Wednesday, August 7, 2013

MGOMO MKALI WA MADEREVA WA COASTER KWA BARABARA YA KYELA, TUKUYU MBEYA NA TUNDUMA MBEYA WASABABISHA ADHA KUBWA NA KUSIMAMA KWA SHUGHURI NYINGI ZA KIUCHUMI


 Gari hili linalodhaniwa kuwa la Serikali nalo lilihusika kubeba abiria 
 Moja kati ya Magari yakingoja kubeba Abiria katika kituo cha Mwanjelwa 
 Noah nazo hazikuwa nyuma
 Moja ya Gari ambalo lilikuwa likingoja kuchukua Abiria
 Askari wa usalama wa Barabarani akisimamia usalama wa Magari na Abiria 
 Abiria wakiwa tayari kwa safari kuelekea wilayani Tukuyu kyela
 Safari ndio hiyooo........... inaendelea
 Moja kati ya Magari ambalo nalo lilikuwa likingojea kubeba Abiria
 Gari hii kubwa aina ya Fuso nalo Lilikuwa linatoza nauli kwa Tsh 4000 mpaka Tukuyu
 Makubwa haya... Hata Gari za nje ya Nchi nazo zilikuwa zikifanya Biashara
Hawa  Abiria wote wapo tayari kuwachukua Abiria.....

Ezekiel Kamanga
Shughuli za kiuchumi kwa Wakazi wa Mkoa wa Mbeya Leo zilisimama kwa siku nzima hususani kwa wasafiri wanaotumia usafiri wa mabasi aina ya Coaster baada ya madereva ma mabasi hayo kugoma.
Kutokana na hali hiyo ya mgomo huo shughuli za kiuchumi zilidorora kwa kiasi kikubwa  na baadhi yao kushindwa kwenda kazini baada ya madereva na wamiliki wa vyombo hivyo kushindwa kutokea barabarani na kuleta adha kubwa.

Hata hivyo ililazimu kupatikana njia ya dharua ambapo maroli yalilazimika kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo kwenda Wilaya za Kyela,Mbozi,Rungwe na Tunduma wilaya ya Momba.

Hali hiyo ilipelekea kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kukutana kwa dharula ili kupata mustakabali wa suala hilo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na Umoja wa Madereva wakiongozwa na chama cha wasafirishaji.

Madereva hao walimshukia lawama Meneja wa SUMATRA Mkoa kuwa ndiye chanzo kwa kuwatoza faini kubwa na wakati mwingine fedha wanazolipa kutopatiwa stakabadhi hali inayotia shaka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wasafirishaji Bwana Ezekiel Mwakapala amesema kuwa wao hawajagoma bali wameona ni afadhali kutotoa magari barabarani kuliko kutoa pesa nyingi kwa SUMATRA.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Diwani Athuman amesema hajafurahishwa na kitendo hicho kwani migogoro inatatuliwa kwa njia ya mazungumzo na kitendo cha kugoma kinawaumiza wananchi wasio na hatia.

Kamati ya ulinzi na usalama iliuagiza uongozi wa wasfirishaji abiria kuleta malalamiko yao ili yaweze kushughulikiwa na kupata ufumbuzi wa kudumu.

Baadhi ya wenye maroli walifurahia huduma hiyo wakidai kuwa magari yao yalikuwa yakiegeshwa bila bila kazi kutwa nzima na kwamba nauli zilikuwa zikitozwa kati ya shilingi elfu tatu hadi elfu kumi kutoka Mbeya kwenda Kyela au Mbeya kwenda Tunduma na Jeshi la Polisi liliimarisha usalama barabarani kuhakikisha wasfiri hawapati bughudha yoyote njiani.

Baada ya kikao kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa madereva na wamiliki wa vyombo hivyo walikuwa wakikutana katika ofisi zao zilizopo ofisi za nane nane.
....................................

No comments: