Wednesday, July 3, 2013

WATU KADHAA WASHIKIRIWA NA POLISI BAADA YA KUHAMASISHA WANANCHI WA KIWIRA WILAYANI RUNGWE KUKATAA KULIPA USHURU WA SOKO KWA HALMASHAURI YA RUNGWE NA HII IKIWA NI TAMKO LA SERA YA CHAMA CHA CHADEMA KIPINDI CHA UCHAGUZI WA DIWANI KATIKA KATA HIYO ULIOPELEKEA CHADEMA KUIBUKA KIDEDEA, KUKAMATWA KWA WATU HAO KUMEPELEKEA WATU WACHACHE KUHAMASISHANA KUFUNGA BARABARA NA KULETA USUMBUFU KWA WASAFIRI WANAOTUMIA BARABARA YA KYELA MBEYA

SOKO LILILOJENGWA NA HALMASHAURI YA RUNGWE KATIKA KATA YA KIWIRA IKIWA NDIO CHANZO CHA VURUGU KWA BAADHI YA WATU MAARUFU WANAO FADHIRI VIJANA KUFANYA VURUGU  KUPITIA DIWANI WAO WA CHADEMA KUHAMASISHA WATU KUKATAA KULIPA USHURU WA SOKO
DIWANI  WA KIWIRA KWA TIKETI YA CHADEMA RAULENTMWAKALIBULE SIKU ALIPOKUWA AKITOKA MAHAKAMANI KWA DHAMANA BAADA YA KUSOMEWA SHITAKA LA KUSABABISHA WATUMISHI WA HALMASHAURI KUTOFANYA KAZI BAADA YA KUWAFUNGIA OFISIN NA KUSABABISHA KUSIMAMA KWA SHUGHURI ZA SERIKALI

MARABARA HII NI YA KIMATAIFA IKIUNGANISHA NCHI ZA KUSINI MWA TANZANIA KWA KUPITIA NCHI YA MALAWI  NA NDIO TEGEMEO LA WATU KIUCHUMI SASA VIJANA WA KIWILA WAKIWA NA MATATIZO YAO NA UONGOZI WAO WALIOUCHAGUA WENYEWE WAO WANAKIMBILIA KUFANYA VURUGU KATIKA BARABARA HII NA KUICHOMA MOTO NA KUWEKA MAWE


UMOJA WA WAENDESHA BODABODA KIWIRA WASIKIKA WAKISEMA WAMECHOSHWA KUBULUZWA KUFANYA VURUGU KITENDO KINACHOWAFANYA KUCHUKIWA NA WENGI NA KUTOFANYA BIASHARA HIVYO WAMEWATAKA WANAOFANYA VURUGU HIZI KUKAA MEZANI NA KUTATUA MATATIZO YAO NA SIO KUFUNGA BARABARA


ASKALI POLISI WA TUKUYU NA VIJANA WAZALENDO WAKASHIRIKIANA KUONDOA VIZUIZI VYA MAWE BARABARANI

WAKISUBIEI AMRI TU YA KIONGOZI WAO


MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA LEO AMEFIKA WILAYA RUNGWE AKITOKEA MOROGORO KIKAZI NA AMEAHIDI KUFIKA KATIKA KATA YA KIWIRA KUONGEA NA WANANCHI ILI KULIPATIA UFUMBUZI WA SUALA HILI LA WATU KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA KUFUNGA OFISI YA SERIKALI NA KUFUNGA BARABARA JAMBO LINALOLETA USUMBUFU KWA WANANCHI WANAOTUMIA BARABARA HII YA KYELA MBEYA.

 ...............................................................................................................................................................
MGOGORO WA USHURU WA NYAMA  WILAYANI RUNGWE WATINGA OFISIN KWA MKUU WA WILAYA IKIWA NI SIKU YA TATU BUCHA ZA NYAMA ZIMEFUNGWA BAADA YA WAFANYA BIASHARA YA NYAMA KUGOMA BAADA YA KUAZIA TAREHE MOJA KUPANDA KWA USHURU KUTOKA SH 1000/= YA AWALI NA KUFIKIA 4500/=
MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AKIONGEA NA WAFANYA BIASHARA WA MABUCHA YA NYAMA NA WATENDAJI WA HALMASHAURI YA RUNGWE NA  KUFIKIA MWAFAKA WA KUANZA KUUZA NYAMA PIA KUTOA USHURU WA SH 3000/= BADALA YA 4500/=

KATIKA MWAFAKA HUU WA KUANZA KUUZA NYAMA NA KUTOA USHURU WA SH 3000/= WILAYANI RUNGWE KIKAO KIMEWASHIRIKISA WATENDAJI WA HALMASHAURI YA RUNGWE NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI PAMOJA NA WAFANYA BIASHARA YA NYAMA WILAYANI RUNGWE


MGOGORO HUU UMETOKANA NA WAFANYA BIASHARA KUTOKUBARI SHERIA YA HALMASHAURI KULIPA GHARAMA YA KILO MOJA KWA MFUGO UNAOUZWA HIVYO KWAKUWA GHARAMA YA KILO MOJA YA NYAMA SASA NI SH 4500/= HIVYO YAPASA KULIPA KIASAI HICHO. NA HII SHERIA IMEKUWEPO BILA YA KUREKEBISHWA KWA MUDA SASA MAANA TANGU GHARAMA ZA KILO YA NYAMA SH 1000 HADI SASA IPO HIVYO ILA WATENDAJI KWA KUTOKUWA MAKINI KILA KILO YA NYAMA ILIPOPANDA WALIKUWA HAWACHUKUI USHURU WA KILO YA NYAMA

 BAADA YA MWAFAKA HUU KUPATIKANA WAFANYA BIASHARA SAIZI WAKO MACHINJIONI NA BAADA YA MUDA NYAMA ITAPATIKANA KWA WAKAZI WA WILAYA YA RUNGWE BAADA YA SIKU TATU KUTOPATIKANA KWA NYAMA MABUCHANI

........................................................................................................

KIJANA APANIA KUUA BABA YAKE MZAZI, DADA NA MKEWE



 Polisi Mbeya wakipambana kwa mikono na Lusajo Kabuje mkazi wa Iwindi Mbeya Vijijini baada ya Bunduki kugoma kufanya kazi ambapo mmoja wa askari alipata majeraha ya visu alivyokuwa navyo mtuhumiwa kabla hajadhibitiwa.
 Baba mzazi wa mtuhumiwa. mzee Emmanuel Kabuje ambaye pia alikusudiwa kuuawa na kijana wake, akizungumza na kalulunga blog eneo la tukio muda mfupi baada ya mwanae kukamatwa na polisi.
 Ujumbe aliouandika kijana Lusajo kabla hajatimiza adhima yake ya kufanya mauaji ya kutisha kwa mkewe, Baba yake mzazi, Dada yake na kisha kujiuua yeye mwenyewe.
 Makazi ya mtuhumiwa
 Wananchi wakishangaa baada ya kukamatwa mtuhumiwa huyo
 Jeneza likiwa ndani katika nyumba ya mtuhumiwa
 Polisi wakiwa wamemdhibiti mtuhumiwa Lusajo Kabuje eneo la Isanga kijiji cha Iwindi wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya leo Julai 2, 2013.

 Kulia ni askari kanzu akiwa na moja ya kisu alichotaka mtuhumiwa kumchoma askari huyo kifuani kabla ya kudhibitiwa ambapo askari huyo alilazimika kukidaka kisu hicho kwa kushika sehemu ya makali.
 Mke wa mtuhumiwa. Oliver Mwaluanda akizungumza  baada ya kujitokeza kutoka mafichoni baada ya mumewe kukamatwa na polisi. Oliver akisema kuwa aliruka ukuta huku akiwa na mtoto mgongoni kwa ajili ya kunusuru maisha yake baada ya kuona mumewe anataka kumuua kikatili.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Iwindi wakitoa jeneza ndani kwa Lusajo Kabuje na kwenda kulipakia kwenye gari la polisi ambapo mtuhumiwa alipoambiwa alale ndani ya jeneza hilo alikataa huku akisema kuwa anaogopa...

KIJANA Lusajo Kabuje mkazi wa kitongoji cha Isanga kijiji cha Iwindi wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani hapa, amekamatwa na polisi kabla ya kutekeleza mpango wake wa kufanya mauaji ya kutisha kwa ndugu zake.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa na polisi majira ya saa 11;24 jioni eneo la klabu ya pombe ya Isanga Julai 2, mwaka huu huku akiwa na visu viwili ambavyo alikusudia kufanyia unyama huo huku akiwajeruhi polisi waliofika kumkamata kabla hajatekeleza adhima yake hiyo ovu.


Kabla ya kukamatwa, mtuhumkiwa alitaka kumchoma kisu kifuani mmoja wa askari nwaliofika eneo hilo ambapo askari huyo aliyekuwa amevaa nguo za kiraia alifanikiwa kukwepa na kukamata kisu hicho sehemu ya ncha kali huku askari aliyeshika bunduki, risasi zikiwa zinagoma kuingia kwenye Magazine ili kufyatua risasi juu.


Baada ya kumkamata na kumvisha pingu, askari polisi walifika nyumbani kwake na kukuta jeneza, mslaba, katoni ya chumvi na mafuta ya kupikia ambavyo vyote aliviandaa kwa ajili ya mazishi yake, mkewe, Baba yake mzazi na Dada yake.


Baba mzazi wa Lugano, Emmanuel Kabuje, alimwambia mwandihi wa habari hizi kuwa kijana wake hajawahi kuwa na matatizo ya akili lakini Juni 28, mwaka huu alimtishia kumuua kwa kumkatakata vipande.

‘’Hajawahi kuugua ugonjwa wa akili lakini tarehe 28, mwezi wa sita alinitishia kuniua ndipo nikaenda kutoa taarifa kituo cha polisi Mbalizi’’ alisema Kabunje.


Mke wa mtuhumiwa asema aliruka ukuta kujiokoa

Mke wa mtuhumiwa huyo Oliver Mwaluanda, alijitokeza na watoto wake watatu kutoka mafichoni ambako walishinda na njaa kutoka majira ya saa tisa alasiri.

Baada ya mumewe kukamatwa na polisi, Oliver alijitokeza mbele ya umati wa wananci na kuwashukuru kufanikiwa mumewe kukamatwa kabla hajatekeleza adhima yake ya kumuua yeye, wifi yake, Baba Mukwe na mtuhumiwa mwenyewe.


‘’Alikuwa akinipiga mara kadhaa na aliyekuwa akiniokoa ni Baba mukwe na ndiyo chanzo cha kumchukia na aliahidi kuniua kwa kutumia shoka, muache aende labda leo na watoto wangu tutaweza hata kula chakua kwa uhuru’’ alisema Oliver huku akiwa na watoto wake wakitetemeka kwa baridi baada ya kutoka mafichoni.

Alisema kuwa, mchana alifika nyumbani hapo na kumwambia kwa yeye si binadamu wa kawaida bali siku hiyo atakufa na kufanya mauaji mengine kabla yeye hajajiua ambapo naliahidi kumuua dada yake aitwaye Mariam Kabuje.

Alipoulizwa matatizo ya mumewe anayoyafahamu, alisema kuwa hakuwa na matatizo ya akili bali tatizo lake alikuwa akinywa sana pombe aina za viroba ambazo anahisi kuwa zilichangia kufikia hatua hiyo ya kutaka kuchukua maamuzi ya kufanya mauaji.

Baadhi ya wananchi wanaoifahamu familia hiyo, walisema kuwa mzee Kabuje alipewa taraka na mkewe miaka mingi hali iliyompelekea kukataa kuoa mke mwingine akiwahofia watoto wake kuteswa na mama wa kambo na kufanya jitihada za kuwasomesha watoto wake wote ambapo baadhi ni wafanyabiashara na mmoja yupo chuo kikuu.

No comments: