Tuesday, June 25, 2013

DIWANI KATA YA KIWIRA WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA RAULENT ABEL MWAKALIBULE KWA TIKETI YA CHADEMA APANDISHWA KIZIMBANI MAHAKAMA YA WILAYA YA RUNGWE KWA TUHUMA KUSABABISHA WAFANYAKAZI WA SERIKALI ZA MITAA KATIKA KIJIJI CHA KIWIRA KUTOFANYA KAZI ZAO BAADA YA KUFUNGIWA OFISI TANGU TAREHE 20.06.2013 HADI SASA.


DIWANI WA KATA YA KIWIRA WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA RAILENT ABEL MWAKALIBULE AKITOKA MAHAKAMANI BAADA YA KUPEWA DHAMANA HADI TAREHE 25.07.2013 KESI ITAKAPOTAJWA TENA


DIWANI MWAKALIBULE AKIWA NA WANACHAMA WAKE WA CHADEMA WILAYA YA RUNGWE BAADA YA KUACHIWA HURU KWA DHAMANA

AKIONGEA NA MWANDISHI WA HABARI M WAKALIBULE AMESEMA KUWA VIONGOZI WALIOPEWA DHAMANA YA KUONGOZA WAJIFUNZE KUONGOZA WATU NA KUTATUA MIGOGORO YAO KWA WAKATI MUAFAKA KULIKO KUSUBIRI WANANCHI WANAPOHOJI NA KUCHUKUA HATUA ZAO WANANZOZIJUA,

 Kata ya Kiwira ni kata inayoongoza wilayani Rungwe kwa kuwa na mambo ya vurugu zisizokwisha tangu uchaguzi ufanyike baada ya kutokea kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo john mwankenja na uchaguzi ulipofanyika uchaguzi ulioipa chama cha Chadema ushindi

kushikiliwa kwa diwani Mwakalibule kumetokana na diwani huyo kwa kushirikiana na wananchi wake wachache kufunga ofisi ya kijiji kwa kumtuhumu mwenyekiti wa kijiji cha kiwira kutosoma mapato na matumizi kwa muda mlefu kitendo kilichopelekea mkuu wa wilaya Chrispin meela kuingilia kati.

kwakuwa mkuu wa wilaya yuko safari hadi sasa katika kikao kilichofanyika katika kijiji cha kiwira akatumwa mwakilishi wa mkuu wa wilaya ndipo kikundi cha watu wachache kikaibuka na kukaataa uwakilishi huo wa mkuu wa wilaya kwa sababu ya kuwa mgogoro huo una hadhi ya kuwepo mkuu wa wilaya na si mwakilishi wake, hivyo taarifa ya mapato na matumizi haikusomwa na ndipo mzozo ulipoanzia kuwa kwa nini mkuu wa wilaya amsimamishe kazi mwenyekiti kabla ya kusomwa mapato na matumizi?

Maazimio ya kikao baada ya kuvunjika yalikuwa moja kufunga ofisi ya kijiji mbili kikundi hicho kilitangaza kutotoa ushuru wa soko na magari eneo lote la kiwira kwahiyo tangu tarehe 20.06.2013 hadi sasa hakuna ushuru wowote unaokusanywa kiwira hivyo kupelekea Halmashauri ya wilaya kukosa mapato kutokana na soko lililopo eneo hilo.

baada ya kamati ya ulinzi na usalama kukaa tarehe 24.06.2013 na kumshirikisha Diwani wa kata ya kiwira  katika kikao hicho Diwani mwakalibule akakili kuwa yeye anazo funguo za ofisi hiyo ya kijiji ndipo kamati ya ulizi na usalama ikaamua kumpeleka polisi ili akatoe maelezo ya kina na ndipo diwani wa kata ya kiwira amefikishwa mahakamni kwa kosa la kuzuia watumishi wa serikali za mitaa katika kata ya kiwira kutofanya kazi zao baada ya kufungiwa ofisi. kesi itakayo tajwa tena tarehe 25.07.2013 baada ya upelelezi kukamilika.

 

 

.................................................................................................................................

Hali si Shwari Ndani ya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU).

 
 Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA Amani Simbeye akifungua mkutano kati ya waandishi wa Habari na Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU)
Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU)  wakifuatilia kwa umakini kikao  hicho wakati kikiendelea
  Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA Amani Simbeye pamoja na katibu wake wakisikiliza kwa umakini wahadhiri wakichangia hoja
  Mmoja wa Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) , akikazia jambo  ya yale ambayo yalikuwa yamezungumzwa
 Mmoja wa Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU), akitila  mkazo na kujibu swali ambalo liliulizwa na mmoja wa waandishi wa Habari.
Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) wakipiga piga Meza kuashiria kuunga MKONO Hoja ilizo somwa.
 Kikao kikiwa kinafungwa kwa Sala
 Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU)  wakiwa wanaimba wimbo wa Solidarity 
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Dr. Daniel Mosses Akiwa anauficha Uso akihofia kupigwa picha na kuhojiwa na waandishi wa Habari kuhusiana na Mgogoro unao endelea  Chuoni hapo 

***************

HALI si Shwari  Ndani ya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) baada ya Uongozi wa Chama cha Wahadhili wa Chuo hicho (TEKUASA) na wanachama wake kutangaza mgomo wa kutotunga mitihani ya kufungia Mhula, Mitihani ambayo inatarajiwa kufanyika Julai Mosi Mwaka huu kwa kile walichodai Menejimenti ya Chuo kutotoa majibu ya matatizo yao.
Mgomo huo  umetangazwa leo na Kaimu Mwenyekiti wa Tekuasa Amani Simbeye katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Chuo hicho kilichopo  Block T kata ya Iyela Jiji na Mkoa wa Mbeya na kuhudhuriwa na zaidi ya Wahadhili 30.
Simbeye amesema kuna mambo mengi na changamoto za elimu inayotolewa Chuoni hapo ambazo Menejimenti ya Chuo inahusika moja kwa moja hivyo kuhatarisha mustakabali wa Elimu Nchini hususani inayotolewa Chuoni hapo ambapo ameongeza kuwa zaidi ya yote ni kukosa ushirikishwaji wa maamuzi yanayohusu Taaluma.
Kwa taarifa zaidi na madai ya Wahadhili hao hadi kupelekea kususia kutunga mitihani ya kumaliza muhula inatarajiwa kufanyika Julai Mosi Mwaka huu yameandikwa kwenye  barua hapo chini lakini habari kamili itawajia baadaye kwa Lugha ya Kiswahili endelea kuwa nasi.

.................................................................................................................................

WATU ZAIDI YA 10 WANUSURIKA KUFA KATIKA AJALI JIONI HII ENEO LA UYOLE MBEYA

PICHA ZOTE NA MICHAEL - UYOLE 
............................................................................................................................
 mandela 655d6
RAIS mstaafu wa Mandela Nelson Mandela, bado yuko hali mahututi ingawa madaktari wanadhibiti hali yake baada ya afya yake kuzorota mwishoni mwa wiki.
Taarifa kutoka ikulu ya rais zinasema kuwa Mandela angali yuko chini ya uchunguzi wa madaktari ambao wameweza kuidhibiti hali yake.
 Anaugua maradhi ya mapafu na amelazwa hospitalini kwa zaidi ya wiki mbili sasa.
Mapema leo familia yake ilimtembelea hospitalini, mzee Mandela ambaye anasifika kwa vita alivyopigana dhidi ya utawala wa wazungu nchini Afrika Kusini.
Amekuwa akiugua ugonjwa wa mapafu mara kwa mara na hii ni mara ya tatu kwa Mandela kulazwa hospitalini mwaka huu.
Rafiki na jamaa wameendelea kukusanyika katika hospitali alikolazwa Mandela mjini Pretoria kumtakia afya njema mzee Mandela.
Mmoja wa waliomtembelea Mandela , mfanyabiashara Calvin Hugo, aliawachilia huru njiwa weupe, kama heshima yake kwa Mandela anaeyendelea kuugua hospitalini.
Alisema kitendo chake kilikuwa ishara ya, hatua ya Mandela kuikwamua nchi ya Afrika Kusini kutoka kwa mkoloni.
Baadhi ya jamaa zake wamekusanyika nyumbani kijijini eneo la Qunu, kujadili kile wanachosema ni habari muhimu sana. Chanzo: bbcswahili
.......................................................................................................................................................

JE, Mwizi au Mtuhumiwa wa Wizi?


untitled 6f71c

 ..............................................................................................................................................

No comments: