..............................................................................................................................................
RAIS KIKWETE AWASILI BUKOBA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU SITA
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. Fabia
Massawe baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Bukoba leo tayari
kuanza ziara ya kikazi ya siku sita mkoani humo
Rais Kikwete akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman ambaye pia yuko mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi
Rais Kikwete akisalimiana na Mstahiki Meya wa Bukoba Mhe Anatory Amani
Vijana wa Skauti wa Bukoba wakimlaki Rais Kikwete uwanjani hapo
Kijana wa Skauti akipiga saluti kuomba kumvisha skafu Rais Kikwete
Rais Kikwete akivishwa skafu
Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli. Kushoto ni Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe
Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
Rais Kikwete akisalimiana na viongozi na wananchi waliofika uwanjani kumlaki
Rais Kikwete akisalimiana na Mkuu wa JKT
Rais Kikwete akisalimiana na viongozi wa dini mbalimbali waliokuwepo uwanjani
Rais Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni
Karibu Bukoba mheshimiwa Rais….
Sehemu ya viongozi waliohudhuria sherehe ya kuweka jiwe la msingi la ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba
Waziri
wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe akimkaribisha Rais Kikwete kuongea
na wananchi kabla ya kuweka jiwe la msingi la ukarabati na upanuzi wa
uwanja wa ndege wa Bukoba
Rais Kikwete akiongea na wananchi kabla ya kuweka jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
Rais Kikwete akipata maelezo kabla ya kuweka jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
Rais Kikwete akifunua kitambaa kama ishara ya kuweka jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
Waziri
wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya
Miundombinu Mhe Peter Serukamba wakishangilia wakati Rais Kikwete
akiweka jiwe la msingi
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wadau baada ya kuweka jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
Rais Kikwete akisalimiana na Mhashamu Methodius Kilaini, Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba
Rais Kikwete akiwasili Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
Rais Kikwete akisalimiana na wanachama wa KCU alipowasili Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
Rais Kikwete akisalimiana na wananchi waliofurika kushuhudia ufunguzi wa jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
Rais Kikwete akiendelea kusalimia wananchi
Rais Kikwete akipokea zawadi ya kahawa toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya KCU (1990)LTD John Binushu
Rais Kikwete akifunua kitambaa kama ishara ya Kufungua rasmi jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
Rais Kikwete akihutubia wananchi baada ya Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
Rais Kikwete akihutubia
Rais
Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi wa KCU baada ya kufungua
jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
—————————————————————msajili wa vyama vya siasa aionya CHADEMA
Na Jennifer Chamila,MAELEZO
Msajili
wa vyama vya Siasa nchini amewaasa wanachama na viongozi wa Chama Cha
Democrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutumia muda wao kufanya shughuli za
siasa ili kuchangia maendeleo ya nchi badala ya kutumia uwezo na muda
wao kubuni mambo yanayoleta mtafaruku na kuhatarisha amani ya nchi.
hdg
Pia amepinga tamko la chama hicho la kuanzisha mafunzo ya kujilinda kwa vijana wake nchi nzima.
Kwa
mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jijini Dar es
Salaam na kusainiwa kwa niaba ya Msajili wa vyama vya siasa Sisty
Nyahoza alisema kuwa hajawahi kuruhusu CHADEMA au chama chochote cha
siasa kufanya mafunzo ya ukakamavu au mafunzo ya kutumia nguvu ya aina
yoyote kwa wanachama wake au mtu yeyote yule.
Anaongeza
kuwa CHADEMA wanaruhusiwa kuanzisha vikundi vya kujilinda lakini
hawaruhusiwi kuanzisha mafunzo ya kutumia nguvu kwaajili ya kujilinda
kama walivyo tangaza katika mikutano yao ya hadhara kwani ni kinyume na
Demokrasia na Katiba ya Jamuhuri ya Muungano.
Nyahozo
ametoa ufafanuzi kuhusu vikundi vya ulinzi na usalama vilivyopo katika
Katiba ya Vyama vya Siasa kwamba vikundi hivyo haviruhusiwi kufanya
mafunzo ya kutumia nguvu ya aina yoyote katika kutekeleza majukumu yao.
Bali
wajibu wao ni kutoa taarifa wa vyombo vya Dola pale wanapo sikia au
kuona uhalifu ukitokea na wala sio kupambana na wahalifu au watu
wanaotaka kuwadhuru kama tamko la CHADEMA la tarehe 9 mwezi huu linavyo
sema.
"Hakuna
maelezo yoyote katika Katiba ya CHADEMA yanayoruhusu kutumia nguvu
kufanikisha shughuli za kulinda mali na Viongozi wa Chama.Ni vyema
wananchi wote waelewe kuwa Sheria za Nchi zimeweka masharti maalumu kwa
Vyama Vya Siasa kutokana na umuhimu wa vyama hivi katika kudumisha aman
utulivu na umoja wa Kitaifa", alisema Nyahoza.
Alisema
kuwa kutokana na Ibara ya20(2)C ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1997 inasema kuwa "Bila kujali masharti ya ibara ya
(1) na (4),haitakuwa halali kwa chama chochote cha siasa kuandikishwa
ambapo kutokana na katiba au sera yake:-kinakubali au kunapigani
matumizi ya nguvu au mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya
kisiasa.
Nyahoza
alimaliza kwa kuwataka CHADEMA kuacha kutekeleza mpango walio tangaza wa
kuanzisha makambi ya kufanya mafunzo ya kujilinda kwa vijana wao nchi
nzima,kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria za nchi na endapo
watashindwa kutii agizo hilo hatua za Kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment