Wednesday, June 26, 2013

SINTOFAHAMU YA HALI TETE KATIKA CHUO KIKUU CHA TEOFELO KISANJI, UONGOZI WA CHUO NAO WATOA TAMKO .


Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji Dk.Daniel Mosses akisoma Tamko kwa Waandishi wa Habari


 Waandishi wa Habari wakiwa nje ya ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo kwa zaidi ya Masaa Matatu
 Waandishi wa Habari wakimsikiliza Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji Dk.Daniel Mosses akisoma Tamko kwa Waandishi wa Habari
 
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofelo kisanji wakingoja kusikia Hatima yao


Hali bado ni tete katika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji baada ya siku moja kupita tangu Chama cha Wahadhili wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKUASA) kutangaza kutotunga mitihani ya kufungia Mhula, Uongozi wa Chuo wasimama na kukanusha Mgomo huo.
Akisoma Tamko la kukanusha uwepo wa Mgomo huo, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Daniel Mosses amesema Mitihani itafanyika kama ilivyopangwa kuanzia Julai Mosi Mwaka huu hadi Alhamisi ya Julai 11, Mwaka huu.
Hata hivyo Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA, Amani Sembeye,alivyopigiwa simu kuhusiana na maamuzi ya Menejiment amesema msimamo wao uko pale pale.

Ameongeza kuwa kama  kungekuwa na msimamo tofauti na walivyotoa kwa vyombo vya habari awali basi wangeitisha tena mkutano mwingine kwa ajili ya kubatilisha.
................................................................................................................... 

WIZARA YA NISHATI NA MADINI; TANGAZO KWA UMMA


3 e271e
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
TANGAZO
Ndugu Watanzania,Tujitokeze kumuunga mkono Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano utakaofanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 28 Juni, 2013 hadi 01 Julai, 2013 maarufu kama SMART PARTNERSHIP INTERNATIONAL DIALOGUE.Tuchangie hoja zitakazoleta mabadiliko na maendeleo ya taifa letu. Tafadhali jiandikishe kupitia tovuti ya www.globaldialogue2013.go.tz
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
24/06/2013
........................................................................................................................................
 

Mzee Mandela afanyiwa maombi maalum

mande a42d8
 
ASKOFU mkuu wa kanisa la kianglikana mjini Cape Town, Afrika Kusini, Thabo Makgoba, amejitolea kufanya maombi kwa niaba ya rais mstaafu Nelson Mandela ambaye anaugua sana hospitalini.
Kasisi huyo anamuombea Mandela aweze kupata nafuu na amewataka wananchi kumshukuru kwa yote aliyowafanyia.
Jamaa za Nelson Mandela wamekutana nyumbani kwake huko Kunu, huku hali yake ya afya ikizidi kudorora hospitalini, Pretoria.
Afya ya Bwana Mandela ilikuwa mbaya zaidi Jumapili.
Maombi hayo yalitolewa baada ya Askofuu huyo kumtembelea Mandela hospitalini ambako kiongozi huiyo wa zamani amekuwa akilazwa kwa wiki mbili na nusu zilizopita baada ya kuugua mapafu.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa wajukuu wa rais huyo wa zamani wa Afrika kusini wanakutana nyumbani kwake kijijini katika mkoa wa Eastern Cape province, ambako viongozi wa kitamaduni wamealikwa.
Halikopta ya jeshi kadhalika zilionekana zikipaa karibu nyumbani kwa mandela. Afisi ya Rais jacob Zuma ilitangaza jumapili kuwa hali ya mzee Mandela ya afya ilikuwa mbaya sana. Chanzo: bbcswahili

No comments: