Saturday, June 29, 2013

KWAYA YA VALVARY KKKT TUKUYU YAANDAA MKANDA WA VIDEO ALBAM YA PILI INAYOKUJA KWA JINA LA(NIMEBEBA )

ALBAMU HII INAYOANDALIWA ITAKUWA NA NYIMBO 9 NA INAKUJA NA KWA UJUMBE WA (NIMEBEBA)

KULIA BAADHI YA WALEZI WA KWAYA NA WANA KWAYA  YA CALVARY TUKUYU WAKIWA MBELE YA KANISA KUU LA KKKT TUKUYU
BAADHI YA WALEZI WA KWAYA YA CALVARY KKKT TUKUYU

KUANZIA KUSHOTO YUKO NISSA, KATIKATI CAROLINE KINGO NA MUSA


MARY  KINGO AKIIMBISHA KWAYA

KWAYA IKIWA KATIKA SAFU ZA MILIMA YA LIVINGSTON KATIKA MBUGA ZA KITULO WILAYA YA MAKETE MKOA WA IRINGA


KINGO AKIWA KAZINI

LUCAS MBOYA AKIWA KAZIN MKURUGENZI WA LTV

KWA KAZI NZURI NA UHAKIKA YA KUANDAA VIDEO DOCUMENTARY ZA KWAYA USISITE KUFANYA KAZI NASI LTV KWA MAWASILIANO PIGA (LUCAS MBOYA MKURUGENZI LTV 0713519162 AU KINGO 0752881456)

KWAYA IKIWA ARUSHA
MCHUNGAJI  CHIBONA WA KKKT USHARIKA WA TUKUYU AKIONGOZA WIMBO UNAOZUNGUMZIA SAFARI YA WANA ISRAEL


WAFUGAJI WAKAACHA MIFUGO YAO WAKAJUMUIKA KATIKA HUDUMA YA KUMSIFU MUNGU
KWAYA ILISAFIRI  KATIKA MKOA WA IRINGA, MOROGORO, NA KUMALIZIA KAZI YA KUAANDAA PICHA ZA VIDEO ARUSHA KATIKA USHARIKA WA KKKT  KIMANDORU
MWANAMPOTEVU

USINIPITE MWOKOZI
KINGO 0752881456
LUCAS 0713519162

...................................................................................................

Simulizi za Mzee Madiba; Mandela Bondia alipokutana na bondia…

2 1bd4f
Ndugu zangu,
Kuna simulizi nyingi za Mzee wetu Madiba. Hakika, Nelson Mandela hajawahi kuwa mpenda makuu.
Mzee Mandela yuko simple sana, ni tangu enzi za ujana wake. Lakini, kuna ambao hawajui kuwa Mandela anapenda sana mchezo wa ngumi, na kuwa , yeye mwenyewe aliwahi kuwa bondia.
Kuna wakati akiwa Ikulu kama Rais, Mandela alipata habari za bondia wa Afrika Kusini aliyetwaa taji la  kimataifa. Mandela alifurahishwa sana na habari hizo. Akataka ampongeze mwenyewe bondia  huyo.
Siku moja akiwa na wasaidizi wachache sana, Mandela alikwenda hadi nyumbani kwa bondia huyo. Alihakikisha kuwa
bundia huyo yuko nyumbani kwake. Alipofika, Mandela aliwaambia wasaidizi wake wakamwambie bondia huyo kuwa nje kuna mtu anayehoji ubingwa wake.  Wamwambie kuwa  mtu huyo ( Nelson Mandela) anadai kuwa yeye ndiye bingwa wa uzito huo katika Afrika Kusini ( Nelson Mandela!) Kwamba anataka mkutane mpange siku ya kupigana ili apatikane mshindi halali wa taji hilo.
Basi, bondia yule akapokea habari hizo na akatamani sana amwone huyo anayedai kuwa ana ubavu wa kupambana naye.
Alipotoka nje akakutana na Nelson Mandela akiwa amesimama getini na amekunja ngumi yake. Akatania; “ Nimekuja kwako tuzipige ili dunia imjue bingwa halisi!”
Ikawa ni furaha kubwa kwa bondia yule. Hakuamini macho yake. Kuwa Rais wan chi amekuja nyumbani kwake kumpongeza.  Kumpongeza kwa jambo kubwa alilolifanya kwa taifa la Afrika Kusini. 
Na Mandela akawa tayari kuingia nyumbani kwa bondia huyo na kunywa nae chai!
What a Great Leader Of Africa! Yes, Nelson Mandela!

Wengi wamtakia Mandela afya njemaak 0631aMAMIA ya watu wanaendelea kukusanyika nje ya hospitali alikolazwa Nelson Mandela mjini Pretoria Afrika Kusini. Inaarifiwa Mandela bado yuko hali mahututi.
Wamekuwa wakimuimbia nyimbo na kumuombea nje ya hospitali. Wengine wamekusanyika katika iliyokuwa makaazi ya Mandela mtaani Soweto.
Watu wana wasiwasi kuhusu hali y mandela lakini pia wanataka kuonyesha wanavyojivunia kiongozi wao ambaye wanamuona kama baba wa taifa lao.Watu wana wasiwasi kuhusu hali y mandela lakini pia wanataka kuonyesha wanavyojivunia kiongozi wao ambaye wanamuona kama baba wa taifa lao.

Rais Obama awasili Afrika kusini, kuzungumzia uchaguzi wa Zimbabwe

obama ef5a2
RAIS wa Marekani Barack Obama amewasili nchini Afrika kusini kuendelea na ziara yake ya nchi tatu katika bara la Afrika inayolenga kupanua uhusiano wa Marekani na bara hilo.

Ziara yake imekuja wakati kukiwa na wasiwasi wa afya ya kiongozi aliyepigania haki dhidi ya ubaguzi wa rangi, Nelson Mandela, ambaye yupo mahututi katika hospitali ya Pretoria.

Akizungumza na waandishi wa habari waliopanda ndege ya Rais ya Air Force One, Ijumaa bwana Obama alisema sio lazima kwake  kumtembelea bwana Mandela katika hali yake ya sasa.

Maafisa wa White House walisema Alhamis kuwa ziara ya aina hiyo wanaiachia jukumu familia ya Mandela.  Jumamosi Rais Obama anapanga kutembelea kisiwa cha Robben, gereza ambalo bwana Mandela alifungwa kwa miaka 27.
 
Rais Obama pia atakutana na kiongozi mwenzake wa Afrika Kusini, Jacob Zuma. Mshauri msaidizi wa usalama wa kitaifa nchini Marekani, Ben Rhodes aliiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba miongoni mwa masuala ambayo bwana Obama inaonekana atazungumzia ni suala la Zimbabwe ambayo inaelekea kufanya uchaguzi wa urais.

Rhodes alisema Marekani inataka kuona uchaguzi huru, sawa na wenye hadhi nchini Zimbabwe pamoja na nafasi ya uhuru wa vyombo vya habari na mambo mengine ya demokrasia nchini humo.
 
Marekani inamshutumu Rais Robert Mugabe kwa kutumia ukandamizaji na wizi kushinda uchaguzi wa urais uliopita ikiwemo ghasia na mzozo kwenye vituo vya kupiga kura mwaka 2008.Chanzo: voaswahili
Post a Comment