Monday, June 10, 2013

WAFANYABIASHARA WATOGO (MACHINGA) WAFURAHIA UTARATIBU WA HALMASHAURI YA RUNGWE MKOANI MBEYA KUWATENGEA SEHEMU MAALUM YA KUFANYIA BIASHARA ZAO

ASUBUHI NA MAPEMA WAFANYA BIASHARA WADODOGO MJI WA TUKUYU WAKIANZA KUPANGA BIASHARA ZAO

SASA HAKUNA KUZURULA NA BIASHARA  NA KUFANYIA BIASHARA SEHEM ZISIZO RUHUSIWA

MTAA MPYA WA MACHINGA TUKUYU MJIN


KULIA PAPA CHERI AKIWA KATIKA MICHAKATO YAKE
MUUZA SAMBUA MAARUFU TUKUYU

UTARATIBU WA KUWEKA TAKATAKA NA GALI LA TAKA KUZIONDOA KUPELEKA DAMPO
.................................................................................................................................................

BAADA YA KUSIMAMA KWA MUDA UJENZI WA BARABARA YA CHUNYA UNAENDELEA KWA KASI KUBWA SASA .

Ujenzi wa Barabara ya Mbeya kuelekea Chunya , hili ni eneo Maarufu kona ya Mkoa

 
Barabara ya kiwango cha Rami kutoka Mbeya kuelekea Chunya eneo la Chalangwa
Ujenzi wa Barabara ukiendelea 
 Moja ya Gari likitoka Mbeya kuelekea Chunya
 Ujenzi ukiendelea kwa kasi katika eneo hilo.
 Mmoja wa wadau akiwa katika eneo ambalo Barabara hiyo inatengenezwa
Hili ni eneo ambalo lilikuwa ni kikwazo kikubwa kabla ya kujengwa na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wasafiri.

Wananchi Wilayani Chunya mkoani Mbeya waipongeza Serikali kwa kuharakisha ujenzi wa barabara  kutoka Mbeya, kuelekea Chunya  ambapo barabara hiyo inatarajiwa kuunanisha Mkoa wa Mbeya na mikoa ya jirani Singida, Dodoma na Tabora mara baada ya kukamilika kwake.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kuwa kwa sasa barabara hiyo inawapa matumaini makubwa kutokana na kasi kubwa ya ujenzi huo unaofanywa na Kampuni ya Kichina.

Hata hivyo wameelezea wasiwasi wao juu ya wamiliki wa vyombo vya usafiri wa abiria vinavyo tumika kwa sasa kukosa soko kutokana na ujenzi wa barabara hiyo.
.............................................................................................................................
Warioba: Ikulu kugawanywa
 
,Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba 
Na Fidelis Butahe, Mwananchi

Amesema kuwa kutokana na taifa kufanya mabadiliko ya Katiba ni lazima kuwepo mpangilio wa kugawana mambo mbalimbali yaliyokuwa chini ya Muungano ikiwamo majengo, wafanyakazi, Ikulu, hata vitendea kazi na kwamba utaratibu huo ni kama ule uliotumika wakati Tanganyika na Zanzibar zilipoungana.

 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema iwapo Mfumo wa Serikali Tatu utaridhiwa na wananchi ni lazima mambo yaliyo ndani ya Muungano yatagawanywa ikiwa ni pamoja na Ikulu ya Rais.
Amesema kuwa kutokana na taifa kufanya mabadiliko ya Katiba ni lazima kuwepo mpangilio wa kugawana mambo mbalimbali yaliyokuwa chini ya Muungano ikiwamo majengo, wafanyakazi, Ikulu, hata vitendea kazi na kwamba utaratibu huo ni kama ule uliotumika wakati Tanganyika na Zanzibar zilipoungana.
Kauli ya hiyo ya Jaji Warioba imekuja siku tatu tangu Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kueleza kuwa Tanzania Bara itaanza mchakato wa kutunga Katiba yake Aprili mwaka 2014 na kumalizika Desemba mwaka huohuo.
Jaji Warioba aliyasema hayo katika mahojiano maalumu na waandishi waandamizi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), inayochapisha magazeti ya Mwananchi, Mwananchi Jumamosi, Mwananchi Jumapili, Mwanaspoti, The Citizen na The Citizen on Sunday, Tido Mhando ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa MCL na Theophil Makunga, Meneja wa Uendeshaji na Biashara MCL.
Swali: Makao Makuu ya Serikali ya Muungano yatakuwa wapi?
Warioba: Ukibadili Katiba wakati wowote ni lazima kuwe na makubaliano fulani.
Unajua Serikali ya Muungano na Tanganyika ilikuwa pamoja, sasa ukianzisha Serikali ya Tanganyika, lazima kwenye mpangilio muanze kugawana hata wafanyakazi kwa kuwa wafanyakazi hao walikuwa ni wa Muungano. Hapo ndiyo mtaamua wafanyakazi gani watakwenda katika Serikali ya Tanganyika, watakaobaki katika Muungano na wale watakaokwenda Zanzibar.
Hata katika majengo hali inakuwa hivyo hivyo, lazima kutakuwa na majengo yaliyokuwa yakitumiwa na wizara mbalimbali na hata Ikulu. Hapo pia lazima myagawanye na kukubaliana viongozi wa Tanganyika watakuwa wapi na wale wa Muungano watakuwa wapi. Lakini, hata vifaa vya kutendea kazi navyo inatakiwa mgawane kulingana na makubaliano yenu.
Suala hili linategemea zaidi mazungumzo ya pande zote mbili, baada ya kukamilika kwa mchakato huu kwa sababu hii iliyopatikana sasa ni rasimu tu, ambayo itajadiliwa na wananchi kabla ya kuanza kwa Bunge la Katiba na baadaye kuwepo kwa kura ya maoni. 

Wapo watakaokuwa wakihoji kuhusu vyeo, katika hili itakuwa kama tulivyokuwa tukiungana Tanganyika na Zanzibar, wakati huo wapo ambao walikuwa wakuu wa mikoa na wakajikuta wameingia katika Muungano huku wakiwa na vyeo hivyo. Kilichofanyika ni kuendelea tu na nafasi hizo mpaka utakapofanyika utaratibu mwingine kwa njia ya mazungumzo.
Unajua jambo hili siyo jukumu la tume hii, tunaliacha kwa sasa na hatujui litakuwaje kwa sababu ni suala la mazungumzo.
Swali: Majukumu ya Rais yatakuwaje?
Warioba: Rasimu imeeleza majukumu (roles) ya Rais kama mkuu wa nchi, ambaye anakuwa kama taasisi na sisi tulichokifanya ni kujenga taasisi hizo, kwamba ijulikane akifanya chochote awe ameshauriwa, isiwe yeye peke yake.
.........................................................................................................................................................

No comments: