Thursday, June 6, 2013

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewatunuku Nishani Askari 29 wa Magereza kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

 
Msafara wa Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja ukiwasili katika viwanja vya Chuo cha ufundi Ruanda Jijini Mbeya kwa ajili ya kuwatunuku nishani Maaskari wa Jeshi la Magereza 
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja  Akikagua Gwaride maalum lililoandaliwa na maaskari wa Jeshi la Magereza kwa ajili yake mara baada ya kuwasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuwatunuku nishani Maaskari.

 Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja  akipokea Salam za heshima kutoka kwa Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mbeya

 Baadhi ya Maaskari wa Jeshi la Magereza wakitoa heshima kwa Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja  (ambaye haonekani pichani) wakati wa hafla ya kuwatunuku nishani.
 Brass band ya Jeshi la Magereza kutoka Kiwira Rungwe wakitumbuiza katika Sherehe hizo 
 Baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Magereza wakiwa wamesimama kwa ukakamavu kutoa heshima kwa Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja 
 Baadhi ya Maaskari wastaafu wa Jeshi la Magereza pamoja na maofisa wakifuatilia kwa umakini Sherehe za    kutunuku nishani 
 Baadhi ya Maaskari wakisubiri kutunukiwa nishani kutoka kwa Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja 
SACP C. A Keenja akitaja majina 29 ya Maaskari wanaotakiwa kutunukiwa Nishani ya Utumishi uliotukukuka Tanzania, Utumishi Muda Mrefu Tanzania, Utumishi mrefu na tabia njema na Mwenge wa Uhuru daraja la nne.

 Askari Mwanamke akitembea kwa ukakamavu kuelekea eneo linalotumika kutunukia Nishani kwa Maaskari wa Jeshi la Magereza 
 
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja (kulia) akimvisha nishani ya utumishi ulio Tukuka Tanzania ACP Hawa M. Simon ambaye pia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Rukwa.
 Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja Akimvalisha Nishani SGT ambaye Jina lake halikupatikana Mara Moja.
 Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akimvisha Nishani ya utumishi mrefu na tabia njema SGT Yusufu F. Nzunda kutoka chuo cha Magereza Kiwira 
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja Akimvalisha Nishani SGT ambaye Jina lake halikupatikana Mara Moja.

 Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja Akimpongeza Askari mara baada ya kutunukiwa nishani ya utumishi mrefu na Tabia njema.
 Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja Akiwa katika picha ya pamoja na Maaskari 29 waliotunukiwa Nishani mbalimbali 
  Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Magereza wastaafu.

 Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Mbeya


Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake waliotunukiwa Nishani
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akibadilishana jambo  na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Barakael Masaki
Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja  akiwa katika picha ya Pamoja na Afisa Habari wa Jeshi la Magereza Makao Makuu Insp. Lucas Mbonje wakizungumza na waandishi wa Habari mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya.

**********************
RAISI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewatunuku Nishani mbali mbali Askari 29 kwa Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Nyanda za juu kusini.
Mbali na Nishani hizo pia Jeshi hilo limesema limejipanga kuhakikisha linaanza kujitegemea na kuepukana na Bajeti za Serikali katika kujiendesha kutokana na uwepo wa Rasilimali nyingi zinazoweza kuzisaidia hususani Wafungwa na Ardhi kwa ajili ya kuzalisha Chakula.
Kauli hiyo imetolewa Leo na Kamishina Jenerali wa Magereza Nchini, CGP John C. Minja wakati wa hafla fupi ya kuwatunuku Nishani Maaskari wa Jeshi hiyo iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Magereza Ruanda Jijini Mbeya.
CGP Minja amesema Jeshi la Magereza linauwezo wa kujiendesha kutokana na kuwa na rasilimali na nguvu kazi ambazo zitatumika katika kuzalisha chakula ili kuepuka kusubili Fedha kutoka Serikalini  ambazo huchukua muda mrefu kupatikana na milolongo kuwa mingi.
Ameongeza kuwa hata baada ya kuanza kujitegemea kwa Jeshi hilo kutawapunguzia gharama walipa kodi ambao wamekuwa wakikatwa fedha zao kila siku ili kufanikisha upatikanaji wa Chakula kwa Wafungwa na Shughuli nzima za Jeshi la Magereza Nchini ikiwemo upungufu wa Majengo.
Kamishina huyo pia ameiomba Serikali kuunga mkono juhudi hizo na mikakati ya kutaka kujitegemea ili kuzipunguzia Taasisi Mbali mbali kama Wabunge ambao kila mara wamekuwa wakijadili suala la uboreshaji wa Jeshi la Magereza Nchini.
“ Tangu niingie madarakani lengo langu na ajenda kuu ni kuboresha jeshi la Magereza ili liweze kujitegemea ikiwa ni pamoja na kuwapunguzia gharama zisizokuwa za ulazima kwa wanaokatwa fedha  katika vipato vyao” alisema CGP Minja.
 Katika Hafla hiyo Jumla ya Askari 29 walitunukiwa Nishani  Kutoka kwa Kamishina Jenerali wa Magereza ambaye alitumia Mamlaka aliyokasimiwa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Kifungu cha 34(4) Cha katiba ya Jamhuri ya Muungano ya kuwavisha Nishani   Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza ambao walitunukiwa Nishani mbali mbali lakini hawakuvishwa na Raisi Aprili 26, Mwaka huu.
SACP Keenja ambaye ndiye alikuwa akitaja majina ya Askari waliotunukiwa Nishani hizo alisema  Orodha ya majina ya Maafisa na Askari pamoja na Nishani zao yameelezwa na kuainishwa katika Taarifa ya Kawaida na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali namba 84/2013 la April 26, Mwaka huu.
Alizitaja Nishani hizo kuwa ni pamoja na Nishani ya Utumishi uliotukuka ambayo hutunukiwa Maafisa waliokwenye Utumishi wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania ambapo kwa Jeshi la Magereza hutunikiwa wenye Cheo cha Mrakibu au wa juu ya Cheo hicho waliotumikia jeshi hilo kwa Miaka 20 Mfululizo ambayo alitunukiwa Askari mmoja ambaye ni ACP Hawa Mollel Simon ambaye pia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Rukwa.
Nishani ya Pili hutunukiwa kwa Askari kuanzia Nyota Moja ambao wametimiza utumishi wa miaka isiyopungua 15 mfululizo akiwa na tabia njema ya kuweza kusifiwa, Nishani ambayo alitunukiwa Askari mmoja ambaye ni ACP Ally Abdalah Kaherewa ambaye pia ni Mkuu wa Magereza  Mkoa wa Ruvuma.
Nishani ya Tatu ni kwa ajili ya askari wenye Cheo cha Wakaguzi, Wakaguzi wasaidizi, Stesheni Sajini, Sajini na Koplo waliotumikia jeshi la Magereza miaka 15 Mfululizo ambayo huitwa Nishani ya Utumishi Mrefu Tanzani ambayo walitunukiwa Askari 18.
SACP Keenja ameitaja Nishani ya nne waliotunukiwa asakari hao kuwa ni kwa wale wanajeshi waliohai ambao walizaliwa Disemba 9, 1961 au kabla ya hapo na mbao wamefanya kazi katika katika Majeshi ya Ulinzi na Usalama kwa muda wa Miaka 35 au zaidi wakiwa Jeshini wenye sifa na tabia njema ambayo huitwa Nishani ya Mwenge wa Uhuru daraja la Nne waliyotunukiwa askari 9.
Na Mbeya yetu Blog.
......................................................................................................................

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU MABADILIKO KWA BAADHI YA MAKAMANDA

Advera-Senso
     (Msemaji wa jeshi la polisi nchini Advera Senso-SSP)
………………………………………………………………………………
 Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734                                                                                    Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556                                                                                                           S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:                                                                                       DAR ES SALAAM.
                                                                                        06 JUNI, 2013
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Said Mwema, amefanya mabadiliko ya makamanda na wakuu wa upelelezi katika baadhi ya mikoa hapa nchini.
Katika mabadiliko hayo aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Michael Kamhanda amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhani Mungi ambae alikuwa Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai.
Aidha, DCP Ally Mlege aliyekuwa Makao Makuu ya Polisi amehamishiwa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwenda kuwa Mkuu wa utawala na raslimali watu.
Vilevile, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi wa makosa ya jinai  na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Arusha ACP Camilius Wambura. Aidha, ACP Duwan Nyanda aliyekuwa Makao Makuu ya Upelelezi anaenda kuwa Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Arusha.
Uhamisho huo ni wakawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (T).

.....................................................................................................

MBAKAJI APOTA KICHAPO

untitled20 9fcaf
Mtu alie sadikika kumbaka mototo  wa umri wa miaka nane mkazi wa manispaa ya Iringa,  akipokea kichapo toka kwa wananchi wenye hasira   huku akisindikizwa kituo cha Polisi .
...................................................................................................................................................... 

STARS YAWASILI MOROCCO WATANZANIA WANASUBIRI KUPEWA RAHA

taifa-stars-2 82d75
Taifa Stars imewasili leo hapa Marrakech, Morocco tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Morocco itakayochezwa Jumamosi- Juni 8 mwaka huu.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia hoteli ya Pullman ambayo pia ilifikia timu ya Ivory Coast ilipokuja kucheza na Morocco. Stars imetua na kikosi cha wachezaji 21 wakati Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu watawasili kesho- Juni 4 mwaka huu saa 8 mchana wakitokea Maputo, Msumbiji ambapo jana- Juni 2 mwaka huu timu yao ya TP Mazembe ilicheza mechi ya Kombe la Shirikisho.
Mechi kati ya Stars na Morocco itachezwa kuanzia saa 3 usiku kwa saa za hapa ambapo Tanzania itakuwa saa 5 usiku
..................................................................................................................... 

No comments: