Wednesday, July 3, 2013

T.MARC WAENDESHA MAFUNZO NA KUPIMA KWA HIYARI UKIMWI KATIKA VIWANJA VYA SOKO JIPYA LA MACHINGA NA STANDI YA DALADALA ZAMANI KAMA CCM TUKUYU MJINI WILAYANI RUNGWE

LEO TUKUYU NA MUONEKANO WA HALI YA HEWA PIA NDIO MUONEKANO WA MLIMA ULIO WATATU KWA UREFU TANZANIA MLIMA RUNGWE UNAOSABABISHA HARI YA HEWA KUWA SAFI NA MVUA ZA KUTOSHA PAMOJA NA VYAKULA VYA UHAKIKA KWA  MWAKA MZIMA

MR SERAPHINO SALEMA MFANYA KAZI WA T.MARRC AKIONGEA KINGOTANZANIA AMESEMA KUWA WATANZANIA SAS NI WAKATI WA KUAMKA KUPIMA AFYA ZAO ILI KUWA NA UHAKIKA WA KUISHI BILA YA KUWA NA WASIWASI PAMOJA NA KUJIKINGA NA KUMLIDA MWENZAKO NA MAAMBUKIZI YA MAGOJWA HUSUSANI UKIMWI AMBAO HADI SASA HAUNA TIBA WALA KINGA DUNIANI

KULIA KINGOTANZANIA AKIPATA MAELEKEZO JINSI T.MARC WANAVYOFANYA KAZI TANZANIA USUSANI MKOA WA MBEYA HIVYO MR SERAPHINO AMESEMA KUWA MKOA KWA TAKWIMU MKOA WA MBEYA NI WA TATU TANZANIA KWA KUWA NA MAAMBUKIZI MAKUBWA HIVYO KILA MTU ANATAKIWA KUGUSWA NA HAYA MAPAMBANO YA UKIMWI ILI KUFIKIA KILA MTU KUWA NA UELEWA WA JINSI YA KUJIKINGA NA UKIMWI NA KUMLINDA MWENZAKO

BAADHI YA WATEJA WAKIPATA HUDUMA HUKU MR SERAPHINO AKISEMA MUITIKIO WA WANAUME KUPIMA NI MKUBWA KULIKO MUITIKIO WA WANAWAKE UKIWA MDOGO NA CHANGAMOTO HII INATOKANA NA WANAWAKE WENGI KUTOJIAMINI NA KUOGOPA KUPIMA MCHANA NA MAHALI PEUPE HIVYO USHAURI MAHARI PENGI WATU WAMESHAURI T.MARC WAANZE KUWA NA MAFUNZO KWA NJIA YA SINEMA NYAKATI ZA USIKU ILI WANAOOGOPA MCHANA WAJITOKEZE WAKATI HUO WA USIKU ILI KUWA HURU KUPIMA AFYA ZAO

MMOJA WA WADADA WALIOJITOKEZA KUPIMA AFYA YAKE NA KUPATA MAELEKEZO JINSI YA KUTUMIA KINGA ILI KUJIKINGA NA UGONJWA WA UKIMWI NAYE AMEWASIHI WADADA WENZAKE KUJITOKEZA SEHEMU ZINAPOTOLEWA HUDUMA HIZI HATA KATIKA HOSPITAL KWA MAANA AFYA NDIO IPEWE KIPAUMBELE KWANZA

BAADA YA MASOMO KWA KINA NA KUPIMA PAMOJA NA KUPATA NASAHA T.MARC WANATOA ZAWADI KWA WALE WANAJITOKEZA KUSIKILIZA ELIMU HII YA KUPIMA VVU KWA HIYARI

BAADHI YA MABANDA YA KUPIMIA VVU  KATIKA UWANJA WA SIKO JIPYA LA MACHINGA TUKUYU MJINI ZAMANI MAARUFU KAMA CCM

SOKO LA MACHINGA TUKUYU MJINI

PAMOJA NA ELIMU ITOLEWAYO UWANJANI HAPO PIA KUNA BURUDANI IKIAMBATANA NA MAFUNDISHO YATOLEWAYO JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA UKIMWI NA KUJITOA KWA MOYO KUPIMA KWA HIYARI
................................................................................................................................................

MJENGWA;... 

Angalia Tofauti Hii KUBWA Kati Ya Marekani Na Tanzania...!

MJENGWA AKIWA NA MWANAFUNZI WAKE WA HABARI ZA MITANDAONI KINGOTANZANIA
00 ea7c2


Ndugu zangu,

Katika saa 20 na zaidi Rais Obama alipokuwa katika ardhi ya Tanzania, sikusikia mahali popote akitamka jina la chama chake cha Democrat. Obama ametamka ' AMERICA!' mara zisizohesabika.

Kwa kweli ujio wa Obama umetusaidia Watanzania kupumzika na kelele za vyama, maana, kwa siku kadhaa, kabla na wakati wa ujio wa Obama, Watanzania tumepata kupumzika na kusikia habari za
vyama vya siasa na malumbano yasio na hoja za msingi, mara nyingi yasio na tija kwa nchi na maendeleo yake.

Hakika, siasa ni kitu kizuri sana kwa nchi. Lakini siasa za ' ovyo ovyo' ni kitu kibaya kwa nchi. Na mara nyingi, siasa za ' ovyo ovyo' ni kitu cha hatari kwa nchi na mustakabali wake.

Picha hiyo hapo juu ina mengi ya kutufundisha; kuwa siasa si uhasama. Uchaguzi ukiisha watu mnarudi kwenye kufanya kazi. Kupigania maslahi ya taifa. Si kuendeleza migogoro ya kisiasa na hata kuwepo kwa vurugu. Hayo hayana tija kwa nchi.

Unapomwangalia Obama na Bush kwenye picha ya pamoja wakiwa Dar na kwenye kutoa heshima kwa wahanga wa ugaidi kwenye mlipuko ulitokea kwenye Ubalozi wao mwaka 1998, inadhihirisha ukomavu wa kisiasa.

Unachotumainia hapa, kuwa ifike siku, hata hapa kwetu Tanzania, kwa Rais aliye madarakani na Rais Mstaafu kutoka vyama viwili tofauti, tuone picha yao wakiwa wamesimama pamoja kwenye makaburi ya kumbukumbu ya mashujaa wetu wa Vita Vya Kagera kule Uganda.

Ndio, picha hiyo hapo juu ni somo kwetu. Hawa wawili; Bush na Obama, ndio tuliowaona kwenye kampeni zao wakipambana kiasi huwezi kufikiri wanaweza kusimama pamoja kama ndugu wa taifa moja.

Lakini, kwa wenzetu Marekani, siasa si uhasama wala mambo ya kuwindana. Wanachogombania kwenye siasa ni kupewa heshima ya kuitumikia Marekani.

Na heshima hiyo akipata mpinzani wako, basi, kwa wenzetu wanachofanya ni kuungana mkono kwenye kazi ya maslahi ya Marekani bila kujali tofauti zao za kiitikadi. Na ndicho tunachofundishwa kwenye picha hiyo.

Swali linabaki, Watanzania tuko tayari kubadilika kifikra kwa maslahi ya taifa letu?

Maggid,
Iringa.
0754 678 252
........................................................................................................................................................

No comments: