Wera wera.....
Nafunguka kuhusu Chadema, sisi tunahitaji uchumi
Dr. Mary Mwanjelwa akiwasisitiza jambo vijana wa mtaa wa Ng'osi kata ya Mwakibete mkoani Mbeya
Kijana Baraka Mwaisumo akieleza jinsi walivyokuwa Chadema na kwa nini wameamua kuhamia CCM
Hapa Dr. Mwanjelwa akiweka mkutano kama darasa ili kila mmoja afunguke
Wananchi waliokuwepo katika mkutano huo wakisikiliza na kushuhudia vijana hao wakizungumza na Mbunge Dr. Mwanjelwa
Pokea kadi
Pokea Laki Moja hii kwa ajili ya ufunguzi wa kikundi chenu na nitawasaidia mkisajili
Tumeamua wenyewe kutoka Chadema wala si kwa kushawishiwa bali tunataka uchumi.
Dr. Mary Mwanjelwa
''Sekretariti''
Burudani hazikukosa katika mkutano huo
Sisi ni vijana tunajitambua
Dr. Mary Mwanjelwa akiwa na mzeeFesto Mlaga na mkewe ambao wamejitolea chumba cha ofisi ya vijana hao ambpo Dr. Mwanjelwa aliwaahidi kuilipia ofisi hiyo ili uwe mradi wa mzee huyo eneo la Ng'osi kata ya Mwakibete mkoai Mbeya.
Asante sana Baba na Mama kwa kuthamini vijana na chama pia.
Tumezipata kadi za UVCCM, hizi hapa
Naenda kufungua shina na kupandisha bendera
Napandisha bendera
Nimefungua shina hili la wakereketwa
VIJANA waliokuwa mashabiki wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wameng'atuka katika chama hicho na kuanzisha kikundi cha ujasiliamali ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM shina la Ng'osi kata ya Mwakibete Jijini Mbeya.
Hali hiyo imebainika jana katika kikao cha pamoja kati yao na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya (CCM) Dr. Mary Mwanjelwa, aliyealikuwa mgeni rasmi katika kufungua tawi la vijana hao eneo la Ng'osi.
Akizungmza kwa niaba ya wenzake, Katibu wa vijana hao Cosmas Mbwembwe, alisema yeye na vijana wenzake walikuwa mashabiki wa Chadema huku wakiwa na matarajio makubwa ya kupata maisha bora na walipojaribu kumshirikisha Diwani wa kata yao Lucas Mwampiki(Chadema) waliambuliwa kutukanwa na kukejeliwa na diwani huyo.
Alisema baada ya kupata majibu hayo, yeye na wenzake waliamua kwa pamoja kuwaendea akina mama wa CCM katika eneo hilo ambao waliwaunganisha na viongozi wa wilaya ambao waliwahakikishia kuwa malengo yao ya kuanzisha shughuli za ujasiliamali zitaungwa mkono na viongozi wa CCM hali iliyowafanya waungane zaidi.
''Tulianza kikundi hiki tukiwa 34 na sasa tupo vijana zaidi ya 69 ambao baadhi tumetoka Chadema na tulikuwa mashabiki maana hata kadi hatukuwa nazo wengi, na kisa kikubwa cha kuondoka Chedema ni kutokana na diwani wa kata hii Lucas Mwampiki kutupuuza katika masuala ya uchumi tukitaka kujiendeleza na kutafuta ufadhili zaidi'' Alisema Mbwembwe.
Lucas Mwampiki akizungumza na Rock FM ya jijini Mbeya, alisema kuwa hizo ni propaganda na hawezi kuwapuuza waliomchagua.
''Tatizo alikuwa anakuja mmojammoja hivyo nilikuwa nashindwa kuwasaidia na ninawaambia wananchi wa Mwakibete wawe na msimamo na waendelee kupokea fedha kutoka CCM'' alisema Mwampiki.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa (NEC) kutoka wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya George Mwanisongole, aliwasifu vijana kwa kuamua kujiunga na CCM kwa kile alichodai kuwa ni chama kinachothamini makabila yote tofauti na vyama vya ukanda.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Mbeya Dr. Mary Mwanjelwa aliwataka vijana kujiamini na kujithamini kwa elimu zao walizonazo ili wasiweze kutumika kisiasa bali wawe na kikundi cha ujasiliamali kitakachowezesha vijana hao kuwa na uchumi imara.
Akifungua shina la wakereketwa la UVCCM Ng'osi, alisema kuwa anawapongeza vijana hao kwa kutambua njia sahihi ya maendeleo na kuachana na Chadema.
Alitoa Shilingi 100,000 kwa ajili ya usajili wa kikundi cha vijana hao na kuahidi kuwapatia vifaa vya michezo na kwamba pindi watakaposajili kikundi hicho cha ujasiliamali ataenda kukifungua na kuwawezesha huku akiwatafutia wafadhili wa kukiimarisha.

........................................................................................................................
UTALII WA NDANI;..
MAGARI MATANO YALIYOWAHI KUTUMIWA NA HAYATI BABA WA TAIFA ENZI ZA UHAI WAKE
Leo
tupo katika utalii wa ndani kwa kutazama baadhi ya magari aliyotumia
Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere wakati wa harakati za Uhuru na baada ya Uhuru mpaka
alipofariki Oktoba 14,1999. Maelezo ya makala haya ni kwa mujibu wa
nyaraka zilizopo Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam hasa kuhusiana na
magari na miaka ya magari yalipotumika. Fuatana nasi.
AUSTIN MORRIS A-40
|
Gari
aina ya Austin Morris A-40 lilitengenezwa nchini Uingereza kati ya
mwaka 1940 – 1950. Ni gari la kwanza kutumiwa na Baba wa Taifa na Rais
wa kwanza Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mwalimu
Nyerere alilitumia gari hilo toka mwaka 1955 – 1960 katika shughuli
mbalimbali za kuendeleza chama cha TANU likiendeshwa na dereva wake
maarufu kwa jina la SAID TANU. Baadaye Mwalimu Nyerere alilikabidhi gari
hilo kwa vijana wa TANU kwa kazi za chama kabla ya kupelekwa Makumbusho
ya taifa na kuwa sehemu ya Historia ya Tanzania.
AUSTIN MORRIS (A-40 VAN GUARDS) |
Gari
aina ya Austin Morris A-40 maarufu kama Van Guards lilitengenezwa kati
ya miaka ya 1945 – 1950. Gari hili lilitumiwa na Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere kwa shughuli za TANU akiwa Dar es Salaam na
ziara za mikoani kuhamasisha shughuli za chama. Dereva wake alikuwa ni
SAID
ROLLS ROYCE |
Gari
aina ya ROLLS ROYCE lilitengenezwa 1938 na kuletwa na Gavana wa wakati
huo Harold Mac Michael katika utawala wa wakoloni waingereza na
lilitumiwa na Gavana wa mwisho kuitawala Tanganyika Sir Richard
Turnbull.
Rolls
Royce lilitumika kupokea wageni mbalimbali waliotembelea Tanganyika
wakati huo wakimwemo Rais wa zamani wa Liberia Hayati William Tubmann na
Mfalme wa zamani wa Ethiopia Hayati Haille Sellasie.
Gari
hilo lilitumika hadi mwaka 1962 baadaye mwaka 1978 Rais wa kwanza
Tanzania Hayati Julius Kambarage Nyerere aliagiza Rolls Royce kuhamishwa
toka Ikulu hadi Makumbusho ya Taifa. Kwa sasa ni sehemu ya Historia ya
Taifa la Tanzania.
ROLLS ROYCE (PHANTOM V) |
Gari
aina ya Rolls Royce Phantom V lilitengenezwa nchini Uingereza na
kutolewa na nchi hiyo kwa Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere Novemba 05,1965.
Rolls
Royce Phantom V lilianza kutumika mwaka 1970 kwa kupokea viongozi wa
nchi mbalimbali wakiwemo Marais na mabalozi wa nchi mbalimbali
waliotembelea Tanzania.
Gari
hilo lina sifa za kipekee kwa wakati huo likionekana la kisasa zaidi
kwani lina sehemu ya mbili za kuweka bendera, moja upande wa kulia
ambako aliketi mgeni na upande wa kushoto bendera ya Tanzania alikoketi
mwenyeji wake (Mtanzania). Sehemu
ya juu ya Rolls Royce Phantom V yaweza kufunguliwa kwa minajili ya
kuwaruhusu viongozi kusimama na kuwapungia mikono wananchi au kuruhusu
hewa kuingia hasa wakati wa joto (hapa ni kama AC/kiyoyozi kwa magari ya
sasa). Kwa kweli tumetoka mbali na huu ndio uhondo wa historia.
Rais
wa awamu ya pili wa Tanzania Alhaji Ali Hassan Mwinyi alilitumia gari
hilo na Rais wa awamu ya tatu Benjamini William Mkapa akalitumia pia
kabla ya kuamua kulipeleka Makumbusho ya Taifa Machi 08,2006 na kuwa
sehemu ya Historia ya Tanzania.
5.MERCEDEZ BENZ 230.6
Mercedez Benz 230.6 lilijulikana kama gari la jumuiya kwani lilitumiwa na Rais wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa shughuli za jumuiya Afrika Mashariki iliyoundwa mwaka 1967 na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda ambapo kila nchi ilikuwa na gari kama hilo.
Moja
ya sifa ya gari hilo kwa wakati huo ni kuwa na uwezo wa kubeba watu
wengi zaidi.Uwezo wake ni kubeba marais wageni wawili, mpambe wa Rais,
mwandishi habari wa Rais na Rais mwenyeji kwa mara moja.
Mercedez
Benz 230.6 lilikuwa na namba za kipekee ambazo ni RE-1 (yaani Royal
Excellecy 1).Hata hivyo Jumuiya ya kwanza ya Afrika Mashariki ilidumu
kwa miaka 10 tu (1967 – 1977) ambapo ilivunjika kwa sababu mbalimbali.
Gari hilo likapelekwa Makumbusho ya Taifa Oktoba mwaka 2002 na kuwa
sehemu ya Historia ya Tanzania.
MERCEDEZ BENZ E 300
|
Mercedez
Benz E 300 lilitengenezwa nchini Ujerumani na kununuliwa na serikali ya
Tanzania Desemba 17, 1996 ambapo Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere alilitumia kwa shughuli za kitaifa na binafsi katika
mikoa ya Dar es Salaam na Pwani baada ya kustaafu Urais.
Mercedez
Benz E-300 litaendelea kukumbukwa zaidi kwani ndilo gari la mwisho kwa
Hayati Mwalimu Nyerere kulitumia enzi za uhai wake hapa nchini kwani
alilitumia kwa mara ya mwisho kabisa Agosti 31,1999 akienda kupata
matibabu huko nchini Uingereza.
Alisafiria gari hilo kutoka nyumbani kwake Msasani hadi uwanja wa kimataifa wa Dar es Salaam (kwa sasa Mwalimu Julius Nyerere).
Hata
hivyo kwa MASIKITIKO MAKUBWA Baba wa Taifa hakurudi tena kulitumia tena
gari hilo kwani alifariki dunia Oktoba 14, mwaka 1999 katika hospitali
ya Mtakatifu Thomas huko nchini Uingereza. MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALA
PEMA PEPONI,AMEN.
Gari lake alilotumia kwa mara ya mwisho (Mercedez
Benz E 300) likatolewa na mkewe Mama Maria Nyerere kwa ajili ya
kuhifadhiwa katika Makumbusho ya Taifa Septemba 24, 2004.
Katika
utalii wa ndani tumeangazia kipengele kidogo tu cha usafiri kwa
kuangalia magari aliyotumia Rais wa kwanza Tanzania Hayati Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere na wenzake hivyo kama Watanzania nadhani kuna
mambo mengi ya kujifunza kupitia utalii wa ndani hasa wa Kiutamaduni na
kuangalia historia mila na desturi za Watanzania kabla na wakati wa
ukoloni hatimaye baada ya Uhuru.
Kuna mambo mengi ambayo Watalii kutoka nchi za nje wanayafahamu kuliko Watanzania wenyewe.Mathalani,
mtu wa Bagamoyo hajui historia ya mji wa kale ya Kaole, Caravan Serai
na mengineyo huku mtu wa Dar es Salaam akishindwa kufika Makumbusho ya
Taifa jijini humo au kijiji cha Makumbusho Kijitonyama kujua Historia
mbalimbali. Vivyo hivyo, Mtanzania anayeishi Mikumi, Kilimanjaro au
Serengeti anashindwa kujua mambo yanayomzunguka huku mtu kutoka
Ujerumani au Marekani anafahamu mengi kuhusu maeneo. Hii ni changamoto
kubwa kwa Watanzania.
Kuna
watu wanasema umasikini wa kipato lakini wale wanaozunguka maeneo hayo
mara nyingi viingilio ni bei ambayo Mtanzania anaweza kumudu mathalani
shilingi elfu miatano (1500) kuingia katika Makumbusho ya Taifa, ukitoka
Magomeni jijini utatumia nauli shilingi 600 kwenda na kurudi maeneo ya
Posta. Ni ukweli usiopingika kuwa uchumi umeyumba kwa wananchi lakini
mwananchi huyo huyo ana uwezo wa kununua bia 3 – 5 kila siku lakini hana
uwezo wa kugharamia shilingi elfu 1500 au 5000 kwa kutembelea kivutio
kimojawapo karibu na anapoishi angalau mara moja kwa mwaka. ….huenda
kuna lingine zaidi ya kipato.
Afisa
Elimu wa Makumbusho ya Taifa Mawazo Ramadhani anasema mwamko wa
watanzania ni mdogo hasa utalii wa kiutamaduni huku akikiri kupokea
makundi makubwa ya wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo na
wageni kutoka nje.
Utalii wa kiutamaduni unahusisha vitu ambavyo mwanadamu anavizalisha kila siku mavazi,mila na desturi za jamii ya watanzania.
Hata
hivyo Afisa elimu huyo amesema katika siku za hivi karibuni wamekuwa
wakipokea watalii wa ndani hasa familia katika siku za wikiendi na
sikukuu jambo linalotia faraja kwa kiasi kikubwa katika sekta hiyo.Kila
laheri kuelekea maadhimisho ya mwaka mpya 2013.
...................................................................................
No comments:
Post a Comment