Wednesday, August 7, 2013

MMANDA AWATAKA WAJUMBE WA TUME YA KATIBA KUACHA KUFANYA KAZI YA KUJIBU MAPUNGUFU YALIYOMO KATIKA RASIMU YA KATIBA

3 
NA SULEIMAN MSUYA
MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (MNEC) Wakili Evod Mmanda amewataka Wajumbe wa Tume ya Katiba kuacha kufanya kazi ya kujibu mapungufu yaliyopo katika rasimu hiyo kwani huu ni wakati wa Mabaraza kufanya kazi ya kurekebisha na kupendekeza.
Mmanda alitoa kauli hii wakati akiongea na mwandishi wa habari hii jana jijini Dar es Salaam ambapo alisema ameshuhudia baadhi ya wajumbe wa Tume wakitoa maelekezo kwa wajumbe wa mabaraza jinsi ya kutoa maoni.
Alisema ni vema Tume hiyo ikatambua kuwa wakati wao wa kuandaa rasimu umepita na sasa ni wakati wa kuyapa fursa mabaraza kutokana sheria inavyotaka jambo ambalo ni muhimu kuheshimiwa.
Mjumbe huyo wa Mkuatano Mkuu alisema CCM wanaamini kuwa fursa zikipatikana upo uwezekano wa kupatikana na kwa katiba ambayo itakuwa na maslahi na Taifa hivyo kuingilia maoni ya watu ni kinyume na katiba inavyotaka.
“Napenda kutumia nafasi hii kuwaasa wajumbe wa Tume ya Katiba kuwa wakati huu ni wakuwaachia wajumbe wa mabaraza kutoa maoni na mapendekezo yao hivyo kukaa na kujibu hoja hizo wakati wanatakiwa kusubiri ni kwenda kinyume na sheria inayowaongoza,: “ alisema.
Mmanda alisema iwapo wajumbe watatumia nafasi elekezi kuwashawishi wajumbe wa mabaraza kukubaliana na mapendekezo yao ni dhahiri kuwa kutakuwepo na katiba ambayo ina mitazamo ya watu wachache.
Alisema kuna mapungufu mengi ambayo yameonekana katika rasimu hiyo hivyo ni wakati muafaka kwa jamii na vijana kwa ujumla kutumi nafasi zao kutoa maoni ambayo yataweza kusaidia kizazi cha leo na kijacho.
Mjumbe huyo ambaye alionyesha dhahiri kutokuunga mkono wa uwepo wa Serikali tatu aliishutumu tume kwa kuweka maoni hayo kwa kile alichodai kuwa haikuwa sehemu ya muuongozo wao kufanya.
Aliweka bayana kuwa yeye ni muumini mkuwa wa serikali mbili hivyo hakuona sababu ya kuwepo mapendekezo juu ya aina ya muungano na kuwataka wachangiaji kupitia nafasi mbalimbali kuwa makini kwa maslahi ya Taifa.
Mmanda alitoa rai kwa vijana wa CCM kuwa watumie nafasi yao kuhakikisha kuwa katiba ijayo inakuwa na maboresho yesnye tija na kuacha tabia ya kuwa katika mitazamo ya watu amabao wanaweza kuwa na maslahi yakiuongozi.

..................................................................

Kenya’s main airport, JKIA on fire


K1 03646
K2 c552c
K3 1a99f
NAIROBI, Kenya Aug 7 – Operations were grounded at Kenya's main airport, JKIA on Wednesday following a major fire that broke out at dawn, authorities said, adding flights were being diverted to other airports."There is a serious fire at JKIA, but we are doing everything possible to avert a crisis," Interior and Coordination of National Government Principal Secretary Mutea Iringo said.
His office also posted on twitter "A serious fire at JKIA kindly take caution."
Fire fighters were battling the inferno.
Witnesses said they had seen a huge smoke billowing from the international arrivals and departure areas, but there were no immediate reports of casualties.

  .................................................................

AJALI MBAYA YATOKEA MSWISWI MBEYA MMOJA AFARIKI PAPO HAPO

GARI AINA YA TOYOTA COROLLA  ILIYOGONGANA NA BASI LA HOOD MENEO YA MSWISWI MBEYA DEREVA WA GARI NDOGO AMEFARIKI PAPO HAPO
HATI YA KUSAFIRIA YA MAREHEMU DAVIS HANAMUNDE MZAMBIA
Picha zote na Mbeya yetu Blog


MNAMO TAREHE 04.08.2013  MAJIRA YA SAA 06:45HRS HUKO MSWISWI WILAYA YA MBARALI BARABARA YA MBEYA/IRINGA, GARI NO T. 159 AXM AINA YA SCANIA BUS MALI YA KAMPUNI YA   HOOD LIKIENDESHWA NA DEREVA OMARY  SAID, MIAKA 50, MZIGUA, MKAZI WA MABIBO DSM LILIGONGANA NA GARI NO IT.3014 TOYOTA COROLLA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA DEVIS  ANAMUNDE, MIAKA 28, MZAMBIA MKAZI WA MUNZE LUSAKA NA KUSABABISHA KIFO CHA DEREVA HUYO PAPO HAPO.

 MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA MAGARI YOTE MAWILI NA DEREVA WA HOOD BUS AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHANA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

No comments: