Wednesday, August 14, 2013

Mwakyembe aahidi kuendelea na vita

mwakyembe1 8bd7f
Waziri wa uchukuzi wa Tanzania Dkt. Harrison Mwakyembe amehaidi kufichua mtandao wa waliohusika na usafirishaji wa madawa ya kulevya yaliyokamatwa katika uwanja wa ndege wa Johanesburg,afrika kusini julai 5 mwaka huu.

Waziri Mwakyembe alisema hayo hii Jumatano alipofanya ziara ya ghafla katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam ili kujionea namna mamlaka mbalimbali za uwanja zinavyofanya kazi za kupitisha abiria na mizigo.
Dkt.Mwakyembe amesisitiza kwamba suala la madwa ya kulevya limechafua jina la Tanzania kimataifa kwani watanzania wengi wamekuwa wakishikiliwa katika mataifa mbalimbali kwa tuhuma za kukamatwa na madawa ya kulevya .

Julai 5 mwaka huu watanzania wawili Agness Gerald na mwenzake Melisa Edward walikamatwa na kuhusishwa na kusafirisha dawa za kulevya za uzito wa kilo 150 zilizokuwa katika mabegi 6 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Or Thambo Afrika Kusini mabegi ambayo yalipita siku hiyo majira ya alfajiri katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere bila ya kukamatwa.

Dkt. Mwakyembe amesisitiza kwamba suala la madawa ya kulevya limechafua jina la Tanzania kimataifa kwani watanzania wengi wamekuwa wakishikiliwa katika mataifa mbalimbali kwa tuhuma za kukamatwa na madawa ya kulevya.

 ...............................................................

BAKWATA YATAKA TUKIO LA KYELA LIFANYIWE UCHUNGUZI

images 08607
NA JENNIFER CHAMILA – MAELEZO
BARAZA Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) limeviomba vyombo vya dola kuendelea kufanya uchunguzi kuhusu tukio la kuvamiwa,kupigwa na kujeruhiwa kwa Imamu na waumini wa Kiislamu wakiwa msikitini wakati wa swala ya Idd-el-Fitri iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya na kuhakikisha
hdg

Aidha baraza hilo limesikitishwa na kitendo hicho, na kuvitaka vyombo hivyo kuhakikisha kwamba wahalifu wote wanafikishwa mbele ya sheria.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kwa kwa vyombo vya habari na Mufti wa Tanzania Sheikh Issa Simba,imelaani kitendo hicho na kusema watu waliofanya kitendo hicho wamegeuka maagizo ya ya Qur'an Tukufu pamoja na Sheria za Nchi.

"BAKWATA imewataka wananchi wote kufuata taratibu sahihi jambo lolote linapo tokea."Kama yupo mtu yoyote ana manung'uniko au hoja yoyote dhidi ya mwenzake au taasisi yoyote,ni lazima watumie taratibu sahihi za kidini au za kisheria na sio kuchukua sheria mkononi"alisema Sheikh Issa.
Alisema baraza hilo linamuomba Mwenyezi Mungu awaponye watu wote waliathirika na tukio hilo.
.............................................................................

RAIS DKT. KIKWETE APOKEA ZAWADI YA JEZI NAMBA 10 KUTOKA BARCELONA, ANAYOVAA NGULI MESSI KUTOKA!!

t5 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Kushilla Thomas akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete jezi iliyosainiwa na wachezaji wote wa timu ya FC Barcelona Ikulu jijini Dar es salaam jana ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuendeleza soka na ikiwa ishara ya kutambua ushirikiano wa kihistoria kati ya Castle Lager na FC Barcelona uliosainiwa hivi karibuni huko Camp Nou Hispania. Wanaotazama ni Meneja Mauzo wa TBL Kanda ya Kusini James Bokella (wa kwanza kulia) na Meneja Masoko wa TBL Bi. Natalia Celani (wa pili kulia). Na kushoto ni Meneja wa Castle Lager, Kabula Nshimo na Aggrey Marealle, Mkurugenzi wa Executive Solutions washauri wa mahusiano wa TBL. (Picha ya Ikulu)
t6 t8 
Rais Dktk. Jakaya Mrisho Kikwete, Mpenzi mkubwa wa michezo  amepewa zawadi ya Jezi namba 10 ya mwanasoka bora  wa FIFA mara nne mfululizo, mshambuliaji wa Barcelona, Raia wa Argentina, Lionel Andrew Jorge Messi

No comments: