Tuesday, June 4, 2013

DELEVA NA MTOTO WAKE WAFARIKI HAPOHAPO BAADA YA KUTOKEA AJALI MBAYA ENEO LA UWANJA WA NDEGE KIWIRA TUKUYU WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA

HAPA NDIPO ENEO LINALOTAMBULIKA KAMA UWANJA WA NDEGE AMBAPO KILA MALA AJALI HUTOKEA KWA MAGALI KUFERI BREKI NA KUSHINDWA KUKATA KONA HIVYO KUPITILIZA BONDENI

MABAKI YA GALI AINA YA SCANIA T669ACU MALI YA KAMPUNI YA LAKE OIL ILIYOKUWA IKITOKEA DSM KUELEKEA KYELA

HAPA NDIPO WALIPOKUTWA KONDACTA ALIYENUSURIKA KIFO AMBAPO DEREVA WAKE NA WANAE WAMEFARIKI

KABLA YA KUPATA AJALI MAREHEMU ZAWADIEL ALIIKWEPA COSTA ILIYOKUWA NA ABILIA NA KUIVAA CENTA ILIYOBEBA NDIZI NA KWA USHUHUDA WA KONDACTA MAREHEMU ALISEMA "AFADHARI KUFA SISI KULIKO KUIGONGA GALI HII YA ABILIA" MWISHO ALIPOIKWEPA NDIPO AKAPOTEZA MUELEKEO ULIOFANYA GALI YAKE KUTUMBUKIA KORONGONI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE NA MWANE

MAREHEMU ZAWADIEL SAMWELI AMBAYE NDIYE DELEVA WA GALI LILILOPATA AJALI NA KUFA HAPOHAPO

MTOTO WA MAREHEMU ZAWADIEL AMBAYE HAKUFAHAMIKA JINA LAKE ILA ILIFAHAMIKA KUWA KIJANA HUYU NI MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE NA KWAKUWA NI KIPINDI CHA LIKIZO ALIAMUA KUMSINDIKIZA BABA YAKE ILI KUTEMBEA NA KUFAHAM MIJI NA KUFIKA MBEYA KYELA LAKINI SAFARI YAKE KUISHIA HAPA
NASIBU RAMADHANI AMBAYE NI KONDACTA WA GALI HILO AMBAYE AMEJERUHIWA KATIKA AJALI HIYO

MAJERUHI NASIBU RAMADHANI AKIPATA HUDUMA KATIKA HOSPITAL YA TUKUYU KABLA YA KUKIMBIZWA KWENDA HOSPITAL YA RUFAA MBEYA

MABAKI YA GALI SCANIA T669 ACU NA PALE JUU NDIPO BARABARA KUU ILIPO

MABAKI YA GALI

BAADA YA AJALI KUTOKEA POLISI KWA HARAKA WAKAFIKA ENEO LA TUKIO NA KUIMARISHA ULINZI ILI WATU WASIIBE MALI NA MAFUTA ZILIZOSALIA


LEO HAKUNA DILI "IJANA WA KIWILA WALIOZOEA KUIBA MAFUTA BAADA YA AJALI ZINAZOTOKEA MAENEO HAYO, LEO KWAKUWA POLISI WAPO NA WAMEIMALISHA ULINZI WANARUDI NA MADUMU YAKIWA TUPU

ALIYE VAA SUTI NI DIWANI WA KATA YA KIWIRA AKISHUHUDIA AJALI ILIYOTOKEA

MOJA YA GALI ILIYOONGOZANA NA GALI ILIYOPATA AJALI ENEO LA KIWIRA TUKUYU NA KUUA BABA NA MWANAE ALIYEMSINDIKIZA BABA YAKE KWAKUWA SASA NI KIPINDI CHA LIKIZO.

  ........................................................................................................

MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEA WAWASILI NCHINI TAYARI KWA MAZISHI

Umati wa waombolezaji ukijaribu kulikaribia jeneza la msanii huyo huku watu wngine wakijaribu kupiga picha wakati mwili wake ulipowasili kwenye uwanja wa JK Nyerere leo. 3 
Ukiingizwa kwenye gari. 4 
Wapiga picha wakipiga picha. 5 
P. Funk na wasanii wengine wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa JK Nyerere 9Mwanamuziki Lady Jay Dee akiwasili katika eneo hilo la mapokezi 10 
Ndugu na jamaaa wakiwa na majonzi huku wengine wakilia kwa uchungu. 11 
Hapa ni vilio tu wakimlilia Albert Mangwea 12 
Tipo na Bazo nao wameshiriki katika kuupokea mwili wa marehemu Albert Mangwea 13 
Edwin Temba na Abraham Mosi nao walijumuika katika mapokezi hayo.


