Monday, August 19, 2013

RAIS KIKWETE AMFARIJI MZEE PHILIP MANGULA KWA KUFIWA NA BINTI YAKE

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Profesa Mark Mwandosya alipoenda kumfariji  Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mangula kwa kufiwa na binti yake, Nemela Mangula, aliyefariki mwishoni mwa juma kwa ajali ya gari. Hapa ni nyumbani kwa Mzee Mangula Oyterbay jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2013 ne3 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi kitabu cha maombolezo alipoenda kumfariji  Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mangula kwa kufiwa na binti yake, Nemela Mangula, aliyefariki mwishoni mwa juma kwa ajali ya gari. Hapa ni nyumbani kwa Mzee Mangula Oyterbay jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 20 ne4 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pole Mama Mangula alipoenda kuifariji familia ya Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mangula  kwa kufiwa na binti yake, Nemela Mangula, aliyefariki mwishoni mwa juma kwa ajali ya gari. Kulia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Anne Makinda. Hapa ni nyumbani kwa Mzee Mangula Oyterbay jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 20 ne7 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mangula na familia yake kwa kufiwa na binti yake, Nemela Mangula, aliyefariki mwishoni mwa juma kwa ajali ya gari. Anayefuata ni Profesa Mark Mwandosya, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Jordan Rugimbana na Bw. Ali Kikwete  Hapa ni nyumbani kwa Mzee Mangula Oyterbay jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 20 ne8 
Mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula, Neema Mangula (25) amefariki dunia juzi usiku kwa ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Aga Khan Wilayani Ilala. Alikumbwa na mkasa huo wakati akitokea kwenye sherehe ya harusi iliyokuwa ikifanyika katika Ukumbi wa Waterfront uliopo Gerezani.

Akizungumzia tukio hilo, baba wa marehemu, alisema kuwa Neema alipoteza maisha muda mfupi baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Aga Khan ambako aligundulika kuwa alikuwa amepata majeraha ya ndani.

"Neema alikuwa anatoka kwenye harusi na alipofika maeneo ya Aga Khan, alipunguza mwendo kupisha gari lingine lililokuwa mwendokasi, lakini alimfuata upande wake, wakagongana uso kwa uso," alisema Mangula.

"Baada ya kupata ajali hiyo muda wa saa tano usiku alikimbizwa hospitali na baadaye nilikwenda kumtembelea kama kwenye saa 8 usiku. Niliambiwa kuwa alikuwa anavuja damu kwa ndani na ndiyo iliyosababisha kifo chake," alisema Mangula na kuongeza: "Msiba uko hapa Oysterbay na tunatarajia kuzika keshokutwa," alisema

No comments: