Thursday, July 11, 2013

KAULI YA POLISI KUHUSU CHADEMA KUANZISHA KIKUNDI

DSC 0698 d13fc


                                                                                                Ofisi ya  Inspekta  Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734                                                                                    Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556                                                                                                  S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:                                                                                       DAR ES SALAAM.
10 Julai, 2013


TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI

Mnamo tarehe 09/07/2013, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe, Freeman Mbowe alitoa kauli kwamba wanaunda kikundi chao cha kuwalinda ambacho watakipatia mafunzo ya ukakamavu.

Kitendo cha chama chochote cha siasa ikiwemo CHADEMA kuanzisha kikundi cha kujihami ni kinyume cha sheria za nchi na endapo watafanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Kufuatia kauli hiyo, Jeshi la Polisi nchini limeanza uchunguzi na litachukua hatua kulingana na ushahidi utakaopatikana. Aidha, Jeshi la Polisi litamshughulikia mtu yeyote atakayekwenda kinyume cha sheria bila kujali wadhifa wake.

Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
......................................................................................................................................
 

UTALII WA NDANI;.

Hili Ndilo Gari Mandela Alimkuta Nalo Nyerere Pale Msasani siku alipomtembelea na kumkuta Rais anaendesha mwenyewe gali na akikaa nyumba isiyo ya kifahari


4 27be5


Ndugu zangu,

Leo mchana niliingia na kulikuta gari hilo pale nyumba ya Makumbusho Dar. Itakumbukwa, kuwa Mandela alifika kwa Julius Nyerere Msasani mwaka 1962. Alishangazwa sana kumwona Rais wa nchi anaendesha mwenyewe gari ya kawaida kabisa aina ya Austin( Pichani).

Utotoni kila sikukuu tulikuwa na mazoea ya
kwenda Makumbusho, Magogoni na tulihitimisha kwa kupanda pantoni kwenda ng'ambo ya pili ya bahari; Kigamboni. Hapo ndio siku kuu imekamilika.

Nilipenda sana kuingia Makumbusho ya Taifa. Moja ya sehemu niliyoipenda sana ni kuangalia picha za kumbukumbu ya Dar es Salaam tangu ikiitwa Mzizima. Picha hizo sasa hazipo.

Lakini, nilipenda pia kuangalia magari yaliyotumika na viongozi zamani. Nakumbuka miaka hiyo niliiona Austin hiyo ya Nyerere pichani kuwa bado ilikuwa gari ya maana sana, tena kubwa!

Leo najiuliza, hivi Julius Nyerere, mkewe na watoto walitosha kweli kwenye kigari hicho, au labda walipakatana!

Naam, historia ni mwalimu mzuri.

Maggid,
..............................................................................................................

Post a Comment