
kujenga hata chumba kimoja cha Zahanati wala kutoa msaada kwa wananchi wasiojiweza
lakini wao wanazidi kuwachangisha wananchi.
“ Jamani watanzania fungukeni muone huyu
kiongozi wa namna gani Mlafi, Mchoyo na mchochezi asiyependa kuona amani
ya Nchi ikistawi” alisema Kajuna.
Aliongeza kuwa pamoja na Chadema kupata fedha
zote hizo bado zinaishia mikononi mwa watu wachache hususani Dar Es Salaam
ambapo Mikoani hawazipati na ndiyo sababu Ofisi za Chadema Mkoa wa Mbeya
zilifungwa kutokana na kutolipia pango la Nyumba deni la Shilingi Laki tatu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Uwt Prisila Mbwaga
alisema kama Wanawake wa Chama cha Mapinduzi hawako tayari kuona matusi
yanayotolewa na Mke wa Dk Slaa Josephine Shumbusho juu ya Mama Salma Kikwete
kwamba anachangia kuibomoa Nchi.
Alisema Shumbusho alinukuliwa akitoa matusi
makubwa dhidi ya Mama Salma katika mkutano wa hadhara uliofanyika Wilayani
Mbozi akisema ameshindwa kumshauri raisi kuhusu uongozi na namna ya kuongoza
nchi.
Aliongeza kuwa katika matusi yake alimtuhumu Mke
wa Raisi kuwa ni Mwanamke Mpumbavu anayeibomoa nchi nyumba yake kwa mikono yake
Mwenyewe kama Biblia inavyosema na kwamba yeye atakuwa tayari kumshauri Dk.
Slaa atakapokuwa Raisi mwaka 2015.
Kutokana na tuhuma hizo Umoja wa Wanawake wa
Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mbeya wamemtaka Mke wa Dk. Slaa kuacha tabia ya
kumsema vibaya Mama Salma na akiendelea hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi
yake.
Picha na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment