Thursday, June 20, 2013

WATU watatu wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kutenda kosa la kumuua kwa kukusudia aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha kuweka na Kukopa (Saccoss), Mbeya

Jailo Rashid (30), Niza Hamis (24) na Medi Keya(33) ambao kwa pamoja wanadhaniwa kumuua kwa maksudi, Ambrose Shayo(45) aliyekuwa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Saccos Taifa na Tazara Saccos ya Jijini Mbeya.
Hili ndilo eneo alilouwawa mwenyekiti huyo wa saccos



WATU watatu wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kutenda kosa la kumuua kwa kukusudia aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha kuweka na Kukopa (Saccoss), Mbeya
Akisoma mashtaka hayo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali Hebel Kihaka mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya Venance Mlingi alidai Watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa la mauaji kwa maksudi kinyume cha Sheria ya Makosa ya Jinai kifungu cha 196 sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Jailo Rashid (30), Niza Hamis (24) na Medi Keya(33) ambao kwa pamoja walimuua kwa maksudi, Ambrose Shayo(45) aliyekuwa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Saccos Taifa na Tazara Saccos ya Jijini Mbeya.
Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo  April 20, Mwaka huu majira ya saa 3 usiku katika Kijiji cha Itagano Kawatere Jijini Mbeya ambapo Marehemu alivamiwa na watu hao kisha kumuua.
Kwa upande wake Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Venance Mlingi alisema Kwa mujibu wa Sheria watuhumiwa hawaruhusiwi kujibu chochote kutokana na Mahakama yake kutokuwa na uwezo wa kusikiliza Shauri la Mauaji.
  
Aliongeza kuwa Shauri hilo limeletwa kwa ajili ya hatua za awali ambapo baada ya upelelezi kukamilika litapelekwa Mahakama kuu kwa ajili ya taratibu za kusikiliza, pia aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 3, Mwaka huu itakapotajwa tena.

Na Mbeya yetu

 .................................................................................................................................

AHUKUMIWA MIAKA 30 BAADA YA KUKIRI KUMPORA ASKARI MAGEREZA BUNDUKI

 Ali Salum (32) ambaye ni mshtakiwa namba moja amekiri kosa lake la kupokonya siraha na amehukumiwa kutumikia kifungo kwa miaka 30
Braison Sanga yeye ni mtuhumiwa wa 3 baada ya kuona mwenzake amefungwa miaka 30 nae akaamua kukiri kosa lake kuwa yeye ndiye aliekuwa napanga wakati wa kupokonya siraha hiyo
Hili ndilo panga lililotumika kumkata askari magereza wakati wa kumpokonya siraha yake
Hii ndiyo siraha aliopokonywa askari huyo watuhumiwa waliifunga kwenye mkeka
askari WDR Ambrose akitinga mahakani kusikiliza hukumu ya watuhumiwa wake

Watu wanne  wamefikishwa Mahakamani wakituhumiwa kutenda kosa la kufanya unyang’anyi wa kutumia Silaha kwa kumpora Askari Magereza Bunduki na hukumu ikitolewa kwa Mshtakiwa mmoja ambaye amehukumiwa miaka 30 jela.
  
Mwendesha Mashtaka wa Serikali Mwajabu Tengeneza akisoma Mashtaka Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya Aneth Nyenyema amesema Washtakiwa wote wanne  kwa pamoja walitenda kosa hilo kinyume cha Sheria ya kanuni ya adhabu kifungu cha 287(A) sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
  
Amewataja watuhumiwa kuwa ni Ali Salum (32) ambaye ni mshtakiwa namba moja akiwa na Emmanuel Martin(25), Braison Sanga na John Waziri(22) ambao ilidaiwa kuwa Mei 5, Mwaka katika eneo la Magereza Songwe walimvizia askari WDR Ambrose na kumjeruhi kisha kumpokonya bunduki aina ya SRA yenye namba za usajili TZ PS 39847164020 mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kitengo cha Jeshi la Magereza.
  
Kutokana na Mashtaka hayo watuhumiwa wote walikana isipokuwa Mshtakiwa namba moja ambaye alikubali kutenda kosa hilo hali iliyomlazimu Mwendesha mashtaka kumsomea mara tatu ili kujua kama ameelewa mashtaka yake.
...............................................................................................................................

JESHI la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Mwalimu wa Masomo ya Ziada akituhumiwa kumbaka Mwanafunzi wa darasa la nne mwenye umri wa miaka 10.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athmani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba lilitokea juzi hivi karibuni katika kijiji cha Itunge wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya.

JESHI la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Mwalimu wa Masomo ya Ziada akituhumiwa kumbaka Mwanafunzi wa darasa la nne mwenye umri wa miaka 10.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athmani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba lilitokea Hivi karibunikatika kijiji cha Itunge wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya.
 
Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Ipyana Gidion(30),kyusa,mkulima mwalimu wa masomo ya ziada (tuition) katika kituo cha Itunge Moravian   mtaa wa Mbugani Wilayani Kyela Mkoani hapa.
 
Alisema Mtuhumiwa huyo alimbaka mtoto mwenye umri wa  miaka 10, kyusa,mwanafunzi  darasa  la  nne  katika Shule ya msingi Mbugani mkazi wa Itunge “a” na kumsababishia maumivu makali mwilini.
 
Kamanda Diwani alisema  mbinu iliyotumika ni kuwaruhusu wanafunzi aliokuwa akiwafundisha  kuondoka na kubaki na mhanga kisha kumbaka katika chumba anachotumia kufundishia (darasani).
 
Aliongeza kuwa  mtuhumiwa  aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kosa la kubaka na kutoka kwa rufaa na kwamba mhanga amepatiwa matibabu na kuruhusiwa ambapo taratibu zinafanywa ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani.
............................................................................................................................
 
ajali 14f54

No comments: