Kamishna
wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akipokea Salamu za heshima
kutoka kwa wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba
20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika chuo cha
Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya
Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akikagua wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi
namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika
chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya
Kamishna
wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akimtunuku cheo cha Ukoplo
Askari B4448 Patric Babara kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo ya uongozi
daraja la kwanza kozi
namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika
chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya
Kamishna
wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akimtunuku cheti muhitimu
B7348 Patrick Chalemta aliye fanya vizuri masomo ya Darasani katika
mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi
namba 20
Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akimtunuku cheti
muhitimu aliye fanya vizuri somo la kulenga shabaha 3163 Tatu Amri katika mafunzo ya
uongozi daraja la kwanza kozi
namba 20
Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akimpa zawadi
muhitimu 3914 Leonida Hillu ya mwnafunzi mwenye Nidhamu usafi na ukakamavu katika mafunzo ya
uongozi daraja la kwanza kozi
namba 20
Baadhi ya Maofisa wakitoa heshima katika mahafali ya mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi
namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika
chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya
Kamishna
wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga (kushoto) akiwa na Mkuu wa
Chuo cha Magereza Kiwira Staniford Ntirudura wakipokea Salamu za
heshima kutoka kwa wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi
namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika
chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya
Wahitimu wakiwa kwenye Gwaride wakipita kwa mwendo wa Haraka mbele ya Mgeni Rasmi.
"Hima..... Hima.... Hima!.... " Ni salamu ya utii ikiongozwa na Parade Kamanda SP Lucas Ndoteela
Baadhi ya Maofisa wakifuatilia kwa Makini shughuli za Mahafali
Baadhi ya Wahitimu wakionesha umahili wa kupambana na maadui
Watoto wanaolelewa na kituo cha malezi ya watoto wadogo katika chuo cha Magereza wakitumbuiza katika Sherehe za Mahafali
Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira, Kamishina msaidizi wa Magereza Staniford Ntirudura akizungumza jambo katika mahafali hayo.
Wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 katika
sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika chuo cha Magereza
Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya, wakifuatilia matukio yanayo endelea katika Sherehe zao.
Wahitimu B5414 Peter Ndalahwa na 3469 Matha Mwanjala wakisoma Risara katika mahafali yao
Muhitimu B3494 Willy Timoth akisoma Shairi wakati wa mahafali
Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akizungumza na wahitimu
********************
JUMLA ya Askari 984 wa Jeshi la
Magereza, wanaume 845 na wanawake 139
wametunukiwa Vyeo vya Ukoplo
baada ya kuhitimu mafunzo ya Uongozi daraja la Kwanza kozi namba 20 katika Chuo
cha Magereza Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
Vyeo hivyo vilitolewa na
Kamishina wa Fedha na Utawala Gaston Sanga kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa
Magereza katika Sherehe za ufungaji wa mafunzo hayo zilizofanyika katika
Viwanja vya Chuo hicho leo Juni 7, Mwaka huu.
Akizungumza katika mahafali
hayo, Kamishina wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga amesema Askari wa
Jeshi la Magereza Nchini wanatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili,
taratibu na kanuni za kazi kwa kufuata uwajibikaji, unyenyekevu, ukakamavu,
ujasili, upendo, ushirikiano, uvumilivu, uaminifu na nidhamu.
Kamishina Sanga amesema
Maaskari wanapaswa kuzingatia elimu waliyopewa wakati wa mafunzo ili wakawe
mfano kipindi cha utendaji kazi wao ikiwa ni pamoja na kuhamasisha na
kuwaongoza wenzao ambao hawakupatiwa elimu kama yao.
Aidha amewaasa kutowatesa
Wafungwa walioko magerezani bali kuwahudumia kwa kuzingatia kuwa wanamhudumia
binadamu kama walivyo wao na siyo
kuchukua nafasi ya kuwanyanyasa bila kuogopa haki na Stahili za binadamu
japokuwa ni wafungwa.
Picha na Mbeya yetu Blog
.........................................................................................................................
MBEYA CITY MOTO WAKE HAUZIMWI, WASUKA KIKOS MATATA CHA MAKINDA KUZISUMBUA TIMU ZA LIGI KUU MSIMU UJAO!!
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Ikiwa
katika harakati za kujenga timu ya muda mrefu, klabu mpya ya ligi kuu
soka Tanzania bara msimu ujao, Mbeya City ya jijini Mbeya anaendelea na
mpango wake wa kuandaa kikosi cha pili cha klabu hiyo kwa lengo la kuwa
na timu ya ushindani kitaifa na kimataifa.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo inayonolewa na kocha Juma Mwambusi, Mwalimu Maka Mwalwisyi ameimabia FULLSHANGWE
kuwa kwa sasa wanaendelea na mazozezi ya kikosi cha pili ambacho
kimeteuliwa na benchi la ufundi la klabu hiyo, wakati viongozi wa timu
wakiweka mambo safi ili timu A iingeia kambini kujiandaa na michuano ya
ligi kuu msimu ujao.
“Tunataka
kuijenga falsafa ya Mbeya City, kufanikisha hilo tunahitaji kuwa na
timu bora ya vijana ambao tutakuwa tunawapandisha timu A. Kwasasa tupo
na vijana wengi sana, tunajaribu kuchambua wanaotufaa ili kupata timu ya
chini ya umri wa miaka 20”. Alisema Mwalwisyi.
Kocha huyo alisema kuwa wachezaji wao wanaonesha juhudi kubwa ya kujifunza, jambo ambalo linatia matumaini kwa benchi la ufundi.
“Vijana
wana vipaji vya hali ya juu. Wanacheza kwa kujituma sana, mbali na hayo
wana nidhamu ya mazoezi, wanazingatia sana maelekezo ya waalimu wao”.
Alisema Mwalwisyi.
Mwalwisyi alisisitiza kuwa malengo yao ni kuifanya Mbeya City kuwa klabu ya ushindani mkubwa na sio washiriki wa ligi kuu bara.
Aidha
alisema katika kuhakikisha hilo, benchi la ufundi linataka kuwekeza
katika soka la vijana ambao ndio chagua sahihi kwa soka la sasa.
“Soka
la kisasa kwa kweli linahitaji sana vijana ambao wanaenda sambamba na
kasi ya mpira wa dunia, kwa kulijua hilo, Mbeya City lazima iwe kitalu
cha kuzalisha wachezaji wa Tanzania”. Alisema Mwalwisyi.
Pia
kocha huyo aliwataka mashabiki wa Mbeya kuwaunga mkono wao na ndugu zao
Tanzania Prisons, wawakilishi wa jiji la Mbeya michuano ya ligi ya
Premia ya Tanzania bara.
....................................................................................................................................................
Mbatia ataka walioruhusu vitabu ‘feki’ vitumike sasa wasulubiwe
Dodoma. Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia ameitaka Serikali
isiishie kuivunja Kamati ya Ithibati ya Vifaa vya Elimu, (EMAC), na
badala yake iende mbali zaidi kwa kuwachukulia hatua za kisheria wajumbe
wote wa kamati hiyo.
Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa
NCCR-Mageuzi alisema jana mjini Dodoma kuwa kamati hiyo inahusika moja
kwa moja kuua elimu nchini kutokana na kufumbia macho ufisadi ulioruhusu
kusambazwa kwa vitabu visivyo na ubora.
“Hawa ni wahujumu uchumi wa nchi yetu; wanahusika
kuididimiza elimu yetu... Inaonyesha wazi kuwa watunzi wa vitabu vile
hawakutumia mitalaa. Kutokuongozwa kwa mitalaa kumesababisha vitabu vile
kukosa ubora. Haiwezekani mwandishi, mhariri na mhakiki, awe mtu
mmoja.” alisema.
Mbatia alisema Emac imetoa ithibati kwa vitabu
vyenye maudhui yasiyo sahihi au dhaifu na ambayo hayamo kwenye
mihutasari huku baadhi yao vikiwa vimeiwakilisha vibaya Bendera ya Taifa
pamoja na Nembo ya Taifa kwenye baadhi ya vitabu hivyo.
Alisema miongoni mwa vitabu vilivyopitishwa na
Emac havina majina ya waandishi na kwamba badala ya jina la mwandishi
limewekwa jina la kampuni ya uchapishaji.
“Hakuna hata kitabu kimoja chenye wasifu wa
mwandishi na karibu vitabu vyote havina wahariri wakati ni lazima kila
kitabu kiwe na angalau mhariri mmoja” alisema Mbatia.
Alisema kasoro nyingine iliyopo katika vitabu
hivyo ni makosa mengi ya lugha iliyotumika kuandikia ambayo ni
Kiswahili, hali inayoonyesha kuwa vitabu hivyo havikupitishwa na Baraza
la Kiswahili la Taifa (Bakita).
“Aibu nyingine ipo katika maelezo ambapo eti
wameandika mitalaa ya shule za awali unamwezesha mwanafunzi kukua
kiuchumi, kisiasa na kijamii…na kwa wale wa shule ya msingi, wanasema
mtalaa unamsaidia mwanafunzi kupata uelewa wa lugha ya Kifaransa ili
aweze kupata ajira…Kweli mwanafunzi wa shule ya awali anatakiwa akue
kiuchumi, kisiasa na kijamii….na hii lugha ya Kifaransa inatoka wapi
katika mtalaa wa Tanzania” alihoji Mbatia.
Mbatia aliitaka Serikali vilevile iviondoe sokoni
vitabu vyovyote vya kiada na ziada vyenye maudhui potofu kama
inavyofanya kwa bidhaa nyingine zisizo na ubora.
“Adhabu zitolewe kwa watayarishaji na wamiliki wa
vitabu duni vitakavyoingizwa shuleni kinyume na taratibu ili kuzuia
matendo ya rushwa…chombo cha kupokea taarifa kutoka kwa wadau wa elimu
kuhusu vitabu duni kiundwe” alisema.
Alisema endapo Serikali itapuuza na kuviacha
vitabu hivyo visivyo na ubora kuendelea kutumika, ubora wa elimu utazidi
kuporomoka kwa sababu wanafunzi watalazimika kutumia vitabu visivyo na
ubora.
........................................................................................................................................................
........................................................................................................................................................
No comments:
Post a Comment