Mwili wa Msanii Albert Mangweha 'Ngwair' a.k.a mimi au Cow Boy uwewasili jijini Dar es Salaam hii leo majira ya saa 8 mchana na kupokelewa na maelfu ya mashabiki, wasanii wenzake, ndugu jamaa na marafiki.

Mwili huo uliokuwa umehifadhiwa katika sanduku zuri la kupendeza ulipokelewa na kuingizwa katika kagi maalum la kubebea maiti na safari ya Muhimbili ilianza huku waombolezaji wakilisukuma gari hilo wakielekea Hospitali ya Muhimbili ambako mwili utahifadhiwa hadi kesho utakapo pelekwa viwanja vya Lidaz kwa heshima za mwisho.

Wasanii maarufu wa Tanzania kutoka makundi mbalimbali ya muziki wa kizazi kipya walifika uwanjani hapo kuupokea mwili wa mwenzao.

Mangweha aliyezaliwa Novemba 15, 1982 na kufariki Mei 28, 2013 anataraji kuzikwa katika Manispaa ya Morogoro eneo la Kihonda nyumbani kwa mama yake.

............................................................................................................

TAARIFA YA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 04. 06. 2013.

MWANDISHI WA HABARI RASHID MKWINDA ALIEPATA MADHARA
MBEYA PRESS CLUB
TAMKO LA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA LA KULAANI KUPIGWA KWA MWANDISHI WA HABARI RASHID MKWINDA WAKATI WA MECHI YA MPIRA WA MIGUU BAINA YA KIMONDO FC NA NJOMBE FC ILIYOFANYIKA JUNI 2 KATIKA UWANJA WA KUMBUKUMBU YA SOKOINE JIJINI MBEYA.

JUNI 2, mwaka huu kulikuwa na mechi ya mpira wa miguu ya Ligi ya Mabingwa wa mikoa baina ya timu ya Kimondo FC ya Mbozi mkoani Mbeya na Njombe FC ya Mkoa mpya wa Njombe, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.

Wakati mchezo huo ukiendelea, wandishi wa habari kama ilivyo kawaida yao walifika uwanjani hapo kutekeleza wajibu wao wa kuchukua habari na kuuhabarisha umma wa watanzania.
Wakati wa mapumziko ulipofika, wachezaji wa Timu ya Kimondo FC waliingia kwenye chumba chao cha kubadilishia nguo, lakini wachezaji wa timu ya Njombe FC hawakwenda kwenye chumba chao cha kubadilishia nguo na badala yake walibakia uwanjani na kwenda kukaa mahali lilipokuwa benchi la ufundi la timu hiyo.

Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira Rashid Mkwinda ambaye pia ni mwanachama wa Chama cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya alikwenda kuwapiga picha wachezaji hao ambao kwa wakati huo walikuwa pamoja na viongozi wa timu hiyo.
Kitendo hicho kilisababisha golikipa wa timu ya Njombe FC, Joshua Mwampegeje kuanza kumtolea matusi mwandishi huyo, huku wachezaji wengine pamoja na viongozi wao wakimfuata na kuanza kumpiga, kumjeruhi, kusababishia uvimbe na maumivu mwilini na kumvunjia kamera yake wakati akitimiza wajibu wake.

Mashabiki wa Njombe FC waliokuwa Jukwaani walipoona vurugu hizo nao waliingia uwanjani na kushirikiana na viongozi na wachezaji wa timu yao kumpiga mwandishi na kumjeruhi.
Tukio hilo lilikuwa likishuhudiwa na viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA) ambao walikuwa wamekaa kwenye jukwaa kuu wakishuhudia kila kitu kilichokuwa kikiendelea uwanjani hapo bila ya kuchukua hatua yoyote.

Aidha wachezaji hao walifanikiwa kumpiga, kumjeruhi na kumvunjia kamera mwandishi huyo kutokana na kutokuwepo kwa ulinzi wa aina yoyote uwanjani hapo, hali ambayo pia ilisababisha mashabiki kuingia kirahisi uwanjani na kuongeza ukubwa wa vurugu.
Kutokana na kitendo hicho, Chama cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya kinalaani vikali kitendo cha mwandishi Rashid Mkwinda kupigwa, kujeruhiwa na kuharibiwa zana zake za kazi wakati akitimiza wajibu wake, kikiamini kuwa kitendo hicho hakikuwa cha kistaarabu hata kidogo, kwani ni ukiukwaji mkubwa haki za binadamu na uvunjaji wa Uhuru wa vyombo vya habari nchini.

Hivyo basi, Chama cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya kinakitaka Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya kutoa tamko kuhusiana na tukio hilo, kikielezea hatua zilizochukuliwa kuiadhibu timu ya Njombe FC kwa kitendo cha kumpiga mwandishi wa habari.

Chama cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya pia kinalitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuchukua hatua kwa mujibu wa kanuni na sheria za soka nchini dhidi ya wahusika ili kuhakikisha matukio ya aina hiyo hayajirudii mahali popote nchini.

Chama cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya kinajiuliza sababu za mchezo huo kufanyika bila ya kuwepo kwa ulinzi wa aina yoyote uwanjani hapo, kwani tunaamini kuwa mchezo huo ulistahili kupewa ulinzi wa Polisi kwa mujibu wa sheria za nchi, kwa sababu huwenda uwepo wa ulinzi uwanjani hapo ungepunguza ukubwa na athari za vurugu hizo.

Nakala kwa:
1.       Umoja wa Club Tanzania (UTPC)
2.       Baraza la Habari Tanzania (MCT)
3.       Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
4.       Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA)
5.       Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya
6.       Njombe FC
7.       Kimondo FC
8.       Vilabu vya Wandishi wa Habari vya Mikoa yote Tanzania
9.       Vyombo vya Habari

............................................................................................................

Serikali kuzichukulia hatua kali halmashauri zisizotekeleza miradi ya maji

Na Gladness Mushi,Arusha
SERIKALI  imeziagiza  halimashauri zote nchini  kuhakikisha zinakamiliza utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya miradi ya maji katika vijiji vitano ifikapo septemba  mwaka huu,na kwamba haitavumilia visingizio vya aina yoyote kwa halmashauri ambayo haitakuwa imekamiliza  ujenzi wa miradi hiyo.
Kauli hiyo imetolewa mapema leo na waziri mkuu,Mizengo Pinda alipokuwa akifungua mkutano wa mwaka wa kujadili utekelezaji wa miradi ya maji vijijini unaofanyoka kwa siku tano jijini Arusha,ambapo zaidi ya
washiriki 500 kutoka sekta mbalimbali za  maji wamehudhulia.
Waziri Pinda alisema kuwa serikali haitasita kuchukua  hatua kali kwa wahandisi wa maji wa wilaya ambao hadi kufikia muda huo watakuwa hawajakamilisha  ujenzi wa miradi yote kwani hadi sasa halmashauri
zote zimeshapokea fedha zinazotesheleza ujenzi wa miradi yote mitano.
Hata hivyo alisema kwa kipindi cha miaka mitatu 2013-2016 serikali katika sekretarieti ya maji mapango huo unalenga kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji kwenye maeneo ya vijijini ,huku akisema hali hiyo ni kutokana na asilimia kubwa ya wananchi waishio vijijini  hawapati huduma ya maji ipasavyo kutokana na miradi mingi kuchakaa bila kukamilika kutokana na usiomamizi duni wa watendaji.
Awali akimkaribisha waziri mkuu, waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe alisema katika mwaka 2013-2014 serikali imepanga kutekeleza miradi 1000 ya ujenzi wa  maji  mjini na vijijini utakao wanafaisha watu laki
8.7 kwa nchi nzima.
Aidha alisema  utekelezaji wa mpango huo unalenga kutekeleza mpango wa milennia ifikapo 2020 ili kuwanufaisha wananchi walio wengi hususani waishio vijijini  na kuwafikia kwa asilimia  62 ifikapo mwaka 2014.
.................................................................................................................................................................

HATIMAYE MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI ABSALOM KIBANDA AREJEA NCHINI


KIBANDA AKIONGEA NA WANAHABARI
........................................................................................................................................................
Post a Comment