Friday, July 26, 2013

SHUKRANI KUTOKA TGNP KWA WAANDISHI WA HABARI

SIKU MAFUNZO TGNP YALIPOFANYIKA MBEYA

MKUFUNZI KUTOKA TGNP

25.07.2013

YAH: KUSHIRIKI NA KUCHANGIA KWAKO KATIKA WARSHA YA WAANDISHI WA
HABARI ILIYOFANYIKA MWEZI MEI, 2013.

Saalam toka TGNP Mtandao,

Mpendwa katika harakati za ujenzi wa vuguvugu la kuwakomboa wanawake
kimapinduzi, tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa ushiriki wako katika
warsha ya waandishi wa habari iliyofanyika mwezi Mei, 2013 katika mikoa ya Mbeya,
Morogoro na Shinyanga.

Tunashukuru pia kwa kuendelea kutumia kalamu zenu kama sehemu ya kupaza
sauti kudai na kupigania haki za wanawake na wanaume hasa walioko pembezoni,
katika kufikia usawa kwa kupambana na mifumo kandamizi ambayo imekuwa
ikiendelea kuwanyonya,kuwanyanyasa, kuwakandamiza na kuwabagua wanawake
na kushindwa kufikia malengo na ndoto zao katika kupata maisha endelevu na
maendeleo kwa ujumla.
Tunaamini kuwa ahadi yako uliyotoa wakati wa warsha itasaidia sana kuwa sehemu
ya kufuatilia, kuchambua, na kuendelea kutoa sauti katika kero mbali mbali
zilizoibuliwa wakati wa mafunzo ya kiraghbishi yaliyofanyika katika baadhi ya Kata
zilizofikiwa lakini pia katika kufuatilia masuala yanayowagusa wanawake na
wasichana kwa mtizamo wa kuwakomboa wananchi wote hasa wanawake na
wanaume walioko pembezoni ndani na nje ya nchi ili kuleta mabadiliko chanya.
Tunaamini kuwa tutaendelea kufanya kazi pamoja kwa kutumia kalamu zenu katika
kuchangia na kuleta mabadiliko ya kuwakomboa wanawake na wanaume hasa
walioko pembezoni
Wako katika mshikamano,
Kenny Ngomuo,


k.n.y Mkurugenzi Mtendaji -TGNP
.................................................................................................

TBL YAKABIDHI KISIMA CHA SH. MILIONI 28 KIJIJI CHA ISNURA, MBARALI, MKOANI MBEYA

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Gulam Kiffu kulia na Meneja kampuni ya bia (TBL)
Nicolaus Kanyamala wakizindua kisima cha kijiji cha Isnura 
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Gulam Kiffu akimtwisha maji mwenyekiti wa kijiji
cha isnura Josephine ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima hicho
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Gulam Kiffu akiwashukuru TBL kwa kusaidia maji
katika kijiji cha isnura na kuahidi kukitunza kisima hicho
Meneja uhusiano wa TBL Dorris Malulu akizungumza na wakazi wa Isnura ambapo amesema kuwa TBL imekuwa na sera ya kusaidia maeneo mbali mbali hapa
 nchini kupitia faida kidogo inayopata kwa kuamua kurudisha sehemu ya faida hiyo
kwa wananchi baada ya kubaini uhitaji wa msaada eneo husika, ambapo pamoja na
mambo mengine meneja huyo alitoa rai kwa jamii kuona umuhimu wa kuisaidia
serikali hapa nchini.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Isnura  Josphine Ndimilage akisoma risala kwa niaba ya wananchi
Uchimbaji wa kisima katika Kijiji hicho umefadhiliwa na Kampuni ya Vinywaji ya Tbl kwa gharama ya Shilingi milion 28  ikiwa ni pamoja na Jenereta ndogo kwa ajili ya kupandisha maji katika
Tanki kubwa lenye ujazo wa Lita 45,000.
Picha na Mbeya yetu

No comments: