MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO AKIFUNGUA MKUTANO WA KAMATI YA USHAURI YA MKOA(RCC) JIJINI MBEYA
KATIBU TAWALA WA MKOA MARIAM MUTUNGUJA AKISOMA TAARIFA YA MKUTANO
NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI PHILIPO MULUGO AKICHANGIA JAMBO WAKATI WA KIKAO HICHO
MBUNGE WA MBOZI MASHARIKI NA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MBEYA GODFREY ZAMBI AKICHANGIA JAMBO KATIKA KIKAO HICHO
MKUU WA WILAYA WA MBEYA DR. NORMAN SIGARA AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO
MBUNGE WA VITI MAALUMU(CCM) MKOA WA MBEYA DR. MARY MWANJELWA AKICHANGIA JAMBO KATIKA MKUTANO HUO.
MEYA WA JIJI MBEYA ATANAS kAPUNGA AKICHANGIA JAMBO KATIKA MKUTANO HUO
MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CRISPIN MEELA AKICHANGIA HOJA
WAJUMBE WAKIWA WANAFUATILIA MKUTANO HUO
Songwe
ndilo jina lililopendekezwa kuitwa kwa Mkoa Mpya utakao gawanywa kutoka
Mkoa wa Mbeya ambao utakuwa na Wilaya za Ileje, Chunya, Mbozi na Momba
ambapo Makao makuu ya Mkoa huo utakuwa Mkwajuni Wilayani Chunya.
Mkoa wa zamani Mkoa wa Mbeya utabaki na Wilaya za
Rungwe, Mbarali, Mbeya na Kyela ambapo Makao makuu yatabaki pale pale Jijini Mbeya.
Kupatikana
kwa jina hilo na mwafaka huo umetokana na Mkutano wa Kamati ya Ushauri
ya Mkoa uliofanyika leo katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya ukiongozwa
na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.
Jina la Mkoa huo Mpya limetokana na uwepo wa Uwanja wa Ndege wa Songwe na
Mto mkubwa unaoitwa Songwe ambao umezipitia Wilaya zote zinazounda Mkoa huo mpya.
Hata
hivyo kuhalalishwa kwa jina na Mkoa huo unategemewa na Mamuzi ya Raisi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete baada ya kupelekewa
mapendekezo hayo ya RCC.
PICHA, HABARI NA MBEYA YETU
...................................................................................................................
Jeshi la Misri limemwondoa madarakani Rais Mohammed Morsi
Jeshi nchini Misri limemuondoa
madarakani Rais aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia nchini humo
Mohamed Morsi na imemteuwa kiongozi wa muda wa nchi baada ya maandamano
makubwa yanayoipinga serikali.
Akihutubia kwa njia ya televisheni
jumatano jioni, mkuu wa jeshi, Abdul Fatah Khalil Al-Sisi alisema katiba
ya Misri imesitishwa kwa muda na mkuu wa mahakama ya katiba ameteuliwa
kuwa kiongozi wa muda nchini humo. Sisi alitangaza kwamba jeshi
linaangalia watu wa Misri kufuatana na maandamano makubwa ya upinzani
yakidai kuwa Rais Mohamed Morsi ajiuzulu.
Kufuatia hotuba ya kwenye televisheni
Bwana Morsi alitoa taarifa kupitia akaunti yake ya Twitter, akiita hatua
ya jeshi ni “mapinduzi kamili”. Aliwasihi wa-misri wote kukataa hatua
ya jeshi lakini pia aliwataka kuwa na amani.
Kiongozi mpya wa muda nchini Misri,
Adli Mansour ana umri wa miaka 68 ni mkuu wa sheria katika mahakama ya
juu ya katiba. Ataapishwa alhamisi.Kusoma zaidi bofya
Kama sehemu ya mwongozo mpya unaoungwa mkono na jeshi kwa nchi, sisi aliutaka uchaguzi wa urais na wabunge, jopo kutathmini katiba na kamati ya mashauriano kitaifa. Alisema mwongozo ulikubaliwa na makundi kadhaa ya kisiasa.
Kama sehemu ya mwongozo mpya unaoungwa mkono na jeshi kwa nchi, sisi aliutaka uchaguzi wa urais na wabunge, jopo kutathmini katiba na kamati ya mashauriano kitaifa. Alisema mwongozo ulikubaliwa na makundi kadhaa ya kisiasa.
Pia aliwasihi watu wa Misri kuepukana
na ghasia. Jeshi lilimpa Bwana Morsi saa 48 kutatua matatizo ya kisiasa
au kuwepo hatari ya jeshi kuingilia kati. Viongozi wa jeshi walisema
wataweka “mwongozo” kama tofauti kati ya serikali ya ki-islam na
wapinzani wake hawatamaliza matatizo yao ifikapo jumatano mchana ya
tarehe tatu mwezi wa saba mwaka 2013. Tarehe hiyo ya mwisho ilipita muda
wake bila ya hatua zozote kuonekana.
Bwana Morsi hakika alikataa wito wa
kujiuzulu na aliapa kuendelea kubaki madarakani hata kama itamsababishia
kifo chake. Pia alilalamika jeshi kutoa kitisho chake cha kuingilia
kati katika matatizo ya kisiasa.
Baruti zilipaa angani kwenye umati wa
watu wanaocheza na kupeperusha bendera katika uwanja wa tahriri Square
mjini cairo, kiini cha ghasia za mwaka 2011 ambazo zilimuondoa Rais wa
muda mrefu nchini Misri, Hosni Mubarak.
Katika wiki ilizopita maandamano yenye
ghasia kati ya wafuasi na wapinzani wa bwana Morsi yameuwa takribani
watu 40. Jeshi la Misri limetangaza kuchukua madaraka ya nchi hiyo huku
likitangaza kuwa si mapinduzi lakini Mohamed Morsi si rais tena wa
Misri. Tayari Saudia Arabia imetuma salamu za pongezi kwa mkuu wa jeshi
la nchi hiyo kwa kluchukua madaraka.
Hali ya rais Morsi ilikuwa ngumu pale
wananchi wake walipoamua kuingia mitaani kumpinga siku chche zilizopita
kwa maandamano baada ya kujitwalia madaraka mengi kiutawala kama
mtangulizi wake................................................................................................
No comments:
Post a Comment