Sunday, June 23, 2013

Maaskofu: Serikali isitumie nguvu kudhibiti vurugu

askofu1 e4304


Rais  Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza askofu Telesphori  Mkude wa jimbo katoliki Morogoro wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 25 ya Uaskofu  wake (Silver Jubilee)zilizofanyika katika viwanja vya St.Peters junior Seminary mjini  Morogoro leo.
8E9U6106 
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu Katoliki wakati wa maadhimisho ya Sherehe za Miaka 25(Silver jubilee) ya Uaskofu wa Askofu Telesphori  Mkude wa jimbo Katoliki Morogoro zilizofanyika katika Viwanja vya Seminary ya St.Peters mjini Morogoro leo(picha na Freddy Maro)

Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini wameitaka Serikali kutumia njia ya mazungumzo kumaliza migogoro, badala ya kutumia jazba na nguvu.
Vilevile, wamesema kuwa hawako tayari kukaa kimya huku wakiona amani na utulivu nchini ikivurugika, badala yake wataendelea kusema ili amani na utulivu viweze kurejea.

Kauli hiyo imekuja baada ya Rais Jakaya Kikwete, kuwataka maaskofu hao na viongozi wengine wa dini nchini kuendelea kuisaidia Serikali katika kuimarisha amani na upendo miongoni mwa wananchi.
Akizungumza wakati wa kuadhimisha Jubilee ya miaka 25 ya uaskofu wake kwenye sherehe zilizofanyika jana katika Seminari ya Mt Peter mjini Morogoro, Askofu wa Jimbo la Morogoro, Telesphor Mkude, alisema meza ya mazungumzo ni lazima itumike katika kuimalisha amani na upendo wa Watanzania badala ya kutumia jazba na nguvu.

Mkude alisema kwa hivi sasa kumeibuka mivutano ya kidini na kisiasa na kutoa mfano wa vurugu zilizoibuka wilayani Sengerema mkoani Mwanza juu ya nani ana haki ya kuchinja au kutokuchinja kati ya waumini wa madhehebu ya Kikristo na Waislamu.

Pia vurugu za mikutano ya kisiasa, makanisa kuchomwa, mapadri na watumishi wengine kuuawa na kuteswa, kutupwa kwa mabomu katika mikusanyiko ya watu ikiwamo makanisa na kwamba yote hayo yangeweza kumalizwa katika meza ya mazungumzo.

Vurugu kubwa zilitokea Jumamosi iliyopita mjini Arusha baada ya mtu ambaye bado hajajulikana, kutupa bomu katika mkutano wa Chadema wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika katika viwanja vya Soweto na kuua watu wawili na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa.

Mei 2, mwaka jana, Mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daud Mwangosi aliuawa kwa kulipuliwa na bomu na askari polisi katika vurugu zilizotokea katika eneo la Nyololo mkoani Iringa.
Februaria 18, mwaka huu, Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Minara Miwili, Mji Mkongwe, Zanzibar aliuawa kwa kupigwa risasi asubuhi wakati akienda kuendesha misa katika Kanisa la Mtakatifu Theresia eneo la Mtoni. Mtuhumiwa wa tukio hilo, Omar Musa Makame, anaendelea na kesi mahakamani kujibu tuhuma za mauaji.

Tukio lingine ni lile la watu wawili kuuawa na polisi mjini Songea, Februari 22, mwaka jana, wakati wakizuia maandamano ya wananchi wenye hasira kali waliokuwa wakipinga mauaji yanayohusishwa na imani za kishirikiana.

Hivi karibuni maaskofu hao walitoa tamko la kuitahadharisha Serikali, kudhibiti vurugu za kidini na kisiasa nchini.

Walionya kuwa iwapo vurugu hizo hazitadhibitiwa huenda nchi ikaingia katika machafuko.
Awali, jana Rais Kikwete akizungumza katika hafla hiyo licha ya kumpongeza Askofu Mkude kwa utumishi wake mwema wa miaka 25 ya uaskofu wake, lakini pia alimpongeza kwa kuwa na mchango katika jitihada za maendeleo zinazofanywa na Serikali.

Alisema Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro limekuwa msaada katika kuimarisha huduma za jamii ikiwamo sekta ya elimu na afya na kwamba baadhi ya zahanati na vituo vya afya vimejengwa na kupandishwa hadhi kama Hospitali ya Mt Kizito na Turiani.

Rais Kikwete aliongeza kuwa mbali ya askofu huyo kuisaidia Serikali katika nyanja hizo, pia amekuwa akiiunga mkono katika jitihada zake za kujenga amani na upendo miongoni mwa wananchi ili taifa liweze kuwa na raia wema.

Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, alimtaja Askofu Mkude kuwa ni kuhani asiyekuwa na mwanzo wala mwisho, kwa vile anashiriki katika ukuhani wa Yesu Kristo asiyekuwa na mwanzo wala mwisho.

Alisema mpaka kufikia umri huo katika utumishi wake amekutana na mambo mengi magumu, lakini kutokana na kumtegemea Mungu zaidi ameshinda na kwamba akawaomba waumini wa Kanisa Katoliki kuendelea kumwombea na kumpa ushirikiano ikiwa ni zawadi yao pekee .
Askofu Mkude aliteuliwa kuliongoza Jimbo Katoliki la Tanga mwaka 1988 na aliyekuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Paulo II (kwa sasa ni marehemu), mwenye heri na miaka mitano baadaye alihamishiwa katika Jimbo la Morogoro ambako amelitumikia kwa miaka 20 mpaka sasa. Chanzo: mwananchi

 ............................................................................................................................

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE PAMOJA NA FAMILIA YAKE WAHUDHURIA MAZISHI YA SARGENT DIRECTIVE CHRISTOPHER KYENDESYA

 Marehemu Sargent Detective Christopher Kyendesya enzi za uhai wake

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete Wa katikati akiwa na Mke wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kushoto pamoja na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Diwani Athumani wakiingia katika nyumba ya Mama wa Marehemu kwa ajili ya kuhani Msiba

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfariji na kumpa pole Mama wa Marehemu  aliye kuwa Mbunge wa viti Maalum Mstaafu Mama Kyendesya
 Mke wa Rais Mama Salma kikwete akiwapa pole ndugu jamaa na Marafiki
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa salamu zake za Pole kwa wafiwa pamoja  na neno la Faraja.


 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Muheshimiwa Abas Kandoro akitoa salamu za pole kwa Familia ya Marehemu Ndugu jamaa na Marafiki.
 Kamanda wa Polisi Mkoa Diwani akitoa Salamu za Pole kwa ndugu jamaa na Marafiki kwa Niaba ya Jeshi la Polisi.

 Msemaji Kutoka Jeshi la Polisi na aliye ongoza msafara wa kuuleta mwili wa Marehemu, akisoma Historia fupi ya Marehemu.
 Kaka wa Rais Kikwete   wa Pili kushoto akiwa katika Ibada ya Mazishi
Kutoka kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma kikwete, Mama wa Marehemu Muhemishimiwa Mbunge wa viti maalum mstaafu Mama Kyendesya, Mke wa Marehemu Christopher Kyendesya pamoja na ndugu
 Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Muheshimiwa Abas Kandoro, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani pamoja na Mkuu wa Usalama Mkoa wa Mbeya
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa Heshima za Mwisho katika Mwili wa Marehemu Sargent Detective Christopher Kyendesya
 Kaka wa Muheshimiwa Rais Jakaya Kikwete , akitoa salamu za mwisho katika  mwili wa Marehemu Sargent Detective Christopher Kyendesya
 Mama wa Marehemu Muheshimiwa Mbunge Mstaafu viti maalumu Mama  Kyendesya akitoa salamu za mwisho katika  mwili wa Marehemu Sargent Detective Christopher Kyendesya
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani akitoa salamu za mwisho katika  mwili wa Marehemu Sargent Detective Christopher Kyendesya
Wananchi mbalimbali wakiwa katika Mazishi ya Marehemu Sargent Detective Christopher Kyendesya.
 Kazi ya Mazishi ikiwa inaanza
 Salamu za Rambirambi zikitolewa kwa niaba ya Mbunge wa viti Maalum Dr. Mary Mwanjelwa
 Aliyekuwa Mratibu wa Shughuli ya Mazishi Bwana Mwakipesile akizungumza jambo
 Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha FFU wakifyatua risasi juu ikiwa ni Ishara ya Heshima katika Mazishi hayo
 Mchungaji wa Kanisa la Moraviani ushirika wa Itili akitoa Mbaraka wakati wa kumaliza ibada ya Mazishi

 Mke wa Marehemu Sargent Christopher Kyendesya akiweka Shada la Maua
 Mama wa Marehemu Sargent Christopher Kyendesya , Muheshimiwa Mbunge Mstaafu Mama Kyendesya akiweka Shada la maua katika Kaburi
 Mtoto wa Maremu  Erick akiweka shada la mauwa katika kaburi la Baba yake pia kwa niaba ya Pacha wake ambaye alichelewa Mazishi
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete Akiwa na Kaka wa Muheshimiwa wa Rais Jakaya Kikwete wakiweka Shada la Mauwa katika kaburi la Marehemu Sargent Detective  Christopher Kyendesya
 Muheshimiwa Mkuu wa Mkoa Abas Kandoro pamoja na Mkewe wakiweka Shada la Maua katika kaburi la Marehemu

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani  akiweka shada la maua katika kaburi la maremu kwa niaba ya Jeshi la Polisi

Afisa usalama wa Mkoa akiweka shada la maua katika Kaburi la Marehemu
 Ndugu Shitambala wa Pili kutoka Kushoto akiwa katika msiba
 Hawa ni vijana kutoka Sae ambao ndio waliochimba kaburi la Marehemu .

No comments: