Wakati
msafara wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ukielekea Wilayani
Missenyi kukagua sehemu utakapojengwa uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa
Omukajunguti, gari aina ya Costa lenye namba za usajili T 570 BYU
lilowabeba Waheshimiwa Wabunge 11 lilipata hitilafu na kutaka kuungua.
Ajali
hiyo ilitokea eneo la Mwanzo Mgumu kilometa moja kutoka mpakani mwa
Wilaya ya Bukoba na Wilaya ya Missenyi ambapo gari hilo aina ya costa
lilianza kutoa moshi mwingi kwa upande wa nyuma wakati likiwa kwenye
mwendo mkali na kuleta hofu kubwa kwa abiria walikuwemo ndani ya gari
hilo.
Mara baada ya dereva kugundua kuwa
gari analoendesha linataka kuungua alilisimamisha na kuwaambia abiria
wake kuwa gari linaungua.
Kwa
mujibu wa wabunge waliokuwemo kwenye gari hilo, baada ya kuambiwa kuwa
gari linaungua kila mmoja alifanya juhudi za kujiokoa, wengine wakipitia
madirishani.
Kwa Bahati hakuna Mbunge aliyeumia isipokuwa Mhe. Batenga aliumia mkono kidogo baada ya kubanana sana mlangoni.
Baada ya kila mmoja kutoka gari hilo
liliendelea kutoa moshi mzito sana lakini kwa halikushika moto na baadae
lilizimika na kuacha kutoa moshi.
Wabunge
waliokuwemo katika gari hilo ni Rebbecca Mngondo (Arusha Viti Maalumu),
Rita Kabati (Iringa Viti Maalumu), Mariam Msabaha (Zanzibar Viti
Maalumu), Mhe. Batenga (Kagera Viti Maalumu), Mhe. Madabida (Dar es
Salaam Viti Maalum), Clara Mwatuka (Mtwara Viti Maalumu).
Wengine ni Mzee Hussein (Zanzibar),
Mussa Haji Kombo (Pemba Zanzibar), Abdul Mteketa (Jimbo la Kilombelo),
Mutula Mutula (Jimbo la Tunduru Kusini).
Aidha Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Peter Serukamba Hakuwemo katika gari hilo lilotaka kuungua.
............................................................................................
kijana akamatwa na dawa za kulevya.
Waziri wa
Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akionesha picha ya kijana Leonard
Jeremiah Monyo ( Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za
madawa ya kulevya aina ya heroine
JUHUDI za Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe za kupambana na dawa za kulevya nchini Tanzana zimeanza kuzaa matunda baada ya jana akiwa katika ukaguzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Julius Nyerere kunaswa kijana akijaribu kupita na dawa za kulevya katika uwanja huo.
Kwa kile kuoneshwa kukerwa na tabia hizo, Dk. Mwakyembe amempiga picha kijana huyo ambaye ni rasta na pita yake itasambazwa maeneo tofauti, huku kesi yake ikiendelea ya kupatikana na madawa hayo ya kulevya.
Akizungumza na vyombo vya habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Dk. Mwakyembe alimtaja kijana aliyekamatwa jana kuwa ni Leonard Jeremiah Monyo (Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete 86 za madawa ya kulevya aina ya heroin akitaka kusafiri nazo kuelekea misokoto ya bangi 34 akiwa ameficha kwenye begi lake.
Alisema kijana huyo rasta alinaswa na mtambo wa kukagua mzigo baada ya wakaguzi kuushuku mzigo wake hivyo kuamuru ukaguliwe ndipo alipokutwa na madawa hayo haramu akijaribu kusafiri nayo kwa ndege.
Alisema kijana huyo kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kukutwa na dawa hizo haramu. Alisema kwa kile kuoneshwa kukerwa na vitendo hivyo na kuamua kwa dhati kupambana navyo wamempiga picha kijana huyo na picha zake zitasambazwa maeneo mbalimbali ili aonekane na umma kujua watua ambao wamekuwa wakilichafua taifa nje na ndani kutokana na biashara hizo haramu.
Dk. Mwakyembe amesema atahakikisha anafuatilia kesi ya kijana huyo hadi itakapoishia ili uona hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wahusika na vitendo hivyo kukomeshwa. Alisema maofisa wakaguzi wa mizigo wawili (wote wasichana) ambao walimnasa kijana huyo watazawadiwa na kupandishwa daraja kutokana na kazi nzuri waliyoifanya.
"Jana tu baada ya ukaguzi wenzetu ambao wanaona kama tunafanya mzaha jana tena wakapitisha mzigo wa madawa ya kulevya kiwanja cha ndege cha Dar es Salaam, kwa sababu vijana wetu sasa wameamka na hawataki mchezo wakamkamata kijana huyo...," alisema.
"Picha yake itasambazwa kila sehemu...sidhani kama tunahitaji upelelezi kwa sababu tumekukamata na dawa za kulevya. Mimi na viongozi wangu kupitisha dawa za kulevya akikisha kuuhakikisha.
Alisema kijana huyo alikamatwa majira ya saa mbili na nusu usiku akiwa anasafiri kwenda nchini Italia kwa kutumia ndege ya kampuni ya Swissair. Alisema kwa sasa kila atakayekamatwa na dawa za kulevya picha yake itasambazwa maeneo mbalimbali ya nchi ili watu hao wajulikane.
Alisema kwa sasa taratibu zinafanywa ili kuhakikisha mizigo ya abiria wanaowasili kutoka nje ya nchi kuingia Tanzania nao mizigo ikaguliwe ili kuwabaini wanaoingiza bidhaa hiyo haramu ichini pia. Aliongeza zoezi hilo litafanyika katika viwanja vya ndege na bandarini kwa kila mizigo inapowasili.
Alisema lengo ni kuhakikisha viwanja vya ndege vinakuwa salama na kuacha kutumika vibaya na baadhi ya watu, jambo ambalo limeendelea kulichafua taifa. Alisem kiwanja cha Dar es Salaam ni kizuri na kina vifaa vya usalama vya kutosha ila mapungufu yaliyopo ni kwa baadhi ya wafanyakazi ambao wanatumia vibaya madaraka yao.
Dk. Mwakyembe ameahidi kuwataja na kuweka picha zao hadharani watu ambao wanajihusisha na madawa hayo ya kulevya. Amesema wanatarajia kutaja majina ya Watanzania ambao hivi karibuni walinaswa na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo. Alisema Watanzania wengine wamekamatwa Hong Kong wakihusishwa na dawa hizo na wanafuatilia pia picha na majina yao yatawekwa hadharani muda wowote.
.........................................................................
KIJANA ALIYEKAMATWA NA MWAKYEMBE
Siku moja baada ya ziara ya kushtukiza
ya waziri wa uchukuzi Dk. Harison Mwakyembe, kwenye uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar-es-Salaam, kiasi kikubwa cha dawa
za kulevya kimekamatwa uwanjani hapo katika harakati za kusafirishwa
kwenda nchi za nje.
No comments:
Post a Comment