Saturday, August 17, 2013

RUNGU LAWASHUKIA MTANDAO ULIOSAIDIA KUSAFIRISHA MADAWA YA MASOGANGE

SONY DSC 
Waziri wa uchukuzi Mh. Dkt.Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari leo  ofisini kwake jijini Dares salaam juu ya hatua zilizochukuliwa na wizara ya uchukuzi  juu ya sakata la madawa ya kulevya yaliyokamatwa huko afrika kusini hivi karibuni.
Mwakyembe amewafukuza kazi mtandao mzima uliohusika kusaidia kusafirisha madawa hayo, pia ameliagiza jeshi la polisi kuwakamata wafanyakazi hao na kuwaunganisha na wenzao kujibu mashitaka ya jinai.
SONY DSC 
Waziri wa uchukuzi akionyesha picha ya msanii Agness Gelard maarufu kwa jina la Masogange mbele ya waandishi wa habari. Masogange alikamatwa na madawa ya kulevya huko afrika kusini.
SONY DSCWaandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa uchukuzi 


Sakata la kusafirisha madawa ya kulevya kwenda Afrika kusini limechukua sura mpya baada ya Waziri mwenye dhamana ya uchukuzi hapa nchini Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe kuchukua hatua kali dhidi yao ikiwamo kuwafukuza kazi mtandao mzima uliohusika kusaidia kwa namna moja ama nyingine upitishwaji wa madawa hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Waziri Mwakyembe amebainisha baadhi ya ushahidi uliotumika kugundua mtandao mzima uliohusika kusaidia kusafirisha mzigo huo wa madawa ya kulevya katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius kuwa ni kamera zilizofungwa katika uwanja huo
Dkt. Mwakyembe aliwataja waliohusika kusafirisha mzigo huo, kuwa ni pamoja na askari wa polisi, CPl Ernest ambaye alionekana akiwa bize na kuonesha kila dalili ya kusaidia kusafirisha mzigo siku hiyo
Wengine ni walinzi wa uwanja huo ambao ni Yusuph Isa, Jackson Manyoni, Juliana Thadei na Mohamedi Kalungwana ambao wote kwa pamoja walisaidia kusafirisha madawa hayo na hivyo Waziri kumuamuru muajiri wa wafanyakazi hao kuwafukuza kazi mara moja na wasikanyage uwanja wa ndege
Pia askari ambaye amehusika na kula njama za kusafirisha madawa hayo Waziri  amelitaka jeshi la polisi kumshughulikia askari huyo ipasavyo na kwamba wizara inatarajia askari huyo hawezi kukanyaga tena uwanja wa ndege

........................................................................ RAIS KIKWETE ATUA MALAWI LEO KUHUDHURIA MKUTANO WA VIONGOZI WAKUU WA NCHI ZA SADC MJINI LILONGWE

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Rais Joyce Banda wa Malawi muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Lilongwe tayari kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za SADC
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mtoto muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Lilongwe tayari kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za SADC
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana nawakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama muda mfupi baada ya kuwasili Lilongwe Malawi kuhudhuria Mkutano wa SADC
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenyeji wake Rais Joyce Banda muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Lilongwe tayari kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za SADC
                                          Picha na Fred Maro
 

No comments: