MAHAKAMANI LEO
MCHUNGAJI
wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini
Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa mahakamani kungojea kesi yake.
Wananchi Mbalimbali wakisubiri Kusikiliza Kesi ya MCHUNGAJI
wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini
Mbeya Daniel Mwasumbi
MCHUNGAJI
wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini
Mbeya Daniel Mwasumbi aliye vaa koti Jeupe akiwa anatolewa mahakamani Baada ya kusomewa kifungo cha Miaka 30 Jela
Watoto wa MCHUNGAJI
wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini
Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa wanatoka Mahakamani Baada ya Baba yao kusomewa kifungo
Mtoto wa MCHUNGAJI
wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini
Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa anaongeaa na waandishi wa Habari baada ya kesi kumalizika
Waumini Mbalimbali wakiwa nje Baada ya kesi kumalizika
Binti anaye daiwa kufanyiwa kitendo hicho akilia kwa Uchungu baada ya kesi kwisha
***********
MCHUNGAJI
wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini
Mbeya Daniel Mwasumbi amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 baada
ya kukutwa na makosa mawili ya Kubaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa miaka 19.
Akisoma
hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Mbeya Ndugu Gilbert Ndeuruo amesema
Mahakama imemta hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na Shahidi namba moja
katika kesi hiyo ambaye ni mhanga wa tukio hilo Neema Beni(19).
Amesema
Mtuhumiwa huyo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mwezi Januari 2008 hadi
Mwaka 2011 katika eneo la Iwambi kinyume na Sheria kifungu cha 130(2)e na 131
(1) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwa kosa la ubakaji.
Kutokana
na ushahidi huo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mahakama yake imemkuta Mtuhumiwa na
makosa mawili ya Ubakaji na kumpa ujauzito kwa ushahidi uliotolewa na Mhanga
mwenyewe pamoja na Mwalimu wa Shule aliyokuwa akisoma ambapo alidai kuwa Shtaka
limedhihirishwa pasipo shaka chini ya kifungu cha 235/1985.
Kwa
upande wake Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa aliiomba Mahakama
hiyo kutoa adhabu kali kutokana nan mtuhumiwa kutenda kosa la kinyama tofauti
na umri wake na wa binti ambapo Binti anaumri wa Miaka 19 ili hali Mtuihumiwa
akiwa na Miaka 57.
Pia
alidai kuwa Mtuhumiwa huyo alimwalibia masomo na maisha yake binti huyo na
vitendo hivyo alikuwa akivifanyia sehemu mbali mbali ikiwemo kanisani hivyo
aliiomba mahakama hiyo kuvitaifisha na kutoa amri ya Matunzo ya Watoto kwa
kutumia amri ya kutaifisha malishtakiwa.
Hata
hivyo Hakimu alimuuliza Mtuhumiwa kupunguziwa adhabu ambapo Mshtakiwa huyo
aliomba kupunguziwa adhabu kwa madi kuwa ameachiwa watoto na ndugu zake
aliozaliwa nao wakiwemo wazazi wake hivyo akifungwa hawatakuwa na msaada.
Aidha
kutokana na utetezi huo Hakimu Ndeuruo alimhukumu kifungo c ha Miaka 30 na
viboko 12 kutokana na kosa la kwanza ili hali katika kosa la pili amehukumiwa
kifungo cha Miaka 5 na kuongeza kuwa adhabu hizo zitaenda kwa pamoja na kulipa
fidia ya Shilingi Milion 20 kwa fedha za Tanzania kwa familia ya Mhanga.
Ameongeza
kuwa Mtuhumiwa anahaki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu ya Mbeya kama
hatakuwa ameridhika na adhabu aliyopewa na mahakama yake.
,Picha na Mbeya yetu
...................................................................................................................
Obama arejea Marekani
Gari lililombeba Rais Obama likielekea Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere baada ya kumaliza ziara yake.
Rais Obama na mkewe michelle Obama wakipunga mikono kbla ya kuanza safari
Gari lililombeba Rais Obama likielekea Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere baada ya kumaliza ziara yake.
Msafala wa Rais obama ukipita maeneo ya buguruni kuelekea uwanja wa ndege
|
.............................................................................
MAMA MICHELLE OBAMA ATEMBELEA WAMA FOUNDATION NA KUKUTANA NA MAMA SALMA KIKWETE JIONI HII
Mke wa Rais wa Markani mama Michelle Barack Obama akiwasili katika ofisi za Wanawake na Maendeleo WAMA jioni hii wakati alipotembelea katika ofisi hiyo na kuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete katika makao makuu ya taaisis hiyo leo, Rais Barack Obama na Mke wake Michelle Obama wako katika ziara ya siku mbili ya kikazi nchini Tanzania wakiongozana na watoto wao jioni hii Rais Barack Obama atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete na pia watazungumza na waandishi wa habari Ikulu kabla ya kuendelea na kazi zingine
Mama Michelle Obama akilakiwa na mwenyeji wake mama Salma Kikwete wakati alipowasili katika ofisi hizo kwa mazungumzo mafupi.
Mama Michelle Obama akipozi kwa picha na mwenyeji wake mama Salma Kikwete
Wake wa viongozi wakipunga bendera kama ishara ya kumpokea Mama Michelle Obama
Mama Anna Mkapa ambaye pia ni mwenyekiti wa taasisi ya EPTF akiongozana na mama Aisha Bilal wakati wa mapokezi ya Mke wa Rais Barack Obama Mama Michelle Obama katika ofisi za WAMA jioni hii
.............................................................
Mapokezi ya obama Ikulu jijini Dar es salaam
Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle Obama akipokewa kwa Shangwe Ikulu, Dar es salaam
No comments:
Post a Comment